Na Queen Lema, Arusha
IMEELEZWA kuwa dhana ya kutowajibika kwa baadhi ya Viongozi wa sekta mbalimbali hapa nchini imesababisha Nchi ya Tanzania kuonekana maskini ingawaje ina rasilimali nyingi sana ambazo zingeweza kuwanufaisha jamii
Hayo yameelezwa juzi na Naibu Waziri wa maliasili na utalii,Bw Lazaro Nyalandu wakati akiongea kwenye maafali ya nne ya chuo cha habari maalumu kilichopo katika eneo la Ngaramtoni Jijini hapa.
Bw Nyalandu alisema kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya viongozi wamejisahau katika uwajibikaji wao na badala yake wanajiweka kwenye utaratibu wanaoutaka wao hali ambayo inasababisha kazi na malengo mbalimbali ya taifa kukwama huku nao wananchi wakiendelea kulaumu Serikali.
Alisema kuwa hali hiyo ya kutowajibika kwa baadhi ya viongozi wa sekta mbalimbali ndio iliyosababisha Tanzania ya sasa kuonekana kama ni mojawapo ya nchi maskini duniani ingawaje kuna rasilimali za kutosha ambazo kama zingetumika basi zingeweza kuwanufaisha watanzania wote
Alisema ili maendeleo ya nchi ya Tanzania yaweze kuja ni lazima kila kiongozi ahakikishe kuwa anawajibika ipasavyo lakini pia ahakikishe kuwa anakuwa mbunifu wa kuweza kubuni aina mbalimbali ya njia ambazo zitasababisha nchi isionekane kama maskini lakini pia hata rasilimali nazo ziweze kuwanufaisha wazawa
Awali mkuu wa chuo hicho cha habari Maalumu BwJackson Kaluzi alisema kuwa pamoja na kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ambayo inawasaida vijana wa kitanzania lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
Bw Jackson alitaja Changamoto hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa Ardhi ya kutosha kwa ajili ya kuapanua eneo la chuo jambo ambalo mpaka sasa chuo hicho kimeshindwa kupanua eneo lake
MWISHO
No comments:
Post a Comment