WILAYA YA MERU KUANZA
KUWAPA VIJANA FURSA ZA KUIMARISHA UCHUMI WAO
WILAYA ya Meru Mkoani Arusha inatarajia kuanza kuwapa vijana
wote wa Wilaya mbinu mbalimbali za kuweza kujikomba dhidi ya umaskini ambapo
mbinu hizo zitachangia sana vijana kuacha
kulalamika na kuona kama Serikali imewatenga
huku wilaya hiyo ikiwa ni miongoni mwa Wilaya zenye rasilimali nyingi.
Hayo yamebainishwa
wilayani humo na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw Munasa Nyirembe wakati wa zoezi la
kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Bi Mecy Silla mapema jana Wilayani humo
Bw Munasa alisema
kuwa mpaka sasa kuna kila dalili za kuweza kuokoa uchumi wa kijana wa Meru kwa
kuwa vitenda kazi muhimu vikiwemo Ardhi vipo vya kutosha na kutokana na hali
hiyo sasa Serikali imeshajiwekea utaratibu a kuhakikisha kuwa vijana wanaanza
kunufaika mapema hivi sasa
Alifafanua kuwa mbali na hilo pia wilaya hiyo itaaza kwa kuwapa mawazo
ya kijisariamali vijana wa maeneo hayo ambapo zoezi la kuwapa mawazo pia
litaenda sanjari na zoezi la kuwakuzia zaidi Uchumi wao kwa kupitia fursa
mbalimbali ambazo wanazo
“tunaamini kuwa hawa vijana wa hapa Meri wakipatiwa hata
elimu ya ujasiamali basi wataweza kujikomboa na Maisha mabaya ambayo wengi
wanaishi huku fursa nazo zikiwa ni nyingi sana na kutokana na hali hiyo basi
tunataka kuona kuwa kila kijana anapiga hatua kwenye uchumi na mtu wa kuweza
kuwasaidia ni sisi Serikali kwa kuwa hata wanapofanya maovu sisi ndio tunakuwa
katika heka heka Sasa kila mmoja wetu akikishe kuwa anakuwa na mchanganua hata
wa idadi ya vijana aliona na kisha aweze kufikiri pamoja nasi”aliongeza Bw Munasa
Pia alisema ili kuendelea kuboresha zaidi maisha ya vijana
ambao ni wazawa wa Meru kuanzia sasa wawekezaji wote wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanaachana na tabia ya kutoa ajira kwa vijana wan chi za nje na kuaawacha
vijana wa Kimeru wakiwa wanaranda randa Mitaani
Alifafanua kuwa kila muwekezaji ndani ya Wilaya hiyo
anatakiwa kuanza utaratibu wa kuhakikisha kuwa vijana wananufaika na utendaji
kazi wao na kutokana na hilo pia litachangia sana maendeleo na hata
uchumi wa Wilaya ya Meru
“Nawasihi sana wawekezaji
ambao wapo kwenye wilaya hii ya Meru kuhakikisha kuwa wazawa ambao ni vijana
wananufaika na uwekezaji wao ni vema hata wakarudisha fadhila kwa vijana kwa
kuwa wanapowachukua wafanyakazi kutoka nje ya nchi je hawa vijana waende wapi kama sio kuwaonea jamani”Aliongeza Bw Munasa
Awali aliye kuwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye kwa sasa ni mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga bi Mecy Silla
alisema kuwa hilo linatakiwa kuchukuliwa kama changamoto na watu wote ndani ya Wilaya hiyo kwa kuwa
vijana ndio taifa la kesho.
No comments:
Post a Comment