KAMPUNI ya Mkundi Production yenye makao makuu Jijini Arusha
imeahidi kuibua lakini pia kuwezza kuendeleza vipaji vya mbalimbali vya vijana ikiwa ni pamoja na
kuweza kuwasaida kurekodi na kusambaza kazi zao
Aidha kwa sasa asilimia kubwa ya vijana wenye vipaji vya
uimbaji wanashindwa kufikia malengo yao
mbalimbali kwa kuwa hawana uwezo wa kuingia studio lakini pia kutoa na
kughramikia baadhi ya gharama hali ambayo inachangia sana kupoteza vipaji vingi
Hayo yameelzezwa na mkurugenzi jmtendaji wa kampuni hiyo
Carlos Mkundi mapema jana mara baada ya kuzindua Album ijulikanayo kama “NIMETOKA
MBALI”ambayo imejumuisha vijna mbalimbali wa mkoa wa Arusha
Mkundi alisema kuwa kampuni yakeimejidhatiti kuhakikisha
kuwa kila msanii mwenye uwezo wa kuimba aweze kunufaika na kipaji chake na
kamwe kisingizo kuwa ghrama ni chanzo kisiwepo
Aidha alidai kwa sasa wasanii wa nyimbo mbalimbali ndani ya
mkoa wa Arusha wanashindwa kuimba na kutoa album zao kwa kuwa kuna changamoto
lukuki sana
ambazo ndizo chanzo kikubwa cha wao kushindwa kufanya vema zaidi
Wakati huo huo alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka huu
Kampuni yake tayari imeshwaweza kuwasaidia wasanii saba kuweza kurekodi album
zao na hivyo mikakati zaidi bado itaendelea kuwekwa
Pia alidai kwa kila mwaka wasanii saba kutoka Jijini Arusha
wataweza kurekodi kwa msaada wa kampuni hiyo lakini hata wale ambao bado
hawajaweza kurekodi basi watapewa misaada mbalimbali ambayo inalenga kuinua
vipaji vyao zaidi
MWISHO
No comments:
Post a Comment