IMEBAINIKA kuwa kutokana na tabia ya Maaskofu na wasimamizi
mbalimbali wa makanisa kushindwa kuwafundisha wachungaji wao jinsi ya
kuitumikia jamii ya kikristo ndio chanzo pekee cha baadhi ya viongozi wa dini
kupata dharau ambazo haziwahusu.
Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Askofu Aminiel Mgonja
wa kanisa la Arusha Praise centre lilopo Sekei wakati akiongea na waumini wa
kanisa hilo juu ya maadalizi ya mahafali ya
wachungaji 30 wa kanisa hilo
yatakayofanyika mapema wiki ijayo
Askofu Mgonja alisema kuwa wasimamizi wa makanisa lakini pia
maskofu wanatakiwa kuwa na utaratibu a kuwafundisha mambao mbalimbali
wachungaji wao ili nao watakapofundisha waumini wawe na umoja na wala sio
mgawanyiko
Alisema, kupitia mafundisho ambayo yatakuwa yanatolewa mara
kwa mara juu ya wachungaji yartaweza kuwajenga kiimani lakini pia kiroho kwani
asilimia kubwa ya wachungaji wa sasa wanakabiliwa na mambo mengi sana
Alibainisha kuwa watakapojijenga kiroho na kiimani kutaweza
kuruhusu hata kazi ya bwana iweze kutendeka kwa wepesi zaidi kuliko pale ambapo
kazi ya kulinda na kuwahifadhi kondoo itakapofanywa na wachungaji pekee yao.
“kama wachungaji wakiharibu kazi ya bwana basi sifa chafu
haibaki kwao tu bali inabaki kwenye kanisa zima lakini pia inabaki kwa maaskofu
sasa kabla hatujakubali kuchafiliwa ni lazima sisi kama maaskofu tujiwekee
taratibu za kuwafunidhs kila mara hata kama
wanaelimu ya uchungaji”aliongeza Askofu huyo
Wakati huo huo alidai kuwa hata nao wachungaji wa sasa
wanatakiwa kuangalia zaidi msingi wa maandiko kuliko msingi wa mambo ya dunia
ambayo wakati mwingine wanasababisha wawe wachungaji wa shetani
Alisema ni vema kama wakawa
na tabia ya kufuata zaidi maadili na kuangalia ni aina ya huduma gani ambayo
wanaitoa kwa mkristo kuliko kuacha maadili na kisha kujikuta wakiwa wameshazama
ndani ya dhambi hivyo kusababisha madhara ya madharau ndani na hata nje ya
kanisa
Kanisa hilo
linataarajia kuwafanyia maafali wachungaji wake 30 ambao wamehitimu kozi na
mafunzo ya uchungaji huku somo kubwa kwao likiwa ni maadili ya uchungaji kwa
jamii yote hapa duniani
No comments:
Post a Comment