Monday, June 18, 2012

DOLA BILIONI 148 ZINAPOTEA KILA MWAKA KUTOKANA NA RUSHWA NDANI YA NCHI ZA AFRIKA


.

IMEELEZWA  kuwa kiasi cha dola za Kimarekani Bilion 148huwa zinapotea ndani ya Nchi za bara la Afrika kila mwaka kutokana na kuwepo kwa mianya mingi ya rushwa  na badala yake fedha hizo zinapelekwa katika nchi za Ugaibuni hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana kwa wananchi wan chi hizo.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Dkt Edward hosea wakati akizungumza katika mkutano wa bodi ya ushauri wa masuala ya Rushwa kwa nchi za bara la Afrika mapema leo jijini hapa

Aidha dkt Hosea alisema kuwa kiwango hicho cha fedha hupotea kutokana na baadhi ya mianya ya Rushwa ambayo imo kwenye nchi hizo na badala yake fedha hizo zinapelekwa kwenye nchi za Ugaibuni

Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo ya upotevu wa fedha hizo unachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kukithiri kwa rushwa ndani ya Nchi hizo hali ambayo nayo inachangia hata maendeleo duni ya nchi hizo za bara la Afrika

“hiki ni kiwango kikubwa sana cha fedha ambazo zinapotea kusikojulikana lakini mpaka sasa tumeshaanza kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa nchi za bara la Afrika hazikumbwi na rushwa ingawaje pia changamoto ya kupambana nayo ni kubwa sana”Aliongeza Dkt Hosea.

Katika hatua nyingine alisema kuwa mpaka sasa kwa Upande wa Serikali ya Tanzania tayari imeshaanza miachakato mbalimbali ya kujenga bodi ya kupambana na Rushwa ambapo mchakato huo pia utasaidia sana kupunguza wimbi kubwa sana la Rushwa hapa nchini.

Dkt Hosea alisisitiza kuwa ujenzi wa jengo la bodi hiyo ya kupambana na rushwa utaaanza mara baada ya Kupitishwa kwa bajeti yake ambapo jengo hilo litajengwa ndani ya eneo la Kisongo mkoani Arusha

“kwa sasa tunafurai sana kwa kuwa ujenzi wa jengo hili umeshawekwa katika mikakati na kitu ambacho tunasubiri ni bajeti yake na tunachokiamini ni kuwa kupitia bodi hii tutaweza kuendelea kudhibiti mianya ya rushwa ndani ya Nchi za bara la Afrika”aliongeza Dkt Hosea

Sunday, June 17, 2012

‘Ashindwa kujiunga na Sekondari Handeni kwa kukosa ada’



‘Ashindwa kujiunga na Sekondari Handeni kwa kukosa ada’

Mwanafunzi Mwenjuma M. Magalu aliyechaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wilayani Handeni akimuonesha mwandishi fomu ya kuitwa shuleni
Mama wa mtoto huyo, Hadija Magalu
Na Joachim Mushi, Handeni
LICHA ya Serikali kuliarifu Bunge la Tanzania kuwa wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba mwaka 2011 kutoka mikoa 12 tayari wamejiunga na kidato cha kwanza, imebainika bado kuna wanafunzi wameshindwa kujiunga na shule kutokana na kipato duni cha familia zao.
Mwenjuma M. Magalu aliyechaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wilayani Handeni ni miongoni mwa wanafunzi walioshindwa kujiunga na sekondari kutokana na mama yake kushindwa kumgharamia mahitaji ya shule.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni kijijini Msasa, wilayani Handeni, katika utafiti uliofanyika kwa ushirikiano na Chama cha Wanahabari Wanawake (Tamwa), mama wa mtoto huyo Hadija Magalu aliyetelekezwa na mumewe kwa muda mrefu alisema ameshindwa kumsomesha mwanaye kutokana na kipato duni alichonacho.

Mwenjuma M. Magalu (kulia) akiwa na Bibi yake nyumbani kwao Kijiji cha Msasa, wilayani Handeni

Magalu alisema alipata taarifa za kufaulu kwa mwanae tangu Desemba 12, 2011 na kuanza kujikusanya taratibu lakini hadi muda wa kwenda shule ulipofika (Januari 9, 2012) alikuwa hajakamilisha baadhi ya vifaa vinavyohitajika shuleni vikiwemo fedha ya ada na michango mingine.
“Naweza kukuonesha hata baadhi ya vitu ambayo nilikuwa tayari nimenunua kama sare, kwanja na mahitaji mengine madogo madogo…aliyenikwamisha na kunivunja moyo ni babayake (baba wa mtoto), ambaye awali niliwasiliana naye kupitia kwa ndugu zake na kuahidi angenisaidia ada lakini hakufanya hivyo hadi muda wa kwenda shule ulipofika,” alisema Magalu.

