Sunday, September 22, 2013

WAZIRI NAGU ATAKA MCHANGO WA WALIMU KWENYE TAIFA LA TANZANIA UJULIKANE

dkt Mary Nagu

Serikali imetakiwa kuhakikisha kuwa inatambua na kuthamini zaidi kazi za walimu hapa nchini lakini pia kuwajengea mazingira mazuri ya kazi kwani kama watabaguliwa na kisha kuachwa nyuma ni wazi kuwa sumu mbaya itatembea kwenye maisha ya wanafunzi

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dkt Mary Nagu katika maafali ya nne ya shule ya Msingi haradali iliopo Wilayani Meru mkoani Arusha mapema leo.

Dkt Nagu alisema kuwa Serikali lakini hata nao wanachi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawajengea walimu mazingira mazuri ya kufanya kazi kwani wao wanamchango mkubwa sana kwenye taifa

Alisema kuwa kama wadau mbalimbali lakini pia Serikali itafanya hivyo ni wazi kuwa walimu watafundisha kwa moyo bila kujali aina ya shule na changamoto ambazo wanakabiliana nazo mabazo wakati mwingine ndio chanzo kikubwa cha mdondoko wa elimu

Alifafanua kuwa kama walimu wa nchi ya Tanzania watakuwa wanafanya kazi bila kupewa kipaumbele cha hali ya juu sana basi wao watakuwa mabalozi wazuri wa kupandikiza mbegu mbaya kwa wanafunzi na hatimaye madhara yatajionesha muda usio mrefu.


Wakati huo huo mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo ya Haradani,Bw Simon Kaaya
alisema kuwa ili kukuza na kuwekeza kwenye sekta hiyo ya elimu hapa nchini Changamoto mbalimbali zinatakiwa kutatuliwa kwa haraka sana kwani bado kuna umuhimu mkubwa wa elimu.

Bw Kaaya alisema kuwa mbali na hayo hata wamiliki wa shule mbalimbali wanatakiwa kuangalia zaidi suala la mahitaji kuliko suala la maslahi ambalo wakati mwingine linasababisha baadhi ya watoto kukosa elimu kabisa.



Tuesday, August 27, 2013

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KULIKO KILIMO CHA MAJIRA YA MWAKA



Na Queen Lema, Arusha


Wakulima wa Kanda ya kaskazini wameshauriwa kuhakikisha kuwa wanaanzisha utaratibu maalumu wa kutegemea zaidi kilimo cha umwagiliaji kuliko kutegemea kilimo cha majira ya mwaka kwani aina hiyo ya kilimo kwa sasa inaonekana kupitwa na wakati.

Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Bw Elias Mshiu ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wakulima Tanzania(TFA)wakati akiongea na gazeti hili kuhusu hali ya kilimo kwa kanda ya kaskazini mapema jana

Aidha Bw Mshiu alisema kuwa inashangaza sana kuona kuwa asilimia kubwa ya wakulima hasa wa kanda hii ya kaskazini bado wakiwa wanategenea kilimo cha mvua za Vuli lakini pia mvua za masika hali ambayo ndiyo chanzo cha ukame

Alibainisha kuwa endapo kama wakulima watatumia zaidi aina ya kilimo cha umwagiliaji ni wazi kuwa hata mazao nayo yatawweza kuongezeka tofauti na sasa ambapo wapo baadhi ya wakulima ambao wanafanya kama kubahatisha tu

Alisema, Kilimo cha umwagiliaji kina tija kubwa sana kwa wakulima wa kanda hii hivyo basi ni vema hata kama nayo wizara ikahakikisha kuwa inatoa elimu zaidi  na fursa mbalimbali ili wakulima wazoeee kuliko kutumia kilimo cha majira ya mwaka ambacho wakati mwingine kinakataa kabisa.

Pia alisema katika Chama hicho cha TFAkwa sasa wameweza kugundua changamoto hiyo ya wakulima wengi kutegemea zaidi kilimo cha majira ya mwaka hivyo wamebuni mbinu na njia mbadala ambazo zitaweza kuifanya jamii iweze kuondokana nacho kwa malengo ya kuongeza zaidi chakula

Alitaja Mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuweza kuwakopesha lakini pia kuwawezesha wakulima vifaa mbalimbali kwa ajili ya umwagiliaji ili waweze kufikia malengo yao ambayo wamejiwekea.

“tulikaa na kisha kuona kuwa kuna umuhimu wa kuwasaidia hawa wakulima ili wawe na elimu hii ya umwagiliaji lakini waweze kukopa hata vifaa kwa ajili ya umwagiliaji katika mashamba yao na kwa kweli kama wote wataitiika hata kuja kuchukua elimu hii basi kilimo kwa kanda hii kitaimarika sana”aliongeza Bw Mshiu.

Alimalizia kwa kusema kuwa nao wakulima wanatakiwa kubadilika na wanatakiwa pia kuachana na kilimo cha mazoea ambacho mara kwa mara ndiocho kinachisababisha waonekane ni wakulima lakini faida hawana na badala yake wafuate sheria,kanuni, na taratibu mbalimbali za Kilimo.

MWISHO

MAASKOFU NA WASIMAMIZI WA MAKANISA FUATILIENI MAADILI YA WACHUNGAJI WENU ILI WASIWABISHE-ASKOFU MGONJA





IMEBAINIKA kuwa kutokana na tabia ya Maaskofu na wasimamizi mbalimbali wa makanisa kushindwa kuwafundisha wachungaji wao jinsi ya kuitumikia jamii ya kikristo ndio chanzo pekee cha baadhi ya viongozi wa dini kupata dharau ambazo haziwahusu.

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Askofu Aminiel Mgonja wa kanisa la Arusha Praise centre lilopo Sekei wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo juu ya maadalizi ya mahafali ya wachungaji 30 wa kanisa hilo yatakayofanyika mapema wiki ijayo

Askofu Mgonja alisema kuwa wasimamizi wa makanisa lakini pia maskofu wanatakiwa kuwa na utaratibu a kuwafundisha mambao mbalimbali wachungaji wao ili nao watakapofundisha waumini wawe na umoja na wala sio mgawanyiko

Alisema, kupitia mafundisho ambayo yatakuwa yanatolewa mara kwa mara juu ya wachungaji yartaweza kuwajenga kiimani lakini pia kiroho kwani asilimia kubwa ya wachungaji wa sasa wanakabiliwa na mambo mengi sana

Alibainisha kuwa watakapojijenga kiroho na kiimani kutaweza kuruhusu hata kazi ya bwana iweze kutendeka kwa wepesi zaidi kuliko pale ambapo kazi ya kulinda na kuwahifadhi kondoo itakapofanywa na wachungaji pekee yao.

