,ARUSHA
WITO umetolewa kwa makanisa mbalimbali hapa nchini
kuhakikisha kuwa yanajiwekea utaratibu wa kuombea mapato ya wafanyakazi wake
kwa kuwa wengi wamekuwa wakipoteza hata haki zao za msingi
Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na mchungaji Joel Kessoi katika kanisa la Ngome ya Yesu lilopo Kisongo
Aidha mchungaji huyo alisema kuwa kwa sasa maslahi ya
wakristo wengi sana
wanaibiwa ovyo kwa kuwa baadhi ya waajiri wanashindwa kuwalipa na baadaye
wakristo hao wanaishia kuteseka
Alisema kuwa endapo kama
kanisa litasimama katika nafasi yake na kuanza maombi yake basi waajiri hasa wa
viwanda ambao wananyima haki zao na
badala yake kuanza kuwakata wafanyakazi makato ambayo hayastaili.
“ukiangalia hawa wafanyakazi wa Viwanda kila siku wanalia na
shida lakini wa nahaki sana ya kuweza kufanya kazi zao na kupewa wanachokitaka
lakini kwa sasa kazi zao nyingi sana zimeingiliwa na shetani na wanakatwa hata
makato ambayo hayastaili kwa kweli”aliongeza mchungaji Joel
Pia alisema kuwa kama kanisa litaendelea kuangalia suala hilo ambalo ndilo chanzo cha umaskini wa makanisa ya leo
basi nafasi ya maombi inatakiwa kuanza kutumika katika kuombea wafanyakazi na
makato yao
Alifafanua kuwa kwa kuanza kanisa hilo
limeanza na mchakato wakuombea
wafanyakazi wa kiwanda cha A- Z ambao nao wamekatwa sana makato mengi ambayo hayana faida na wafanyakazi
Alisema kuwa kila mara watakuwa wanaombea wafanyakazi wa
makampuni na viwanda mbalimbali katika maombi maalumu ili wawezen kufikia
malengo yao ya
msingi ambayo wamejiwekea na kuacha kuonewa hasa wakati wa kupewa haki zao
MWISHO
No comments:
Post a Comment