Mume wa Magalu (jina tunalo) ametelekeza familia yake (watoto wanne) pamoja na mkewe kwa zaidi ya miaka minne sasa kwa kisingizio kwamba amekwenda nje ya Wilaya ya Handeni kutafuta maisha, huku mkewe akibaki akiangaikia familia hiyo.
“Tumekuwa tukisikia tu kwamba ameonekana kijiji fulani lakini ukifuatilia humpati, na mara nyingi anapowasiliana na ndugu zake ndio wanatupa taarifa zake…nami niliwasiliana naye mara ya mwisho nikimpata taarifa za mtoto kufaulu lakini hakutekeleza ahadi yoyote juu ya kunisaidia ada ya mtoto.

Michango iliyomkwamisha mwanafunzi Mwenjuma Magalu kujiunga na kidato cha kwanza ni ada ya sh. 20,000, fedha ya taaluma sh. 10,000, fedha ya madawati 15,000, fedha ya sweta sh.10,000, kitambulisho sh. 5,000, ulinzi sh. 5,000, tahadhari 5,000 pamoja na fedha kwa ajili ya nembo ya shule sh. 2,000.

Akihutubia Mkutano wa Saba wa Bunge la Tanzania lililomalizika hivi karibuni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kutoka mikoa 12 ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mara, Morogoro, Mwanza, Lindi, Kilimanjaro, Pwani, Ruvuma na Tanga, wanafunzi wote waliofaulu darasa la saba wamefanikiwa kujiunga na Kidato cha Kwanza.

Hata hivyo mwanafunzi Magalu kwa sasa anafanya vibarua kwa moja ya kampuni za Kichina zinazofanya ujenzi wa barabara inayopita Kijiji cha Msasa, kwa madai anatafuta fedha za ada na endapo akikamilisha atahakikisha anaendelea na elimu ya sekondari hapo baadae.

Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuzungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, Hassan Mwachibuzi alisema ofisi yake haina taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na shule, hivyo kumshauri mwandishi amueleze mtoto huyo kufika ofisi za halmashauri ili aweze kujieleza na ikiwezekana kusaidiwa.

“Kama huyo mtoto yupo mwelekeze aje pale ofisini kuna wataalamu wa utambuzi watamuhoji na kuangalia namna ya kumsaidia…sisi hatuna taarifa hizo na huenda wahusika wanatuficha,” alisema kiongozi huyo.

Wanakijiji wailalamikia Serikali Kuu

Wanakijiji wailalamikia Serikali Kuu


Wanajamii wakiwasilisha mrejesho wa PAR mbele ya viongozi wa kata ya Mkambarani

WANAKIJIJI wa kijiji cha Mkambarani Morogoro Vijijini, wameilalamikia Serikali Kuu na halmashauri ya Wilaya kwa kumuingiza mwekezaji kutoka Korea katika kijiji jirani cha Pangawe na kutumia rasilimali maji bure bila kuwashirikisha.

Wananchi hao kutoka katika kijiji cha Mkambarani Kata ya Mkambarani wilaya ya Mororgoro vijiji na viongozi wao wa kata wameishutumu ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkoa na Wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi kwa kuwaingiza wawekezaji wanaoendesha mradi wa kijiji cha mfano cha Pangawe bila kuushirikisha uongozi wa kata na kuanza kutumia maji ya kijiji cha Mkambarani ambao hawakuuchangia.

Tarafa ya Mikese yenye kata 3 na vijiji 11 haina maji safi ya kunywa isipokuwa kijiji cha Mkamabarani ambacho kimekuwa na mradi wake unaotegemewa na vijiji vingine, lakini mradi huo umeteka maji hayo wakati wananchi wanazuiwa kufunga bomba nyumbani kwao.

Wakizungumza katika mrejesho wa utafiti raghibishi wa kijamii (PAR) uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kata hiyo, wakati wa mrejesho ngazi ya wilaya, wananchi hao na Viongozi wa kata wamesema kuwa mradi wa kijiji cha mfano kwa ushirikiano na Korea Kusini hawakushirikishwa.

Waraghibishi kutoka TGNP wakiwa na kikundi cha kufuga Kuku cha Mkambarani Morogoro

Pamoja nayo wamesema kuwa kata hiyo inachangamoto nyingi ambazo zinasababishwa na uongozi mbovu licha ya wananchi wake kujitahidi kuibua na kuchangia miradi mbailimbali.


