Na Queen Lema, Arusha
Wakulima wa Kanda ya kaskazini wameshauriwa kuhakikisha kuwa
wanaanzisha utaratibu maalumu wa kutegemea zaidi kilimo cha umwagiliaji kuliko
kutegemea kilimo cha majira ya mwaka kwani aina hiyo ya kilimo kwa sasa
inaonekana kupitwa na wakati.
Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Bw Elias Mshiu ambaye ni
Mwenyekiti wa chama cha wakulima Tanzania(TFA)wakati akiongea na gazeti hili
kuhusu hali ya kilimo kwa kanda ya kaskazini mapema jana
Aidha Bw Mshiu alisema kuwa inashangaza sana kuona kuwa asilimia kubwa ya wakulima
hasa wa kanda hii ya kaskazini bado wakiwa wanategenea kilimo cha mvua za Vuli
lakini pia mvua za masika hali ambayo ndiyo chanzo cha ukame
Alibainisha kuwa endapo kama wakulima watatumia zaidi aina
ya kilimo cha umwagiliaji ni wazi kuwa hata mazao nayo yatawweza kuongezeka
tofauti na sasa ambapo wapo baadhi ya wakulima ambao wanafanya kama kubahatisha tu
Alisema, Kilimo cha umwagiliaji kina tija kubwa sana kwa wakulima wa kanda hii hivyo basi ni vema hata kama nayo wizara ikahakikisha kuwa inatoa elimu
zaidi na fursa mbalimbali ili wakulima
wazoeee kuliko kutumia kilimo cha majira ya mwaka ambacho wakati mwingine
kinakataa kabisa.
Pia alisema katika Chama hicho cha TFAkwa sasa wameweza
kugundua changamoto hiyo ya wakulima wengi kutegemea zaidi kilimo cha majira ya
mwaka hivyo wamebuni mbinu na njia mbadala ambazo zitaweza kuifanya jamii iweze
kuondokana nacho kwa malengo ya kuongeza zaidi chakula
Alitaja Mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuweza kuwakopesha
lakini pia kuwawezesha wakulima vifaa mbalimbali kwa ajili ya umwagiliaji ili
waweze kufikia malengo yao
ambayo wamejiwekea.
“tulikaa na kisha kuona kuwa kuna umuhimu wa kuwasaidia hawa
wakulima ili wawe na elimu hii ya umwagiliaji lakini waweze kukopa hata vifaa
kwa ajili ya umwagiliaji katika mashamba yao na kwa kweli kama wote wataitiika
hata kuja kuchukua elimu hii basi kilimo kwa kanda hii kitaimarika
sana”aliongeza Bw Mshiu.
Alimalizia kwa kusema kuwa nao wakulima wanatakiwa
kubadilika na wanatakiwa pia kuachana na kilimo cha mazoea ambacho mara kwa
mara ndiocho kinachisababisha waonekane ni wakulima lakini faida hawana na
badala yake wafuate sheria,kanuni, na taratibu mbalimbali za Kilimo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment