POLISI YAWAKAMATA MAJAMBAZI WANNE WALIOPORA MADINI YA
MILIONI 40 NA FEDHA KIASI CHA MILIONI 5
, Arusha
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwatia nguvuni majambazi wanne ambao walifanya tukio la wizi wa mfanyabiashara wa madini na kisha kumpora madini yenye thamani ya Milioni 40 pamoja na fedha taslimu Milioni 5.
aidha majambazi hayo yalifanya tukio hilo la kumvamia na
kumjerui mfanyabiashara wa madini aliyejulikana kwa jina la Abeli Musa(35)mnamo
Agust 23 majira ya saa nane na nusu mchana.
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Kamanda wa polisi
mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa kukamwatwa kwa majambazi hayo
kunatokana na taarifa za raia wema pamoja na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi
ambao waliingia kazini rasmi kwa ajili ya kuwasaka majambazi kuanzia siku ya
tukio.
Sabas alisema kuwa Majambazi hayo ambayo yamefahamika kwa
majina ya Shangai William(38)mkazi wa Sokoni one, Ally Habibu au dogoo
(23)mkazi wa Tabata Dar es saalam, Eugine Donas(28)mkazi wa makao Mapya
pamoja na Josephat Jerome(29)mkazi wa Sombetini ambapo walikamatwa
Agust 24 katika maeneo ya nyumba za kulala wageni Makao Mapya
Wakati huo huo alidai kuwa mara baada ya kuwamata majambazi
hao pia walifanikiwa kukamata vifaa walivyotumia katika tukio hilo na matukio
mengine ya uuaji yaliyotokea Jijini arusha
Ametaja Vifaa hivyo pamoja na silaha kuwa ni pamoja na
Bastola aina ya Browing Model 83 Cal 9 yenye namba 4738 huku ikiwa na risasi 10
pamoja na bastola ya LAMI ikiwa na Risasi 12.
Vifaa vingine ni pamoja na Gari aina ya Vist yenye namba za
usajili T 368 AUH huku pikipiki aina ya Skygo yenye namba T352CBW pamoja
na pikipiki nyingine yenye namba T 464 APH aina ya Honda nazo zikimatwa kwani
majambazi hayo yalitumia vifaa hivyo kwa ajili ya uporaji maeneo mbalimbali.
MWISHO
No comments:
Post a Comment