“kama wachungaji wakiharibu kazi ya bwana basi sifa chafu haibaki kwao tu bali inabaki kwenye kanisa zima lakini pia inabaki kwa maaskofu sasa kabla hatujakubali kuchafiliwa ni lazima sisi kama maaskofu tujiwekee taratibu za kuwafunidhs kila mara hata kama wanaelimu ya uchungaji”aliongeza Askofu huyo

Wakati huo huo alidai kuwa hata nao wachungaji wa sasa wanatakiwa kuangalia zaidi msingi wa maandiko kuliko msingi wa mambo ya dunia ambayo wakati mwingine wanasababisha wawe wachungaji wa shetani

Alisema ni vema kama wakawa na tabia ya kufuata zaidi maadili na kuangalia ni aina ya huduma gani ambayo wanaitoa kwa mkristo kuliko kuacha maadili na kisha kujikuta wakiwa wameshazama ndani ya dhambi hivyo kusababisha madhara ya madharau ndani na hata nje ya kanisa

Kanisa hilo linataarajia kuwafanyia maafali wachungaji wake 30 ambao wamehitimu kozi na mafunzo ya uchungaji huku somo kubwa kwao likiwa ni maadili ya uchungaji kwa jamii yote hapa duniani

Monday, August 26, 2013

POLISI YAWAKAMATA MAJAMBAZI WANNE WALIOPORA MADINI YA MILIONI 40 NA FEDHA KIASI CHA MILIONI 5

KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,PICHA NA MAKTABA




POLISI YAWAKAMATA MAJAMBAZI WANNE WALIOPORA MADINI YA MILIONI 40 NA FEDHA KIASI CHA MILIONI  5
, Arusha

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwatia nguvuni majambazi wanne ambao walifanya tukio la wizi wa mfanyabiashara wa madini na kisha kumpora madini yenye thamani ya Milioni 40 pamoja na fedha taslimu Milioni 5.
aidha majambazi hayo yalifanya tukio hilo la kumvamia na kumjerui mfanyabiashara wa madini aliyejulikana kwa jina la Abeli Musa(35)mnamo Agust 23 majira ya saa nane na nusu mchana.
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa kukamwatwa kwa majambazi hayo kunatokana na taarifa za raia wema pamoja na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi ambao waliingia kazini rasmi kwa ajili ya kuwasaka majambazi kuanzia siku ya tukio.
Sabas alisema kuwa Majambazi hayo ambayo yamefahamika kwa majina ya Shangai William(38)mkazi wa Sokoni one, Ally Habibu au dogoo (23)mkazi wa Tabata Dar es saalam, Eugine Donas(28)mkazi wa makao Mapya pamoja  na  Josephat Jerome(29)mkazi wa Sombetini ambapo walikamatwa Agust 24 katika maeneo ya nyumba za kulala wageni Makao Mapya
Wakati huo huo alidai kuwa mara baada ya kuwamata majambazi hao pia walifanikiwa kukamata vifaa walivyotumia katika tukio hilo na matukio mengine ya uuaji yaliyotokea Jijini arusha
Ametaja Vifaa hivyo pamoja na silaha kuwa ni pamoja na Bastola aina ya Browing Model 83 Cal 9 yenye namba 4738 huku ikiwa na risasi 10 pamoja na bastola ya LAMI ikiwa na Risasi 12.
Vifaa vingine ni pamoja na Gari aina ya Vist yenye namba za usajili T 368  AUH huku pikipiki aina ya Skygo yenye namba T352CBW pamoja na pikipiki nyingine yenye namba T 464 APH aina ya Honda nazo zikimatwa kwani majambazi hayo yalitumia vifaa hivyo kwa ajili ya uporaji maeneo mbalimbali.

MWISHO


Wednesday, July 24, 2013

NYATI WA AJABU AIBUKA NGORONGORO

Na Bety Alex, ngorongoro


Wahifadhi, watafiti na wataalam kadhaa wako katika harakati za kumsaka
Nyati wa ajabu anayedaiwa kuwa na rangi ya maziwa, ambaye hivi
karibuni amekuwa akionekana katika mwambao wa bonde kuu la Ngorongoro
(Kreta), na kusababisha tafrani kubwa.



Kwa mujibu wa mtalaam wa ikolojia katika mamlaka hiyo Patrice Mattay,
uwepo wa nyati (mbogo) huyo wa aina yake hifadhini hapo kumeibua suala
jipya katika utafiti wa wanyama pori kwani hakujawahi kuwepo Nyati
mwenye rangi nyeupe popote duniani.



Kwa kawaida Wanyama wote aina ya nyati huwa na ngozi yenye rangi nyeusi.



Nyati huyo mweupe aligundulika kwa mara ya kwanza na maafisa wa polisi
wanaofanya kazi katika kituo cha polisi kilichopo ndani ya hifadhi
hiyo ambao wanasema mnyama huyo hupita katika maeneo ya kituo hicho
majira ya asubuhi akiwa miongoni mwa Mbogo wengine takribani 20.
Ngorongoro ina nyati wapatao 350.



“Ni kweli hata mimi binafsi nimemshuhudia Nyati huyo mweupe akikatiza
katika sehemu mbalimbali za hifadhi ya Ngorongoro majira ya asubuhi
akiwa katika kundi la mbogo wengine,” alisema Mkuu wa kituo cha
Ngorongoro Afisa wa Polisi JJ Paul.



Hadi sasa ni maaskari wanaofanya doria katika maeneo ya hifadhi hiyo,
hususan nyakati za asubuhi, ndio wanaothibitisha kwa kiwango kikubwa
kumuona Nyati huyo wa ajabu ambaye sasa anatarajiwa kuwa atakuwa
kivutio kipya cha utalii katika Tanzania nchi ambayo ndiyo pekee
duniani mnyama huyo atakuwa anapatikana.



Meneja wa Uhifadhi katika mamlaka ya Ngorongoro, Amiyo T. Amiyo
amesema tayari shirika lake limekwisha tuma askari wake kadhaa kumsaka
Nyati huyo wa ajabu ili kubaini eneo ambalo anapatikana kwa ajili ya
kuwezesha utafiti zaidi.



“Na kwa mtu yeyote mwenye kutuletea taarifa kuhusu Nyati huyo mweupe
zitakazotuwezesha kumpata mnyama huyo basi naye pia atazawadiwa
ipasavyo,” alisema Amiyo.



Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ndiyo inayoongoza kwa kupata watalii
wengi nchini na kwa mujibu wa Afisa utalii wa shirika hilo, Asantaeli
Melita, zaidi ya wageni 585,000 hutembelea eneo hilo, na hasa Kreta,
kila mwaka. Tanzania kwa ujumla hupata watalii milioni moja kwa mwaka.



Idadi ya wanyamapori walioko Ngorongoro kwa sasa inafikia 300,000
wengi wao wakiwa ndani ya bonde lenyewe huku baadhi, na hasa twiga
wakiishi nje ya kreta.



Mbali na Mbogo wa jabu aliyegunduliwa hivi karibuni, eneo la
Ngorongoro pia lina maajabu mengine kadhaa, ukiwemo kilima cha mchanga
unaotembea bila kusambaratika, idadi kubwa ya Kakakuona, mnyama
anayedaiwa kuwa na uwezo wa kutabiri, pamoja na idadi kubwa ya wanyama
adimu kama Mbwa-mwitu na Faru.

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII 120 WAFUNDWA


ZAIDI ya maafisa maendeleo ya jamii 120 wa halmashauri za wilaya na
wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya wananchi wapatao 36 katika mikoa
mbalimbali nchini wamepewa mafunzo malumu  yanayohusu haki za watoto
,ikiwemo Uhsai, Ulinzi, Maendeleo  Ushiriki wa bila kubaguliwa ili
waweze kuzilinda na kuhakikisha hakuna mtoto anayenyanyaswa.

Hayo yamo katika hotuba ya mkuu wa mkoa wa ARusha, Madesa Mulongo,
aliyoyatoa hivi karibuni katika maadhmisho ya siku ya mtoto wa afrika
ambazo kimkoa zimeadhimishwa katika kijij cha Kikatiti wilayani
Arumeru.

Ameseema kuwa katika kuhakikisha haki za watoto zinalindwa na
kupatikana tayari wlaya 84 zimeshaunda mabaraza ya watoto ikiwemo jiji
la Arusha, kwa ajili ya kulinda na kusimamia haki mbalimbali za watoto
.

Magesa Mulongo, amesema katika kuhakikisha haki hizo zinapatikana
tayari serikali imeingiza kwenye mitaala ya Vyuo vya maendeleo ya
jamii sanjari na kuwepo kwa sera  ya maendeleo ya mtoto nchini
masuala ya haki za watoto ili kuepuka utumikishwaji  wa watoto kwenye
kazi zenye madhjara katika mazingira hatarishi .

Aidha amesema kuwa katika juhudi hizo za kuhakikisha haki za watoto
zinalindwa zaidi ya watoto 720 mkoani Arusha, waishio kwenye mazingira
 magumu wameondolewa kwa ushirikiano na mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali likiwemo shirika la Mkombozi ambalo limeweza  kuondoa
watoto 29 na kuwaunganisha katika mfumo rasmi wa elimu ikiwemo Ufundi

Amesema kuwa watoto 6 wameunganishwa na familia zao ,watoto 8
wameunganikatika familia zao na kupatiwa elimu ya kujitegemea, watoto
20 wamepelekwa kwenye kituo kingine cha Mkombozi kilichopo Moshi
mkoani Kilimanjaro na kuunganishwa kwenye mradi wa bustani 40 sanjari
na kuhudumiwa i  elimu wakiwa katika familia zao

Ameongeza kuwa katika mlolongo huo familia 60 kutoka kata za Unga
limited na Ngarenaro, zimewezeshwa kiuchumi ili ziweze kumudu kulea na
kutunza watoto wao

Amesema kuwa pia Shirika lingine la Action for Children, limeweza
kutoa  elimu  katika shule 12 mbalimbali ambayo inahusu utetezi na
ushawishi ,haki za watoto na kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi
21,  katika halmashauri 3 za Jiji la Arusha, Halmashauri ya Meru, na
Arusha DC.

Amesema kuwa mkoa huo unaendelea na vita dhidi ya dawa za kulevya na
utumikishwaji wa watoto kwenye mazingira hatarishi  kupitia Idara za
maendeleo ya jamii katika halmashauri mbalimbali kwa kushirikiana na
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambapo elimu ya madhara ya dawa za
kulevya imekuwa ikitolewa .

MSISUBIRI MSIMU WA NANE NANE UFIKE NDIO MUANZE KUWEKA VIPANDO MNAWANYIMA WAKULIMA NA WAFUGAJI HAKI ZAO-MAGESA MULONGO



Halmashauri za kanda ya kaskazini zimetakiwa kujiwekea utaratibu wa
kuweka vipando na mashamba darasa katika viwanja vya maonesho ya
wakulima na wafugaji(TASO)kila wakati na kuachana na tabia ya
kustawisha pamoja na kuweka vipando hivyo mwezi mmoja kabla ya
maonesho hali ambayo wakati mwingine inasababisha maana halisi ya
kilimo kwanza kufa.

Wito huo umetolewa Jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Bw Magesa Mulongo
wakati akiongea na wadau wa kilimo wa chama cha wakulima na wafugaji
kanda ya kaskazini (TASO) kwenye maandalizi ya maonesho hayo
yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni

Alisema Halmashauri za kanda ya kaskazini zinakabiliwa na changamoto
hiyo hivyo jitiada mbalimbali bado zinahitajika ili kuweza kuboresha
kilimo kwanza hususani kwenye suala la vipando ambavyo baadhi yake
hufanywa kama mazoea tu

Alizitaja changamoto kubwa ambazo zinafanya halmashauri kupanda
vipando hivyo kwa mazoea ni pamoja na kutojua maana halisi ya chama
hicho pamoja na maonesho kwani asilimia kubw ya watu wanafikiri kuwa
viwanja hivyo vinaweza kutumika kuanzia Agust Moja hadi kumi kwwa kila
mwaka

Mbali na hayo alisema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea katika
maonesho ya wakulima na wafugaji pia kila Halmashauri zinatakiwa
kujituma kwa bidii na kuachana na tabia ya kulalamika kuwa hawajapata
zawadi

Alifafanua kuwa,tabia ya kutojituma ipasavyo na kutotumia mbinu bora
za kilimo kwanza kwa watazamaji ndio inayochangia kwa kiwango kikubwa
Halamashauri zilizokosa zawadi kuona kuwa walionewa na majaji

Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa TASO bw Athur Kitonga alisema kuwa
lengo la chama hicho ni kuendeleza sekta ya Kilimo na wafugaji kwa
kila mwaka lakini Halmashaauri bado hazipeleki wafugaji na wakulima
kujifunza katika mabanda yao mpaka ifike msimu wa maonesho ya Nane
Nane.

