Zaidi ya wakulima 500 kupewa elimu ya
rasilimali fedha.
,Arusha.
ZAIDI ya wakulima 500 kutoka katika kanda ya kaskazini
wanatarajiwa kupewa elimu ya Rasilimali fedha,na kuongeza ufahamu na uelewa juu
ya huduma mbalimbali za kifedha zitolewazo na Mabenki.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa chama cha wakulima wa mbogamboga,matunda
na viungo(TAHA) JacKline Mkindi wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na maonesho ya kuunganisha kilimo biashara na taasisi za kifedha
yatakayofanyika April 25 na 26 mwaka huu katika viwanja vya AVDRC Tengeru.
Alisema
kuwa,kwa sasa asilimia kubwa ya taasisi za kifedha zimekuwa zikiwakandamiza
wakulima kwa kuwatoza riba kubwa kwenye mikopo hali ambayo imekuwa
ikiwasababishia wakulima hao kupoteza imani na mikopo kutoka katika taasisi
hizo.
Alidai kuwa
hali hiyo imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa wakulima hao,kwani wakati
mwingine imewawia vigumu kushindwa kufikia malengo yao waliyojiwekea kutokana
na ukosefu wa fedha za kutosha katika kuendesha miradi yao midogomidogo.
‘kutokana na
changamoto hiyo sasa tumeamua kuandaa maonesho yatakayoweza kuwakutanisha taasisi
za kifedha pamoja na wakulima ambapo hapo taasisi hizo zitaweza kutambua
mahitaji ya wakulima,na jinsi ya kuweza kuwasaidia tofauti na hapo awali’alisema
Jackline .
Pia alisema
kuwa maonesho hayo yataenda sambasamba na uwasilishwaji wa mada mbalimbali
ikiwemo uaandaji bora wa mipango biashara,umuhimu wa soko la hisa katika
kuhakikisha upatikanaji wa mitaji wa muda mrefu,na matumizi bora ya mikopo
katika biashara hususani za kilimo ili
walengwa waweze kujifunza zaidi juu ya mbinu bora za kufikia na kupata mitaji
kwa kufanya biashara.
Kwa upande
wake mratibu wa mtandao wa Agri-Hub Tanzania Bw Tom Ole Sikar alisema kuwa maonesho
hayo yanalenga kuwawezesha wakulima pamoja na wamiliki wa biashara za kilimo
kama vile wachuuzi,wauzaji wa pembejeo na wasindikaji kutambua fursa mbalimbali
za mitaji pamoja na usalama wa kifedha zilizopo kwa biashara za kilimo.
Hata hivyo
alisema kuwa wadau ambao wengi wao ni wakulima wataweza kupata fursa ya
kutambua njia bora za kuboresha biashara na utoaji wa huduma kwa walengwa
pamoja na kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wengine wa kilimo waliofanikiwa
kutembelea maonesho yaliyopita.
MWISHO
No comments:
Post a Comment