NA MWANDISHI WETU,ARUSHA
MKAPA FOUNDATION YATOA MAFUNZO KWA TIMU ZA USIMAMIZI WA
AFYA KUTOKA KATIKA WILAYA 132 HAPA NCHINI
TAASISI ya Mkapa Foundation imefanikiwa kutoa mafunzo timu
za usimamizi wa afya kwenye Wilaya 132
hapa nchini huku mafunzo hayo
yakiwa na malengi ya kuwajengea uwezo wa rasilimali watu ili waweze kutoa
huduma bora zaidi za afya katika maeneo yao
ya kazi.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mpango kitengo cha uwezehsaji
katika taasisi hiyo,Bi Pamela Chiwa wakati akiongea na wataalamu wa afya kutoka
katika vituo vya afya ndani ya kanda ya kaskazini mapema jana
Aidha Pamela alisema kuwa timu hizo za usimamizi wa afya
katika ngazi ya Wilaya ziliweza kupatiwa mafunzo hayo ya rasilimali watu yaliweza kudumu hapa nchini kwa muda wa mwaka
mmoja ambapo mpaka sasa mafanikio makubwa sana
yameshonekana katika sekta hiyo ya Afya
Alifafanua kuwa mbali na kuweza kuwajengea uwezo wataalamu
hao wa afya ambao ni timu za usimamizi wa afya lakini sasa wanashuka zaidi ambapo
wanalenga pia kuwapa mafunzo kama hayo hayo wataalamu
wa afya kutoka katika vituo vya afya.
Alibainisha kuwa yote
hayo ambayo yanafanyika chini ya Taasisi ya Mkapa Foundation yanalenga
kuhakikisha kuwa kila watanzania wanapata huduma bora na kwa wakati ili kuokoa maisha
ya watu wengi zaidi ambao ndio nguvu kazi ya taifa la leo
Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wataalamu wa afya
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaachana na dhana inayosema kuwa wataalamu wa
afya ni wachache katika vituo,na hata hospitali bali wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanafanya kazi tena kwa ubora wa hali ya juu hata kama wapo wachache
Hataivyo alisema kuwa kama wataalamu hao watafanya kazi kwa
ubora ambao unatakiwa basi watachangia sana
huduma za afya kuweza kuboreka zaidi ya sasa huku hali hiyo pia itachangia kwa
kiwango kikubwa maendeleo ya Nchi hivyo
hata malengo ya Taaasisi hiyo ya Benjamini Mkapa nayo yataweza kufanikiwa kwa
kiwango cha hali ya juu sana.
MWISHO
No comments:
Post a Comment