MWISHO

NGORONGORO YATOA MICHE LAKI TATU KWA AJILI YA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI



Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)imetoa miche ya miti laki tatu
kwa shule za Sekondari na Msingi ambazo zinapakana na Mamlaka hiyo
huku lengo halisi likiwa ni kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa misitu
pamoja na kuhifadhi mazingira

Akiongea na waandishi wa habari mwisho wa wiki Afisa Misitu wa mamlaka
hiyo ambaye Ni Bw Naaman Naaman alisema kuwa huo ni mpango mojawapo wa
mamalaka hiyo wa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakuwa na elimu ya
misitu ili wawe mabalozi wazuri wa mazingira

Bw Naaman alisema kuwa mradi huo wa kutoa miche ya miti ambayo ni ya
matunda, mbao, na vivuli ulianza rasmi mwaka 2009 na mpaka sasa baadhi
ya shule za sekondari na msingi zimeshanufaika huku shule nyingine
zikianza rasmi kuzalisha miche yao

Alifafanua kuwa toka kuanza kwa mradi huo ambao mpaka sasa umegharimu
kiasi chazaidi ya Milioni mbili umeweza kuwa na faida kubwa sana
tofauti na hapo awali ambapo mradi huo haukuwepo kwenye mpango wa
mamlaka hiyo

Akitaja faida hizo alisema kuwa ni pamoja na wanafunzi kuanza
kiujifunza aina mbalimbali ya miti toka wakiwa shuleni huku hali hiyo
ikiweza kuwafanya wao waweze kudyahifadhi mazingira na kuona kuwa kuna
umuhimu wa kuhifadhi mazingira

Faida nyingine aliyoitaja ni pamoja na kuanza kujijengea tabia ya kuwa
na misitu ya kifamilia ili kuweza kukabiliana na tatizo la mabadiliko
tabia Nchi ambayo limeathiri sana eneo hilo la Ngorongoro.

Wakati huo huo alisema kuwa mpaka sasa mradi huo unakabiliwa na
changamoto kubwa ya uharibifu wa misitu hasa  kwa upande wa wafugaji
kwani bado mifugo yao inaharibu misitu ambayo imeoteshwa na mamlaka
hiyo.

Kutokana na Changamoto hiyo alisema kuwa ni vema kama viongozi wa
Kijiji wakajiwekea utaratibu wa kuelezea jamii umuhimu wa mradi huo
lakini pia umuhimu wa kuhifadhi mazingira ili kuepusha eneo hilo na
ukame .

MWISHO

UKOSEFU WA GARI LA KUBEBEA MAZIWA WASABABISHA MAZIWA LITA 700 KUSHINDWA KUUZIKA KILA SIKU WILAYANI KARATU



Kiwanda Cha Ayalable Dairy kilichopo katika Wilaya ya Karatu Mkoani
Arusha kinakabiliwa na changamoto ya usafiri hali ambayo inasababisha
waweze kupokea maziwa lita 800 kwa siku badala ya lita 1500 kwa siku
moja kutoka kwa wafugaji jambo ambalo wakati mwingine linasababisha
hasara kubwa sana kwa wafugaji pamoja na matumizi mabaya ya maziwa

Akiongea na Waandishi wa habari wiki hii wilayani humo mtaalamu wa
maziwa wa wilaya hiyo ambaye ni Care Elias alisema kuwa changamoto
hiyo inasababisha madhara makubwa sana kwa wafugaji

Alifafanua kuwa hapo awali walikuwa wanapata maziwa machache sana
kutoka kwa wafugaji lakini kwa sasa maziwa ni mengi sana katika wilaya
hiyo ya Karatu ingawaje sehemu nyingi sana zenye maziwa bado zipo
mbali na eneo la mji hali ambayo inasababisha maziwa yashindwe kufika
katika kiwanda hich

Kutokana na changamoto hiyo alidai kuwa maziwa yanayopatikana kwa
ajili ya matumizi ya kiwanda ni machache sana ingawaje kwa huko
viijijini zaidi maziwa yanazalisha lakini yanashindwa kufika kiwandani


Akiongelea hali ya uzalishaji wa maziwa katika Wilaya hiyo ya Karatu
alidai kuwa uzalishaji wa maziwa umeongezeka sana tofauti na Miaka ya
nyuma ambapo Wilaya hiyo ilikuwa inapata maziwa kidogo sana

Alisema kuwa kwa sasa kiasi cha lita zaidi ya elfu nne kinazalishwa na
wafugaji wa Wilaya hiyo ya Karatu lakini hapo awali kiasi cha lita
elfu moja pekee ndicho kilichokuwa kinazalishwa hali ambayo wakati
mwingine ilikuwa inasababisha uhaba wa maziwa

Alimalizia kwa kusema kuwa pia kituo hicho kilijengwa kwa ufadhili wa
Mamlaka ya Ngorongoro hivyo basi ili kuweza kuokoa kiasi kikubwa cha
maziwa ambacho kinapotea kila siku ni vema kama mamlaka hiyo ingeweza
kuangalia upya tena namna ya kuwapa gari ambalo litaweza kubeba maziwa
hayo kutoka Vijijini zaidi na kuleta katika kiwanda hicho cha Ayalabe

Mwisho

NGORONGORO YATOA NGOMBE 20 ZENYE THAMANI YA MILIONI 20 KWA WANACHI WA WILAYA YA KARATU



Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA)imefanikiwa kutoa Ngombe 20 wa
kisasa wenye thamani ya zaidi ya milioni 20 kwa vijiji vinne vya
Wilaya ya Karatu kwa madhumuni ya kuendeleza Uhifadhi wa maliasili
ndani ya Vijiji hivyo.

