SHULE YATOA UFADHILI WA MILIONI 90 KWA WANAFUNZI 90 KWA KILA MWAKA
SHULE
ya Sekondari Edmund iliopo Sinon Mjini Arusha imetenga kiasi cha zaidi
Milioni 90 kwa wanafunzi 90 kila mwaka kwa ajili ya kuwasaidia watoto
wanaotokea katika mazingira magumu huku lengo likiwa ni kuwaepusha na
mimba za utotoni lakini pia uvunjifu wa amani kwenye jamii
hataivyo fedha hizo zinatolewa na wafadhili wa nje ya nchi
pamoja na mfuko wa shule hiyo ujulikanao kama Mfuko wa Edmund ambao pia
huo unalenga kuhamasisha ufadhili wa ndani
Hayo yameelezwa
na Mkwabi Francis ambaye ni mkuu wa shule hiyo wakati akiongea na
wanafunzi, wazazi pamoja na walezi wa shule hiyo kwenye maafali ya nane
ambapo jumla ya wanafunzi 240 wanatarajia kuhitimu katika shule hiyo.
Mkwabi alisema kuwa mpango huo wa kuwasidia watoto wanaotokea
katika mazingira magumu umeweza kuwanufaisha watoto wanaotokea katika
vijiji vya Murieth, Mkono,Nadosoito,Ungalmtd, na Sinoni ambapo walengwa
ni wale wenye maitaji muhimu
alifafanua kuwa walengwa hao ni wale watoto wanaotokea katika
familia ambazo hazina uwezo,na mayatima ambapo watoto hao huweza
kukupewa ufadhili maalumu kwa ajili ya kusoma na kupata elimu ya
Sekondari.
"wafadhili wetu wakubwa wanatokea katika Nchi za Ausralia,
Newzeland,Iland, na Marekani na hawa wanatufanikikishia hawa watoto 90
kuweza kupata elimu yao bora sana ya Sekondari ingawaje na sasa sisi
tumejipanga kuhakikisha kuwa na sisi hapa hapa shuleni tunatoa ufadhili
kwa watoto wetu ili siku hata kama tukikosa wafadhili basi tunaweza
kusaidia jamii'aliongeza Mkwabi
Pia alisema kuwa nao wazazi wanapaswa kujua na kutambua kuwa
nao wana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwasaidia watoto hasa wale ambao
hawana uwezo wa kupata elimu ya sekondari kwani kupitia njia ya ufadhili
wa ndani inawezekana kabisa
"kama wazazi, na walezi wakiwa na tabia ya kuchangia sekta ya
maendeleo ya shule hasa mifuko ya shule basi wataweza kusaidia jamii na
hatutaweza kuwategemea zaidi wafadhili ambao wanatokea nje ya nchi
kwani wakati mwingine wanapokatisha ufadhili wao wanasababisha watoto
wawe kwenye hali ya uoga'aliongeza Mkwabi.
Wakati huo huo Wanafunzi wa shule hiyo ambao ni wahitimu
waliwashauri walimu wa shule hiyo lakini pia wale wa shule nyingine
kuachana na tabia ya kuwatenganisha wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka
cha nne dhidi ya wale wa kidato cha tano na sita kwani kwa kufanya
hivyo kunasababisha wale wa vidato vya chini kutopata hamasa ya kujiunga
au kufanya vema ili kuweza kujiunga na kidato cha tano na sita.
MWISHO
No comments:
Post a Comment