Katika utafiti huo, changamoto lingine imeonesha wananchi wa Mkambarani hawana ardhi ya kulima mazao ya chakula kutokana na ardhi waliokuwa wakitumia kuchukuliwa na mwekezaji huo na kufye mahindi ya wananchi kitendo kilichosababisha mgogoro kati yao na mgeni huyo.

Akizungumzia mradi huo, Mtandaji wa kata ya Mkambarani, Msekwakadodo Makoko, amesema kuwa uongozi wa kata haikushirikishwa kwenye mradi huo walishangaa wageni wanafika katika kijiji kuuzindua.

“sisi tulishangaa kuona Mwenyekiti na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Pangawe wamepanda ndege kwenda Korea Kusini, waliporudi Waziri Mkuu akaja kuufungua mradi, sisi Kata hatujui chochote, kwa kweli sisi tunausikia tu hatujui ni utaalam gani anaoutoa huyo Mwekezaji,” ameeleza Makoko.

Amesema pia kuwa wanachosikitika ni kwamba maji ambayo wananchi wa Mkambarani walichangia asilimia 5 sasa yanaenda kwa mwekezaji huyo huku wananchi wakikatazwa kuyatumia.

Afisa Kilimo Wilaya ya Morogoro Joseph Malaki amesema kuwa mradi huo wa Korea na Tanzania unalenga kuwajengea wananchi uwezo wa kitaalam kama mafunzo, lakini akalalamikia sera za nchi ambazo zinakubali misaada yenye masharti magumu. “sera za nchi ndo zinazoelekeza ujio wa wageni pamoja na masharati yao, wanakuja na wanasema wanafanya na wataalam wao hatina jinsi, huu ni udhaifu wa sera zetu…,” amesema Ofisa Kilimo huyo.

Akitoa mrejesho wa utafiti huo, mtafiti kutoka TGNP Dinah Nkya amesema kuwa Utafiti umegudua changamoto nyingi ambazo zinaikabili jamii ya kijiji hicho, ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi na serikali ngazi zote.

Masuala makuu ambayo yameibuliwa na jamii katika kijiji hicho ni ukosefu wa maji ya kutosha katika kijiji hicho, wanakijiji wa Fulwe kukosa kabisa maji ya kutumia na kulazimika kununua maji kwa sh. 500 kwa lita 20. Suala lingine ni mgogoro wa ardhi unaotokana na ardhi ya wananchi kuchukuliwa na mwekezaji na taasisi za kiserikali na kidini.

Changamoto nyingine ni kuingiliwa kinyume cha maumbile kwa wasichana wanaofanya kibarua katika mradi huo wa Korea ambapo wanakijiji waliutaka uongozi wa wilaya kumfuatilia mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi kwenye mradi huo ambaye amekuwa akiwadhalilisha wasichana kijinsia.

Kutokana na hilo, mwanchama wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) Mkoa wa Morogoro, Maricelina aliwataka wananchi kuchukua hatua za haraka kudhibiti tatizo hilo ikiwepo kushinikiza uwajibikaji wa viongozi wa ngazi ya kijiji, kata na wilaya.

“Tusipochukua hatua za haraka tutaharibu jamii yetu na hasa vijana wa kesho, wananchi tushikamane, tupambane na watu wanaokuja kutuharibu na kutudhalilisha kijinsia, kwanini asioe anaharibu watu kimaumbile?….,” alisema.

Pia tatizo la mimba za utotoni limeibuliwa kuwa ni tatizo kubwa katika kata hizo kutokana na kukosekana kwa mabweni katika shule ya sekondari Nelson Mandela, ili kuwapa wasichana ulinzi wa kutosha na kuacha kuishi kwenye nyumba za kupanga mitaani.

Aidha changamoto nyingine iliyoibuliwa ni kukosekana kwa soko la kuuzia bidhaa zao za mazao. Wananchi wameitaka serikali kumtaka mwekezaji kampuni ya Mkonge kurudisha sehemu ya shamba kijijini ili litumike sehemu ya soko katika kata hiyo.

*Imeandaliwa na Programu ya Habari na Mawasiliano TGNP

Wanafunzi walemavu Mafinga waipigia magoti Serikali

Wanafunzi walemavu Mafinga waipigia magoti Serikali

Na Joachim Mushi, Thehabari.com- Mafinga

WANAFUNZI wenye ulemavu anuai katika Shule ya Msingi Makalala wameiomba
Serikali na wadau wengine kuwasaidia kuwajengea mazingira bora ya
kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu bora kama
ilivyo kwa watoto wengine.