Akiongea na waandishi wa habari mapema wiki hii Afisa Ugani wa Mamlaka
hiyo ambaye ni Bw Salustin Hallu alisema kuwa huo ni moja ya miradi
inayotekelezwa na mamlaka hiyo

Alisema kuwa mradi huo ambao hapo awali ulianza rasmi na Ngombe wa
kisasa 20 uliweza kuwa na manufaa makubwa sana kwa Vijiji vya Troma,
Ayalabe, lositete,na Upperutele ambapo hapo awali baadhi ya wafugaji
kwenye vijiji hivyo walikuwa wanalazimika kuchunga ndani ya hifadhi

Alifaafanua kuwa mpaka sasa zaidi ya familia 98 kwenye mradi huo
tayari wameshanufaika kwa kuwa kila familia moja sasa ina ngombe wa
kisasa mmoja na lengo halisi likiwa ni kuhakikisha kuwa kila familia
inajijengea uwezo wa kuchunga ndani na wala sio kutoa mifugo kwenda
kutafuta malisho nje

“Ngorongoro inalinda sana ujirani mwema na wananchi wake na ndio maana
tukaona kuwa badala ya kuwakataza tu wananchi wasiingie kwenye pori
ambapo ni hatari kwa maisha yao wao pamoja na mifugo lakini pia tuwape
mbinu mbadala za kuhakikisha kuwa wanajikomboa ndio maana tukaanzisha
huu mpango ambao umeonekana kuwasaida sana wananchi wa hivi
vijiji”aliongeza bw Hallu

Awali alisema Mamlaka pia bado ina mkakati mbalimbali wa kuhakikisha
kuwa wanaweza kufikia familia zote sanjari na kuwapa elimu mbalimbali
juu ya umuhimu wa kufuga ndani laki ni pia kuwapa mbinu imara ambazo
zinatakiwa kutumiwa na wafugaji wa kisasa zaidi

Akiongea kwa niaba ya familia 98 ambazo zimenufaika na mradi huo wa
ngombe wa kisasa kutoka Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro bi Emirita
Martin alidai kuwa pamoja na kuwa wamepata Ngombe lakini bado Mradi
huo unapaswa kuongezewa ngombe ambao wataweza kuwanufaisha wanawake

Bi Emirita alibainisha kuwa kama kila Boma na familia zitapa Ngombe
mmoja ambaye atazaliana basi wakina mama wataondokana na dhana ya kuwa
tegemezi kwenye maisha ya kifamilia kwani ufugaji unabadilisha maisha
duni na maskini ambayo wanayo baadhi ya wanawake katika Wilaya hiyo ya
Karatu

MWISHO

MWANDRI AWATAKA WAKRISTO KUSOMA VITABU VYA MUNGU KULIKO VENYE SIMULIZI ZISIZOJENGA JAMII

Na Bety Alex, Arusha



Waziri Agrey Mwandri amewataka wakristo kuachana na tabia ya kukwepa kujisomea vitabu mbalimbali ambavyo vinaongeza maarifa ya kiroho na kimwili kwani kwa njia ya vitabu hata maarifa juu ya ufalme wa Mungu nayo yanaongezeka sana

Mwandri aliyasema hayo wiki iliyopita katika kanisa la Winner Chapel Intrenational Arusha lililopo maeneo ya Kaloleni Mjini hapa wakati akizindua rasmi Kitabu kilichoandaliwa na Muinjilisti Paul Dickson kijulikanacho kama Ufalmwe wa Mungu hutekwa na wenye nguvu.

Alisema,kwa sasa wapo baadhi ya wakristo ambao wanapenda kujisomea vitabu ambavuyo havina maslahi na Mungu na badala yake vitabu hivyo vinahamsisha dhambi jambo ambalo kwa sasa wanatakiwa kulikataa

Alifafanua kuwa kama kila mkristo atahakikisha kuwa hapotezi muda wake mwingi kwenye vitabu hivyo a,mbavyo havijengi basi ni wazi kuwa hta dhambi ndani ya mkoa wa Arusha lakini Tanzania kwa ujmla nazo zitapungua kwa kiwango

Alibainisha kuwa kwa kusoma vitabu ambavyo vina madharai ya mwenendo wa Kimungu kunasaidia sana kuhimiza hata nguvu za Mungu kushuka na kuongoza katika mambo mbalimbali.

“jamani jiwekeeni utaratibu wa kuhakikisha kuwa mnasoma vitabu venye madhari ya Kimungu msinione hapa napambana kweli kule Bungeni lakini niwaambieni kuwa muda wangu mimi natumia hivi hivi vitabu vya mungu kujisomea na kuhakikisha kuwa naktafuta hata suluhu kule Bungeni hivyo basi igeni mfano huu “aliongeza Mwandri

Katika hatua nyingine Mwandishi wa kitabu hicho ambaye ni Muinjilisti Paul Dickson alisema kuwa lengo na maudhui ya kitabu hicho kijulikanacho kama Ufalme wa Mungu hutekwa na wenye nguvu, kina malengo ya kuhakikisha kuwa kinawakomboa baadhi ya watu katika ufalme wa Mungu

Muinjlisti huyo alidai kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu ambao wanatamani sana kuwa na falme wa Mungu lakini bado hawajaju hata siri za kuweza kuuteka ufalme huo hali ambayo wakati mwingine inasababisha waone kama ni wakosaji

“hiki kitabu kina siri nyingi sana za uponyaji na jinsi ya kuuteka ufalme wa Mungu hivyo basi natamani kuona kuwa watuw a sasa hususani mkoa wa Arusha na Tanzania wanaweza kuinuka  na kutoka katika hali Fulani hata za umaskini kwa kuwa ufalme wa Mungu kuuteka ni bure kabisa’aliongeza muinjilisti huyo

Alimalizia kwa kusema kuwa pamoja na kuwa vitabu vya Mungu vinaweza hata kuokoa lakini bado ipo changamoto kubwa sana kwa waaandishi wa vitabu kwa kuwa baadhi yao huandika zaidi vitabu ambavyo vinahusu mapenzi na kusahau vitabu vya kuwakomboa watu jambo ambalo si jema kwa maendeleo ya watu

MWISHO

UHAMIAJI YATARAJIA KUKUSANYA BILIONI 85



Na mwandishi wetu Arusha

Idara ya Uhamiaji hapa nchini inatrajia kukusanya kiasi cha zaidi ya
Bilioni 85 kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 ambapo makusanyo hayo
yanatokana na mapato mbalimbali ya idara hiyo ambayo ipo chini ya
Wizara ya mambo ya ndani.

Hayo yameelezwa na Kamishana wa utawala na fedha katika idara hiyo
ambaye ni Bw Piniel Mgonja wakati akiongea  katika mkutano wa
tathimini wa utendaji kazi kwa wahasibu wa idara wa uhamiaji
unaondelea Jijini hapa

Piniel alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinaweza kupatikana na
kuvuka malengo kutokana na ukusanyaji wa Madhuhuli kuboreshwa zaidi
tofauti na miaka ya nyuma hali ambayo mpaka sasa itasaidia sana
kuongezeka kwa mapato ya idara hiyo.


