AMBAO hawajibiwi
maombi yao wametakiwa kuanza upya kuomba kwa
kuwa wapo ambao hawajibiwi maombi yao kwa kuwa
wanaomba maombi ya kukomoa na wala sio maombi ya unyenyekevu kama
ambavyo Mungu aliagiza katika maandiko yake
Rai hiyo imetolewa na mchungaji Joseph Msengi alipokuwa
akiongea na waumini wa kanisa la FPCT
Miembeni Usa River Wilayani Meru Mkoani hapa mapema wiki iliyopita
Mchungaji Msengi alisema kuwa watu wanatakiwa kujua jinsi ya
kuomba kwa Mungu na hata kama maombi
hayajibiwa hawapaswi kwenda kinyume cha mapenzi
kwa kuwa Mungu ana makusudio ya kila hitaji na kila ombi
“kuna watu ambao wanaomba maombi kwa kejeli mbele za Mungu
na maombi ambayo wanayaomba ni maombi ya hasira kwa kuwa baadhi ya wengine pia
wanaomba kwa kuwa baadhi ya majirani au ndugu zao wamefanikiwa sasa je tunampangia Mungu kazi
za kufanya jamani’aliongeza mchungaji huyo
Pia alisema kuwa kwa wale ambao hawajajibiwa wanatakiwa
kuacha kuomba kwa hasira au kutoa maneno ambayo yanamfanya kazi za Mungu ziwe
chini na badala yake wanatakiwa kuangalia ni yapi mapendekezo ya Mungu katika
maisha ya kila siku ili maombi yajibiwe kwa haraka sana.
Hataivyo aliongeza
kuwa ni vema hata wakristo wakahakikisha wanafuatilia kwa karibu sana matakwa ya Mungu
hasa kwenye biblia ambapo ndio muongozo wa maisha ya kila siku ingawaje kwa
sasa biblia zinaoneka kubebwa kwa muda wa mara moja kwa wiki
‘jamani basi tuhakikishe kila sekunde na dakika tunaangalia
mapenzi ya Mungu na kwa maana hiyo ukiangalia hata ndani ya makanisa yetu
yeyote yule ambaye anafuatilia kwa karibu sana biblia hayumbi na imani wala
haombi kwa hasira sasa kwa maana hiyo kwa nini tunaacha hili na kujiongoza
wenyewe hii ni mbaya sana na ukiwa hivi utaoimba mpaka ‘alisema mchungaji
Msengi.
Aliwataka wakristo kuhakikisha kuwa wanajitafakari kwa kina
na kuanza kuomba hata toba hasa kwa wale ambao wanaomba maombi ya hasira ya
kulipizana mali
na vitu vya kidunia kwani maombi ya hasira ndio chanzo pekee cha kushindwa
kujibiwa
MWISHO
No comments:
Post a Comment