Kauli hiyo imetolewa katika risala ya wanafunzi hao iliyosomwa jana
Wilayani Mafinga kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika
kiwilaya kwenye Shule ya Msingi Makalala nje kidogo ya Mjini wa Mafinga.

Katika maelezo yao watoto hao wameiomba Serikali na wadau wengine
kuwatizama kundi la watoto wenye ulemavu anuai kwa jicho la karibu, hasa
katika uboreshaji wa mazingira jumuishi ya kujifunzia katika shule zenye
watoto wenye ulemavu.

Pamoja na hayo wanafunzi hao walemavu wameomba kuboreshewa mazingira ya
lijifunzia katika Shule yao ya Makalala, ikiwa ni pamoja na kuwajengea
chumba maalumu kwa ajili ya kujifunzia kitakachokidhi mahitaji ya kundi
hilo maalumu.

Akizungumza katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Mafinga, Bi. Farida Mwasumilwe alisema licha ya Serikali
kujitahidi kuboresha huduma mbalimbali kwa watu wenye ulemavu bado kuna
changamoto nyingi hivyo kuomba wadau kushirikiana kwa pamoja kuwasaidia
watu wenye ulemavu hasa watoto

Acheni Mafinga iitwe Mafinga duh!

 Wadau jana nilikuwa Mjini Mafinga kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, nimejifunza kitu hivyo si vibaya tushirikiane. Mara nyingi kilio cha wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake ni joto linalowakera wengi karibia kipindi kirefu cha mwaka, lakini kwa wanaokerwa na joto hilo si vibaya mnapokuwa mapumziko (likizo) mtembelee Mjini Mafinga kupima baridi mwanana inayopatikana eneo hilo kuanzia mwezi wa sita hadi wa nane. Leo baada ya mdau mkuu wa mtandao wa Thehabari.com kuwasili Mafinga pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Habari Kuhusu Walemavu (ICD), tulilazimika kutafuta namna ya kuidhibiti baridi iliyokuwa ikivuma eneo hilo asubuhi kabla ya kuendelea na majukumu mengine yaliyotuleta.
Nililazimika kuvaa hivi pamoja na mdau kutoka ICD

MAADAM RITAH AJITOLEA DAMU KATIKA KITENGO CHA DAMU SALAMA MJINI DODOMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production Ritha Paulsen akitolewa damu na Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama kituo cha Dodoma Dk Leah Kitundya muda mfupi kabla ya kuanza kwa zoezi la kusaka vipaji vya wasanii chipukizi mkoa wa Dodoma, aliyeko pembeni yake ni Hawa Iche mkuu wa Mawasiliano wa Zantel

Majaji Maadam Ritah katikati Salama Jabir kulia na Paoul wakiwa kazini wakati wa kusaka vipaiji vya Bongo Star Search mjini Dodoma
Vijana wakionyesha vitu vyao mbele ya Camera wakati wa zoezi la kusaka vipaji vya washiriki wa Bongo Satr Search Mjini Dodoma

ZIARA YA NAPE KILOLO MKOANI IRINGA

  Katibu wa Halmashauti Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa michezo mjini Ilula, wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa msaada wa fedha Mwalimu Beatrice Luoga, wakati alipozungumza na walimu wa mjini Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa, juzi.  Nape alimpa msaada huo kwa ajili ya kushughulikia matibabu ya maradhi yanayomsumbua mwalimu huyo, na alizungumza na walimu hao wa shule za sekondari na za msingi ili kujua changamoto zinazowakabili na jinsi CCM iliyounda serikali inavyoweza kuyatatua.
Wananchi wa Kilolo wakimshangilia Nape baada ya kuzungumza nao kwenye Ofisi ya CCM, Kilolo.
Nape akiwatuza wanakwaya wa CCM, Kilolo mkoani, Iringa walipoimba wakati wa mapokezi yake wilayani humo. Kulia ni Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msolla (Picha na Bashir Nkoromo BOFYA HAPA

Friday, June 15, 2012

WAONESHENI WAHALIFU UPENDO NA PIA WAPENI ELIMU


Na Queen Lema,ARUSHA


WAONESHENI WAHALIFU UPENDO NA PIA WAPENI ELIMU

IMEELEZWA kuwa machafuko ndani ya jamii nyingi yanazidi kuongezeka kwa kuwa asilimia kubwa ya wanajamii waliowengi wanawatenga wahalifu mbalimbali badala ya kuwapa elimu ambayo itawafanya waweze kuacha uhalifu wao

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Steve Robert Kutoka Tanga wakati alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha kwa Muorombo Kata ya Terrat Mkoani Arusha mapema jana