Mbali na hayo alisema kuwa  hata kwa sasa vipo  baadhi ya vyanzo
vingine ambavyo  navyo vimechangia sana kuongeza mapato katika idara
hiyo ambapo vyanzo hivyo ni pamoja  vyanzo vya vibali vya kuishi
Nchini, huduma za Pasipoti, Hati za kusafiria,huduma ya uraia ,Viza
kwa wageni wanaoishi hapa Nchini

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa bado idara ya uhamiaji hapa nchini
inakabiliwa na  changamoto kubwa ambayo ni ukosefu wa huduma za
kibenki katika baadhi ya vituo vya uhamiaji hapa nchini hali ambayo
wakati mwingine inasababisha upotevu na umanifu wa kifedha kwa
wafanyakazi pamoja na wadau wa uhamiaji

Alisema kuwa hali hiyo  si nzuri sana kwani nayo inachangia sana
kupunguza hata mapato ya Serikali kwani baadhi ya mapato huwa
yanapungua au kupotea kabisa kutokana na ukosefu wa huduma za kibenki.

Awali Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani
Nchi, bw Mbarak Abdulwakil alisema kuwa wahasibu katika wizara hiyo
wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,Kanuni , na taratibu
zilizopo kwani usimamizi wa fedha unataka usimamizi wa hali ya juu
sana kwani fedha zinaushawishi mwingi sana

Alisistiza huduma ya malipo ya fedha inatakiwa kufanyika kwa njia ya
benki na kwa wakati na kwamba katika ukusanyaji wa maduhuli au katika
matumizi ya fedha na rasilimali nyingine benki ndio mahala sahihi pa
kuweka fedha hizo ili kuondo kasoro zinazoweza kujitokeza.

MWISHO

VIONGOZI WASIOWAJIBIKA CHANZO CHA NCHI KUWA MASKINI INGAWAJE INA RASILIMALI ZA KUTOSHA


Na Queen Lema, Arusha

IMEELEZWA kuwa dhana ya kutowajibika kwa baadhi ya Viongozi wa sekta mbalimbali hapa nchini imesababisha Nchi ya Tanzania kuonekana maskini ingawaje ina rasilimali nyingi sana ambazo zingeweza kuwanufaisha jamii

Hayo yameelezwa juzi na Naibu Waziri wa maliasili na utalii,Bw Lazaro Nyalandu wakati akiongea kwenye maafali ya nne ya chuo cha habari maalumu kilichopo katika eneo la Ngaramtoni Jijini hapa.

Bw Nyalandu alisema kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya viongozi wamejisahau katika uwajibikaji wao na badala yake wanajiweka kwenye utaratibu wanaoutaka wao hali ambayo inasababisha kazi na malengo mbalimbali ya taifa kukwama huku nao wananchi wakiendelea kulaumu  Serikali.

Alisema kuwa hali hiyo ya kutowajibika kwa baadhi ya viongozi wa sekta mbalimbali ndio iliyosababisha Tanzania ya sasa kuonekana kama ni mojawapo ya nchi maskini duniani ingawaje kuna rasilimali za kutosha ambazo kama zingetumika basi zingeweza kuwanufaisha watanzania wote

Alisema ili maendeleo ya nchi ya Tanzania yaweze kuja ni lazima kila kiongozi ahakikishe kuwa anawajibika ipasavyo lakini pia ahakikishe kuwa anakuwa mbunifu wa kuweza kubuni aina mbalimbali ya njia ambazo zitasababisha nchi isionekane kama maskini lakini pia hata rasilimali nazo ziweze kuwanufaisha wazawa


Awali mkuu wa chuo hicho cha habari Maalumu BwJackson Kaluzi alisema kuwa pamoja na kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ambayo inawasaida vijana wa kitanzania lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali

Bw Jackson alitaja Changamoto hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa Ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuapanua eneo la chuo jambo ambalo mpaka sasa chuo hicho kimeshindwa kupanua eneo lake


            MWISHO

MFANYAKAZI WA TANZANITE APIGWA RISASI

MFANYAKAZI wa kampuni ya uwekezaji ya Tanzanite One inayochimba madini eneo la Mirerani, wilayani Simanjiro, Willy Mushi (), ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoaminika kuwa ni wachimbaji wadogo baada ya kukutana mgodini chini ya ardhi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo alilosema lilitokea Saa 6:00 usiku wa kuamkia jana na tayari ametuma timu ya upelelezi unaoongozswa na Afisa upelelezi wa mkoa huo, kuchunguza zaidi tukio hilo.
Marehemu alipigwa risasi mbili kufuani upande wa kushoto alipoongozana na mfanyakazi mwenzake Kennedy Masimbaji kukikagua eneo la mgodi unaoingiliana na migodi ya wachimaji wadogo.
“Tulipofika kwenye mitobozano ambako kumepangwa mifuko ya viroba vya mchanga kutenganisha mgodi wetu na ile ya wachimbaji wadogo, ghafla tukashambuliwa kwa risasi ambazo zote zilimuingia marehemu kifuani na kufariki papo hapo,” alisema Masimbaji
Mfanyakazi mwingine wa Tanzanite One, leonard Paul alisema tukio hilo ni muendelezo wa mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na wachimbaji wadogo dhidi ya wafanyakazi wa mwekezaji pindi wanapokutana chini ya ardhi ambapo siku kadhaa zilizopita uongozi ulilazimika kusimamisha kazi kutoa fursa ya polisi kuchunguzi migogoro ya mitobozano.
 “Serikali lazima sasa ichukue hatua kuzuia matumizi ya silaha za moto chini ya migodi,” alisema Paul
Kwa mujibu wa Mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Tumsifu Mushi, marehemu ameacha mjane na watoto wanne na taratibu za mazishi zinaendelea.
Mwisho.

Monday, May 6, 2013

Bilion 9.8 zatengwa kwa ajili mikopo kwa wachimbaji wadogo

Na Wankyo Gati,arusha

Serikali imetenga  sh.bilioni 9.8 kwa ajili ya mikopo ya vifaa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima ili kuboresha uchimbaji wao na watakopeshwa kupitia vikundi watakavyojiunga na itakuwa mkopo endelevu ili kuinua sekta hiyo ya madini kupitia wachimbaji hao.
Hayo yalisemwa leo na Kamishna wa madini wa kanda ya kaskazini Eng.Benjamini Mchwampaka  wakati wa mahojiano na waaandishi wa habari yaliyofanyika katika ofisi za kanda hiyo zilizoko mkoani arusha.

