Na Mwandishi wetu, Arusha
Chama
cha mapinduzi (CCM)kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha chama cha
demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye chaguzi zake
huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia
sifa na umaarufu pekee kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni
Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za
udiwani katika kata ya sombetini mapema jana.
Mwigulu
alisema kuwa CCM inashangaa sana Chadema kutumia Helikpota kwenye
chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa wanatumia
gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama ambazo zinatumika
hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya Milioni 200.
Alisema kuwa Gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa
Helkopta ni gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama wao lakini
hata matumizi mbalimbali ya chama hicho ambacho bado kinaonekana
kukabiliwa na changamoto nyingi sana
Pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki
kwenye siasa za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine
zinasababisha hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo
Awali Mgombea Udiwani katika kata hiyo ya Sombetini kwa tiketi
ya CCM alisema Bw David Mollel alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya
kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo endapo kama atapata ridhaa ya
kuongoza rasmi kama diwani
David alisema kuwa changamoto ambazo atahakikisha kuwa ameweza
kuzitatua ni pamoja na urekebishaji wa barabara, uboreshaji wa masoko,
kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake na jamii kwa ujumla.
MWISHO
No comments:
Post a Comment