Bw Robert alisema kuwa kwa sasa hakuna elimu yoyote ambayo inatolewa kwa watu ambao wanahasi jamii hali ambayo inawafanya hata baadhi yao kutengwa huku uhalifu ukiwa unakithiri sana

Alifafanua kuwa endapo kama jamii ingekuwa na Muongozo imara hasa katika eneo hilo la Kwa Muorombo basi hata idadi ya uhalifu nayo ingepungua sana kwa kuwa kila mara wahalifu wa matukio mbalimbali wangeweza kupatiwa mafunzo pamoja na madhara ya uhalifu

Alisema kuwa mtu ambaye ni muhalifu hapaswi kutengwa na jamii yake na badala yake jamii inatakiwa kuonesha na kuimarisha zaidi upendo ili waweze kufikia katika hatua za kuacha uhalifu ambao ndio chanzo kikubwa sana cha umaskini

“leo hii unakuta eti mtu ni muhalifu lakini badala ya kupewa elimu mbalimbali ya kumsaidia jinsi ya kuepukana na tabia hiyo anatengwa na jamii na wakati nafasi mbalimbali zinatakiwa kutumikan ikiwemo nafasi ya mashirika na Taasisi za Dini”aliongeza bw Robert

Pia aliongeza kuwa wananchi wanapswa kujua mbinu pekee ya kuweza kukinzana na uhalifu wa aina mbalimbali ndani ya jamii husika ni kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kuanzia ngazi za familia kwa kuwa nazo familia nyingi hazina utaratibu wa kuwaelezea watoto wao madhara ya kuwa waharibifu na wavunjifu wa amani

Awali alitataja madhara ya kukithiri kwa uhalifu hasa wizi mdogo mdogo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa majanga makubwa sana ya umaskini ndani ya jamii wakati taifa lina buni mbinu mbalimbali za kupambana na Umaskini.

MWISHO

MHARIRI WA GAZETI LA RAI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA YA SHILINGI MILIONI 1NA NUSU


MHARIRI WA GAZETI LA RAI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA YA SHILINGI MILIONI 1NA NUSU

Na Queen Lema,ARUSHA


MHARIRI wa gazeti la Rai bw Masiaga Matinyi pamoja na watuhumiwa wengine wawili wamefikishwa katika mahakama ya Arusha kwa kosa la kuomba Rushwa kutoka kwa afisa wa Shirika la Tanesco wilayani Monduli mkoani hapa.

Akisomewa mashitaka pamoja na watuhumiwa wengine wawili ambao ni  bi Bora  Bidiga (36)na  Mwita Chomote (32) walitenda kosa hilo wilayani Monduli

Aidha iliendelea kudaiwa mahakamani hapo mbele ya hakimu mkazi bw Yohana miombo na mwendesha mashitaka wa Serikal bw Amidu Msimbana  kuwa watuhumiwa hao wote walitenda kosa hilo kati ya June 13 na 14 majira ya saa kumi jioni wilayani Monduli Mkoani Arusha

Pia ilidaiwa kuwa watuhumiwa wote hao watatu walimlazimisha kwa nguvu afisa wa shirika la Tanesco ambaye amejulikana kwa majina ya Andew Mahamudu  kutoa Rushwa kwa kuwa hakuwa na vigezo vya kufanya kazi ndani ya shirikan hilo 

“baada ya kufanya hivyo watuhumiwa wote hawa walimshawishi awape kiasi cha shilingi Milioni 5 ili wasitangaze lakini baada ya hapo walipokea kiasi cha shilingi laki mbili ambapo walikamtwa na vyombo vya usalama”aliongeza bw Amidu.

Aidha iliendelea kudaiwa kuwa Mshitakiwa wa pili ambaye ni dereva wa mhariri huyo naye anakabiliwa na mashitaka mawili ambapo shitaka la kwanza ni pamoja na kushawishi kupokea rushwa wakati shitaka la pili ni kupokea rushwa kiasi cha shilingi laki mbili

“inadaiwa kuwa huyu ndiye alieenda kupokea kiasi cha shilingi Laki mbili kwa niaba ya Masiaga ambapo kwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria hivyo anakabiliwa na mashitaka mawili ya kujibu’aliongeza mwendesha mashitaka huyo

Hataivyo watuhumiwa wote watatu walipewa masharti ya dhamana ambapo walitakiwa kuwa na mdhamini  ambaye anafanya kazi katika kampuni inayofahamika pamoja na kusaini hati ya kiasin cha shilingi laki tano ambapo wadhamini walifanikiwa kuweka kukidhi matakwa ya mahakama hiyo.