Alisema kuwa kupitia mikopo hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa wachimbaji hao kupata vifaaa hivyo ili kuweza kuinua uchimbaji wao na kuwa wa kisasa zaidi ili kuongeza uzalishaji wa madini nchini ambapo hivi sasa wamekuwa wakikwamishwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa hali ambayo wanachimba ila hawapati madini ya kutosha.

Ameongeza kuwa wachimbaji wadogo wa kanda ya kaskazini  bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali  katika uzalishaji madini ikiwemo  kutokuwa na vifaa vya uchimbnaji vya kisasa ,bei kubwa ya milipuko na elimu ndogo ya uchimbaji madini hayo  hali ambayo inakwamisha jitihada zao za kuchimba madini hayo na kuwarudisha nyuma katika kujikwamua kiuchumi
.
Alisema kuwa hivi sasa wachimbaji wadogo walio wengi wanachimba kwa mazoea na vifaa duni ambapo elimu ya utambuzi madini  sehemu yalipo ni ndogo hali ambayo inasababisha kutopata madini yakutosha na kutumia gharama kubwa zaidi.

Eng.Mchwampaka alisema kuwa katika kanda hii wachimbaji wamekuwa wakichimba kiholela bila lessen hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao na hata kusababisha kifo na madhara mbalimbali ambapo  maeneo hayo yanachimbwa kwa kesi sana  hali ambayo ni hatari kwa  badala yake wachimbaji wafate taratibu za kuchimba eneo tengefu kwa madini kwa maendeleo yao na usalama wa maisha yao kuepuka kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Aidha aliongeza kuwa hivi sasa ofisi ya kanda imejiwekea mkakati mbalimbali ikiwemo kusogeza huduma karibu na wachimbaji katika kanda hii hususan kutoa elimu ,ya uchimbaji wa madini kitaalamu zaidi,hali ya masoko ,afya migodini  ,ajira na kutoa mafunzo kwa vitendo ya namna ya ulipuaji  mogodini sambamba na watatoa fursa ya namna ya uchimbaji salama na wenye tija na maendeleo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.

Eng.Mchwampakka alisema kuwa hivi sasa wako kwenye mchakato wa kuandaa maonyesho ya vito ,na madini mbalimbali  yatakayofanyika oktoba 28 hadi 30 mwaka huu mkoani hapa  ambapo watahiusisha wafanyabiashara wote ncnini na nchi jiran ikiwemo Kenya ,DRC kongo ,Zambia ,Madagascar ,Malawi ,Ethiopia ,Afrika ya kusini na Msumbiji ili kuweza kubadilishana uzoefu na kuweza kuongeza ushindani katika sekta ya madini nchini.
Mwisho.

WANANCHI WALALAMIKA KIJIJI KUKOSA MAPATO KWA MIAKA MITANO MWENYEKITI ADAI KUWA ANAONEWA VWIVU NA WANANCHI

Na Queen Lema,ARISHA

WANANCHI WALALAMIKA KIJIJI KUKOSA MAPATO KWA MIAKA MITANO MWENYEKITI ADAI KUWA ANAONEWA VWIVU NA WANANCHI

Wanananchi wa Kijiji cha Ilikirioti Kata ya Moivo Wilaya ya Arusha wamemuomba Mkuu wa wilaya  Munasa Nyirembe  kuingilia kati kwenye uongozi wa kijiji hicho kwa kuwa uongozi huo unadai kuwa toka mwaka 2009 mpaka sasa hawajafanikiwa kupata mapato ya aiana yoyote ile.

Wananchi hao waliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Prosper Steven ili kujadili ili kuweza kusoma matumizi ya kijiji hicho.

Wananchi hao walidai kuwa ni aibu kubwa sana kuona kuwa kila siku ndani ya kijiji hicho wanapata asilimia kumi ya mashamba yanaouzwa lakini pia hata michango lakini uongozi wa kijiji unadai kuwa hauna fedha yoyote ile toka mwaka 2009

Aidha walidai kuwa kwa kukosa kijiji kukosa mapato huku wananchi wakiwa wanashangishwa fedha mbalimbali kunaashiria harufu ya Rushwa lakini pia harufu ya ukandamizaji wa hali ya juu jambo amblo kama Mkuu wa Wilaya hataingilia kati basi huenda liksababisha matatizo makubwa sana

“tunamuomba Mkuu wa wilaya hii pamoja na mkurugenzi waje hapa Kijijini waje wajione hali ilivyo hatuna hata barabara lakini tunaambiwa kuwa eti mapato hayapo na sisi tunachanga kila siku na mtu akija kununua shamba ni lazima atoe asilimia kumi sasa kama hali itaendelea hivi je mwisho wake utakuwa ni upi kama sio kudodondosha damu?walihoji wananchi hao.

Lakini mbali na hayo walidai kuwa ndani ya Kijiji hicho hakuna ulinzi pamoja na usalama wa mali zao kutokana na kituo cha polisi kuwa mbali na makazi yao hali ambayo inatakiwa kutatuliwa kwa haraka sana

Walifafanua kuwa umbali ambaop upo ndani ya Kijiji hicho unasababisha baadhi ya waahalifu kuiba huku wakiwa wanajiamini kabisa kwa kile ambacho wanakifanya kwa kuwa mpaka polisi watoke mjini na kufika katika eneo hilo watakuwa wameshamaliza kuiba wananchokitaka jambo ambalo wakati mwingine linasababisha Umaskini wa kutisha.

Awali Mwenyekiti wa Kijiji ghicho Prosper Steven alidai kuwa kinachoendelea kijijini hapo wivu kwa kuwa amejenga nyumba kubwa nay a kifahari lakini kijiji hakina mapato ya iana yoyote ile hivyo wananchi hawapswi kukosa imani nae

“nawashangaa sana hawa wananchi wanaosema kuwa kijiji hakina mapato kwa miaka mimi najua kuwa hii ni roho ya wivu kwa kuwa nimejenga nyumba ya kifahari kuliko wao na ndio maana wanaongoza kwa kudai kuwa ningatuke kwa kuwa ninachakachua mapato ya Kijiji”alisema Prosper.

