VIJANA
ZAIDI 1000 WA UVCCM MERU, WAFUNGA BARABARA, WAVAMIA OFISI ZA CCM MKOA
WAKIDAI KUWA WAMECHOSHWA KUCHAGULIWA VIONGOZI NA MAKAO MAKUU
Na Queen Lema, Arusha
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida vijana zaidi ya 1000 ambao
ni wanachama wa umoja wa vijana chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya
Meru mkoa
wa Arusha wamevamia ofisi za chama hicho kuanzia ngazi ya Wilaya hadi
mkoa huku
wakidai kuwa Makao makuu ya chama hicho wamewaonea kwa kutangaza uamuzi
wao wa
kuwachagulia viongozi tofauti na matakwa yao ambapo wao walimchagua
Kamanda wao ambaye Ni John Palangyo ila CCM makao makuu walitofautiana
nao.
hataivyo maandamano hayo ambayo yaliratibiwa na wajumbe wa
UVCCM Meru yaliweza kusababisha shuguli mbalimbali za chama hicho kuanzia ofisi
ya Wilaya hadi Mkoa kusimama kwa kuwa wajumbe hao walilazimika kuingia kwa
nguvu ndani ya ofisi hizo na kisha kushinikiza kusikilizwa kwa madai yao
Akiongea kwa niaba ya wajumbe hao mmoja wa wajumbe hao
Joshua Mbwana "Mwarabu"alisema kuwa kilichosababisha waweze kufanya
maandamano hayo ambayo yalianzia kuanzia eneo la Usa River Mpaka Arusha ni
kuelezea umma kuwa wapo baadhi ya viongozi katika chama hicho ambao
wanawachagulia viongozi wa kuwaongoza bila kuwauliza
"hivi juzi tulikuwa na tulimchagua kamanda wetu ambaye
ni John Palangyo na tulimpitisha lakini baada ya jina kufika mkoani ghafa jina
lilibadilishwa kama haitoshi makao makuu wakasema kuwa wana mtu wao sasa je wao
ndio wanatuchagulia mtu wa kutuongoza au sisi kamwe hatutakubali na badala yake
tutapigana hadi mwisho hii tabia imetucosha sana"aliongeza Joshua
wakati huo huo alidai kuwa endapo kama hali hiyo itaendelea kufanyika ambapo wananchi, wajumbe, na wanachama watachagua kiongozi alafu makao makuu pamoja na uongozi wa Mkoa wakakataa basi mapambano yatakuwa makubwa sana.
wakati huo huo alidai kuwa endapo kama hali hiyo itaendelea kufanyika ambapo wananchi, wajumbe, na wanachama watachagua kiongozi alafu makao makuu pamoja na uongozi wa Mkoa wakakataa basi mapambano yatakuwa makubwa sana.
Kutokana na hilo mjumbe huyo alisema kuwa pamoja na kuwa
wamevamia ofisi za CCM wakiwa wanachama zaidi ya 300 bado kama hawatapewa
majibu yha kuridhisha juu ya kamanda wa vijana ambaye amechaguliwa kwa kura
zote na wajumbe wa baraza hilo basi ndani ya siku nne kutoka sasa huenda
wakaandamana hadi makao makuu ya ofisi za CCM
"tumesharatibu maandamano hayo na yataenda vizuri
itakuwa ni histori a kwa CCM kuchagulia viongozi kwa maslahi yao binafsi na
matakwa ya viongozi wa ngazi za juu hasa wale ambao wana malengo ya kugombea
nafasi za ubunge katika majimbo kwani ujumbe wetu ni lazima tutauweka wazi na
kila mtu aweze kuosoma lakini hata kuingia ndani ya ofisi hizo bila taarifa
wala kibali cha aina yoyote ile"aliongeza Joshua.
Hataivyo Katibu wa chama hicho Wilaya ya Meru, Langaeli
Akyoo alisema kuwa mchakato wa kumpata kiongozi ambaye vijana hao wanamtaka
ulienda vizuri na majina matatu yalifikishwa Dar es saalam makao makuu lakini
baadaye hayakurudi kama ilivyoratarjiwa
Akyoo alisema kuwa majina mawili yalirudi majina mawili
ambayo yana utata mkubwa ambapo utata huo ndio uliosababisha maandamano makubwa
kuanzia Meru hadi Arusha
"jamani maombi yenu nimeyapata
na ninapenda kuwaambia kuwa majina ambayo yalienda Dar es saalam makao makuu
yalirudishwa mawili ambayo yana utata na wao walisema kuwa mchakato unatakiwa
kuanza moja jambo ambalo sisi hatukubalini nalo kabisa"aliongeza Akyoo
Awali mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya hiyo Bw Elirehema
Mbisse alisema kuwa mchakato wa kumpata Kamanda huyo unaendelea na hivyo
amewataka wawe na subira ili waweze kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo
ambalo limesababisha ofisi za CCM
kusimamisha kazi kwa muda.
Hataivyo
Uongozi wa Uvccm kupitia kikao chake cha kamati ya utekelezaji
kilipendekeza majina matatu ambayo ni John .D.Palangyo, Sioi Solomoni
Sumari, na Daniel Mirisho Palangyo,na baadaye mutsari uliweza kupelekwa
mkoani ambapo Mkoa ulijiridhisha na majina hayo na uliweza kuhoji na
hatimaye waliweza kumpata John.D.Palangyo kama Kamanda wa Vijana Wilaya
ya Meru,lakini baadaye barua ilikuja na kudai kuwa kamanda wa Meru siyo
huyo jambo ambalo si la kweli.
No comments:
Post a Comment