MWISHO

Monday, June 11, 2012

LITA ELFU ZA GONGO ZAKAMATWA


HABARI NA UPAKO WA HABARI

JESHI la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kukamata lita elfu tisa za pombe haramu aina ya Gongo ambayo ilikuwa inayokea nchini Kenya na kuingizwa Tanzania kwa njia za Magendo

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha bw Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea June 10 majira ya saaa kumi na mbili za jioni katika eneo la Namanga

Alisema kuwa kufanikiwa kukamatwa kwa pombe hiyo haramu aina ya Gongo kunatokana na Taarifa kutoka kwa raia wema ambapo ndio waliotoa taarifa kwa jeshi hilo na jeshi hilo likaanza  msako maalumu

Kamanda huyo alisema kuwa mara baada ya taarifa hizo askari walirfanya doria ndani ya eneo hilo la Namanga  na walifanikiwa kumkamata raia mmoja wa kitanzania ambaye alijulikana kwa jina Nicoulaus Thobias(35) akiwa katika katika eneo hilo lita hizo za gongo ambazo zililkuwa kwenye mapipa 150

Aliendelea kusema kuwa mara baada ya kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo askari waliamua kufanya upekuzi katika gari lake na kumkumta na pombe hiyo haramu ambayo aliitoa nchini Kenya na kuileta Tanzania kwa ajili ya matumizi ambayo bado hajafahamika

“hapa mara baada ya kukamtwa askari hao walikagua gari alilokuwa nalo  mtuhumiwa huyo ambalo ni Scania  lenye namba za usajili  T 416 AJX ambalo linamilikiwa na Joseph Masawe ambapo mara baada ya hapo mtuhimiwa aliwekwa chini ya ulinzi’aliongeza kamanda Sabas

Pia alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipohojiwa juu ya pombe hiyo haramu alidai kuwa pombe hiyo Si pombe bali ni Spirit jambo ambalo halikuwa kweli na badala yake alikuwa anadanganya Polisi

Hataivyo Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika ambapo pia gari nalo bado linashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi

mwisho

milion 200 za wanufaisha wajasiamali

KAMPUNI ya Tanzania browaries Limited(TBL) imetoa ruzuku ya vitendea kazi vyenye gharama ya shilingi milioni mia mbili kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Tanzania nzima huku kanda ya kaskazini ikikabidhiwa vitendeakazi vyenye gharama ya shilingi milioni 50 lengo likiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuzisaidia jamii mbali mbali zinazowazunguka.

Akikabidhi vitendea kaz i hivyo kwa wafanyabiashara wa kanda ya kaskazini katika tamasha lililofanyika mjini hapa meneja wa bia ya safari larger bw Oscar Shelukindo alisema kuwa kampuni hiyo imejiwekea mpango wa kuhakikisha kuwa wanawasidia wajasiriamali Tanzania nzima ili waweze kujikwamua katika hali ngumu ya kiumskini.

Alisema kuwa vifaa hivyo walivyovitoa kwa wafanyabiashara hao ni vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kutumika katika biashara zao mbali mbali wanazoziendesha kwa kuwa wako watu wana malengo na maono mazuri ya baishara lakini wanashindwa kufikia malengo kwa ajili ya kukosa vitendea kazi.

“sisi tumeona tuwe na mpango endelevu wa kuwasaidia hawa wafanyabiashara vitendea kazi mfano yuko huyu mfugaji wa kuku tumempatia mashine,mwingine friza ambapo kila mmoja anategemea biashara anayofanya alimaradi tu wamekidhi vigezo vyetu lazima tumapatie vitendea kazi “alisema Shelukindo

Aliongeza kuwa zoezi hili litakuwa endelevu ambapo ametaja kanda ambazo zinahusika na kupatiwa vitendea kazi kuwa ni pamoja na kanda ya kusini ,mwanza, dares saalam pamoja na kanda ya kaskazini ambapo aliwataka wafanyabiashara kujitokeza mwaka huu kujaza fomu kwa kuwa endapo watakidhi vigezo vinavyohitajika nao wataweza kunufaika na vitendea kazi vya kuendeshea biashara zao.

Awali mgeni rasmi katika tamasha hilo afisa biashara manispaa ya arusha bw Niarira Elivelema alisema kuwa swala hilo lililofanywa na Safari Larger ni mfano wa kuigwa na taasisi nyinginezo kwa kuwa wameonyesha ushirikiano wao na jamii inayowazunguka .

Aliongeza kuwa endapo wafanyabiashara wadogo watapewa kipaumbele kama walivyofanya tbl ni wazi kuwa hata taifa nalo litaweza kuongeza kipato kutokana na ushuru ambao utakuwa unalipwa kutoka kwa wafanyabiashara hao.

mwisho

HAYA NDIO MAISHA NA WANAWAKE WA PEMBEZONI ,HAPA NI IWALANJE MBEYA VIJIJINI




habari kwa hisani ya francis godwin ,mzee wa matukio
Bibi kizee mkazi wa kijiji cha Iwalanje kata ya Ijombe wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akitoka kusaka kuni leo jumapili kama alivyonaswa kamera ya mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ,kamera ambayo itaendelea kuimulika kata hiyo kwa takribani wiki moja ,hii yote kwa udhamini wa mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP)

CHUO KIKUU UDSM CHAFANYA KONGAMANO LA WANATAALUMA


Mwanataalum mkonge Profesa Goran Hyden akijibu hoja na maswali mbalimbali yalitolewa na wahadhiri na wanataalum mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania leo mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wake kitaalum. 
Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar e salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Uganda Profesa Apolo Nsibambi(kulia) akichangia mada jana mjini Dar es saam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa  Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania. Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi(katikati) na Profesa Goran Hyden(kushoto)
Katibu Mkuu zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu akichangia mada jana mjini Dar es saam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa  Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania.Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es  salaam Profesa Rwekaza Mukanda. 
Profesa Bernadeta Killian wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akitoa mada jana mjini Dar es salaam kuhusu kitabu cha Profesa Goran Hyden cha Beyond Ujamaa in Tanzania wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wake kitaalum.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es  salaam Profesa Rwekaza Mukanda (kulia) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uganda Profesa Apolo Nsibambi (katikati) na Balozi wa Zambia nchini Judith Kangoma( kushoto) leo mjini Dar es salaam wakati wa kongamano la siku moja la wanataalum liloandaliwa maalum na Chuo Kikuu cha Dar es salaam la kutambua mchango wa Profesa  Goran Hyden alioutoa ndani na nje Tanzania 

WANAFUNZI WA UDOM WAJITOLEA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI



Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula (Wa Pili Kushoto) akiwa amesimama wakati akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni  mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe aliyeongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma, Na Balozi Job Lusinde katika zoezi la kujitolea damu kwa hiari lililofanyika siku ya leo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na Kuandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)

Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe akitoa neno fupi kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma waliofika katika Zoezi la Kujitolea Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma jana.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamejitokeza katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari lililofanyika jana Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) na kuandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Afisa Mahusiano wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Bi Beatrice alipokua akitoa damu kwa hiari katika Zoezi la Kuchangia Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma jana huku Akishuhudiwa na Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Manongi(Mwenye Miwani)
 Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika jana Chuo Hapo.

 Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akiaga wanafunzi na wafanyakazi waliojitoa katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) lililofanyika chuo hapo jana.Picha Zote Na Josephat Lukaza wa http://josephatlukaza.blogspot.com

Askofu Malasusa: Wanasiasa Msiteke Nyara Mchakato Wa Katiba

 

Pamela Chilongola na Bakari Kiango.

WANASIASA nchini, wametakiwa kuacha kujihusishana suala la katiba na badala yake, suala hilo liachwe mikononi mwa wananchi.Rai hiyo ilitolewa jana na jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ,Askofu Dk Alex Malasusa, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa Usharika wa Kinyerezi.

Dk Malasusa alisema katiba ya nchi si mali ya wanasiasa wanaotaka kuiteka nyara na kwamba hiyo ni mali ya Watanzania, wanaopaswa kupewa uhuru wa kujadili kwa kina.
Dk Malasusa alisema wananchi wanapaswa kuwa na fursa kubwa ya kuboresha mchakato wa kuandika katiba hiyo, lakini wanakwamishwa na asilimia kubwa ya wanasiasa, wanachangia.

“Sina ugomvi na wanasiasa katika suala hili, ila naomba wawaachie wananchi, kwanza ili wapate fursa ya kuchangia maoni yao,” alisema Dk Malasusa.Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia maoni yao ili kuboresha katiba inayotarajiwa kuandikwa kwa manufaa ya wananchi wote.

“Wote mjitokeze na kutoa maoni yenu, msikae kimya katika mchakato huu, alisema Dk Malasusa.Pia aliwataka waumini wa kanisa hilo, kubadilika na kufanya mambo yasiyomchukiza Mungu.Alisema lengi la kanisa hilo ni kujaribu kuwasaidia waumini wake, ili waweze kubadilika na si vinginevyo.