Mwisho

BALOZI WA VATIKAN ALIPUKIWA NA BOMU,MMOJA AFA WENGINE ZAIDI YA THELATHINI WAJERULIWA VIBAYA KANISANI. Katika hali isiyokuwa ya kawaida kundi la watu wasiofahamika wametupa bomu katika kanisa la Roman Katoliki la Mt Joseph mfanyakazi liliopo Olasiti Mjini hapa na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia huku wengine thelathini wakiwa majerui Bomu hilo lilirushwa na watu wasiojulikana majira ya saa nne za asubuhi ambapo kanisa hilo lilikuwa linazinduliwa na a balozi wa Vatikan nchini, Fransisko Padika Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea asubuhi wakati balozi huyo akijiandaa kukata utepe wa kanisa hilo jipya Sabas alisema kuwa wakati balozi huyo anakata utepe huo ghafla mtu asiojulika alirushwa bomu ambalo liliweza kuwajerui watu huku likisababisha mauti ya mtoto mmoja "huyu balozi alikuwa hapa Arusha toka siku ya alhamisi lakini leo sisi tulikuwa na ulinzi wa kutosha juu yake lakini wakati anakata utepe ghafla alilipukiwa na bomu hali ambayo ilisababisha vurugu kubwa sana katika kanisa hilo jipya"alisema Sabasi Pia aliongeza kuwa mpaka sasa polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye hajajulikana makazi yake lakini uchunguzi unaendelea huku jeshi hilo likiomba msaada wa wananchi lakini pia msaada wa majeshi mengine ili kuweza kuchunguza tatizo hilo. wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiongea kwa niaba ya Serikali alisema kuwa wananchi wa jiji la Arusha hawapaswi kujiuliza chanzo na kuhusisha tukio hilo na imani za kidini bali wanatakiwa kutoa ushirikiano alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa majerui wote wanapata matibabu ingawaje bado kuna ukosefu wa vifaa katika hospitali ya mkoa wa Arusha (Mt Meru) "kazi ya uchunguzi tunatakiwa kuachia vyombo vya usalama pekee tuwe watulivu na tutoe taarifa kwa Polisi lakini pia tunaomba msaada wa madaktari wa ziada katika hospitali kwani hawa majerui wameumia vibaya sana"alifafanua Magesa Wakati huohuo Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema alisema kuwa matukio ya uharibifu wa makanisa ni mwendelezo wa kile kilichotokea Zanzibar, na Dar es Saalam lakiniSerikali bado haiskii wala kuona mpaka idadi kubwa sana ya watu wafe. Lema alisema kuwa lazima mambo kama hayo yatatokea kwa kuwa wanasiasa wa sasa wanatafuta umaarufu kwenye makanisa hususani uzinduzi bila kujua na kutambua kuwa kuna hatari kama hiyo. Aliyataka makanisa kuachana na tabia ya kuwa karibu na wanasiasa na badala yake wahakikishe kuwa wanajitegemea kwa michango yao wao wenyewe kwan kuwa siasa haziendi kabisa kwenye makanisa. Hataivyo Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za mount Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina Fredirik, Joram kisera, Novelt John, Rose pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, . Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim. Wakati huo huo jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu kumnusuru mwendesha boda boda mmoja katika eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao. MWISHO

picha ya kwanza ni jengo la kanisa la st joseph mfanyakazi mara baada ya baadhi ya waumini wake kupigwa na mabomu



baadhi ya majerui katika tukio hilo


majeruhi wengine tena katika tukio hilo


BALOZI WA VATIKAN ALIPUKIWA NA BOMU,MMOJA AFA WENGINE ZAIDI YA THELATHINI WAJERULIWA VIBAYA KANISANI.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kundi la watu wasiofahamika wametupa bomu katika kanisa la
Roman Katoliki la Mt Joseph mfanyakazi liliopo Olasiti Mjini hapa na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia huku wengine thelathini wakiwa majerui

Bomu hilo lilirushwa na watu wasiojulikana majira ya saa nne za asubuhi ambapo kanisa hilo lilikuwa linazinduliwa na
a balozi wa Vatikan nchini, Fransisko  Padika
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas  alisema kuwa tukio hilo lilitokea asubuhi wakati balozi huyo akijiandaa kukata utepe wa kanisa hilo jipya

Sabas alisema kuwa  wakati balozi huyo anakata utepe huo ghafla mtu asiojulika alirushwa bomu ambalo liliweza kuwajerui watu huku likisababisha mauti ya mtoto mmoja

"huyu balozi alikuwa hapa Arusha toka siku ya alhamisi lakini leo sisi tulikuwa na ulinzi wa kutosha juu yake lakini wakati anakata utepe ghafla alilipukiwa na bomu hali ambayo ilisababisha vurugu kubwa sana katika kanisa hilo jipya"alisema Sabasi

Pia aliongeza kuwa mpaka sasa polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye hajajulikana makazi yake lakini uchunguzi unaendelea huku jeshi hilo likiomba msaada wa wananchi lakini pia msaada wa  majeshi mengine ili kuweza kuchunguza tatizo hilo.

wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiongea kwa niaba ya Serikali alisema kuwa wananchi wa jiji la Arusha hawapaswi kujiuliza chanzo na kuhusisha tukio hilo na imani za kidini bali wanatakiwa kutoa ushirikiano

alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa majerui wote wanapata matibabu ingawaje bado kuna ukosefu wa vifaa katika hospitali ya mkoa wa Arusha (Mt Meru)

"kazi ya uchunguzi tunatakiwa kuachia vyombo vya usalama pekee tuwe watulivu na tutoe taarifa kwa Polisi lakini pia tunaomba msaada wa madaktari wa ziada katika hospitali kwani hawa majerui wameumia vibaya sana"alifafanua Magesa

Wakati huohuo Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema alisema kuwa matukio ya uharibifu wa makanisa ni mwendelezo wa kile kilichotokea Zanzibar, na Dar es Saalam lakiniSerikali bado haiskii wala kuona mpaka idadi kubwa sana ya watu wafe.

Lema alisema kuwa lazima mambo kama hayo yatatokea kwa kuwa wanasiasa wa sasa wanatafuta umaarufu kwenye makanisa hususani uzinduzi bila kujua na kutambua kuwa kuna hatari kama hiyo.

Aliyataka makanisa kuachana na tabia ya kuwa karibu na wanasiasa na badala yake wahakikishe kuwa wanajitegemea kwa michango yao wao wenyewe kwan kuwa siasa haziendi kabisa kwenye makanisa.

Hataivyo Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital z mount Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina   Fredirik, Joram  kisera, Novelt  John, Rose  pius, John  James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt  John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .

Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim.



Wakati huo huo  jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu kumnusuru  mwendesha boda boda mmoja katika eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao.

MWISHO