Sunday, June 10, 2012

BREAKING NEWSSSSSSSSSSSS:PROFESA GEORGE SAITOTI AFARIKI KATIKA AJALI YA HELIKOPTA NCHINI KENYA



BREAKING NEWSSSSSSSSSSSS:PROFESA GEORGE SAITOTI AFARIKI KATIKA AJALI YA HELIKOPTA NCHINI KENYA


 Waziri wa Usalama wa ndani wa Kenya Profesa George Saitoti amefariki dunia kwa ajali ya Helikopta iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Ngong Katika milima ya Magharibi mwa Nairobi nchini humo wakati akiwa katika safari ya kikazi akielekea Kisumu, Saitoti amefariki akiwa na Naibu Waziri wake Orwa Ojode.
Mbunge wa Kenya Najib Balala amethibitisha kutokea kwa kifo hicho katika mtandao wake wa Twitter, Serikali ya Kenya bado haijasema chochote kuhusu sababu za ajali hiyo iliyopoteza mawaziri hao pamoja na watu wengine wanne jumla yao wakiwa Sita, Profesa Saitoti alikuwa akitarajia kugombea urais katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika baadae mwaka huu

Saturday, June 9, 2012

RAISI KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WAPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mhe. Edward Rutakangwa kuwa kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dares salaam
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mh. Semistocles Kaijage (kulia) kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kabla ya uteuzi huo Mh. Semistocles Kaijage alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifuarahia Jambo na kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Edward Rutakangwa (wa tatu kutoka kulia) mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Jaji wa mahakama ya Rufani Mussa Kipenka na Jaji Semistocles Kaijage (wa kwanza kushoto).
Mh. Rufani Mussa Kipenka akipongezwa na baadhi ya ndugu waliohudhuria hafla fupi ya kuapishwa kwake kuwa jaji wa mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es salaam.


Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema atahakikisha kuwaanatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria,kupunguza mlundikano wa kesi na kuhakikisha kuwa maamuzi yanatolewa kwa haki.
Jaji wamahakama ya Rufani Mh. Mussa Kipenka akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Jakaya kikwete leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni jaji mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.
 
 
habari kwa hisani ya father kidevu blog

MWENYEKITI WA UMOJA WA SHULE  BINAFSINA VYUO BINAFSI BI ESTER LEMA AKINENA JAMBO


WADAU WAKIFUATILIWA KWA UKARIBU SANA


HABARI NA UPAKO WA HABARI

WAMILIKI wa shule binafsi wametakiwa kuacha kutoa ajira zaidi kwa walimu wa mataifa ya nje na badala yake wachukue walimu wa kitanzania ambao wanauwezo ili kuepusha shule zao na udanganyifu wa mithiani

Kauli hiyo imetolea mjini hapa na afisa elimu wa manispaa ya Arusha Bw Omary Mkombole wakati akiongea na wanachama wa Tamongsco ambao ni wamiliki pamoja namameneja wa shule mbalimbali jijii hapa

Bw Mkombloe alisema kuwa wamiliki hao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajiamini katika kazi zao ili waweze kufikia malengo mbalimbali ambayo wanayatka lakini kama wataendelea  kuwathamini zadii walimu wa mataifa ya nje basi hawataweza kufikia malengo

Alisema kuwa kuongeaz kingereza kwa mwalimu isiwe ni tija mojawapo ya kusababisha asilimia kubwa ya watu kuweza kuajiriwa bali wanatakiwa kuangalia sifa na vigezo vya mwalimu bora

Wakati huo huo mkaguzi wa elimu kanda ya kaskazini magharibi bw Victor Bwindiki aliwaambia walimu hao kuwa wanatakiwa kuwa wabiunifu dhidi ya shule zao za binafsi ili wali mu wasiwakambie ovyo

Bwindiki alisema kuwa endapo kama wamiliki wa shule wataboresha taasisi zao basi itasaidia kwa kiwango kikubwa sana hata kuweza kuongeza idadi ya wasomi ndani ya nchi ya Tanzania

Awali wamiiki hao wa shule pamoja na mameneja walisema kuwa wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kuweza kuwafikia wananchi kwa kuwapa elimu iliyo baora lakini kinachowasumbua ni utozwaji wa kodi kubwa sana

Akiongea kwa niaba ya  wakuu hao mwenyekiti wa umoja huo jijini hapa Bi Ester Lema alisema kuwa Serikali inatakiwa kuaangalisa shuguli ambazo wanazifanya kwani ni shuguli kubwa sana ya kuweza kusadiia jamii lakini bado Serikali hiyohiyo imekuwa ni chanzo mojawapo cha kuwatoza ushuru.

Mwisho