MADIWANI 23 MERU WATISHIA KUJIUZULU NA KUKUSANYA KADI ZA CCM
NA WANACHAMA WAKE.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida madiwani 23 kutokaa katika
Halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha wametishia kujiuzu wote katika nyadhifa zao
lakini pia kukusanya kadi zote za chama cha mapinduzi sanjari na kuongoza maelfu
ya wananchi kwenda kuchukua ardhi yao ambayo imetekwa
kinyemela,endapo kama Halmashauri hiyo
haitatoa tamko rasmi dhidi ya migogoro ya mashamba inayoendelea Wilayani Humo.
Aidha pia kadi ambazo zitakusanywa zitaweza kuwekwa chini ya
uangalizi maalumu ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na kazi yoyote ile ya chama
cha mapinduzi ikiwa ni fundisho kwa serikali dhidi ya vigogo wake wa Wizara ya Ardhi
ambao wanatumika katika migogoro ya ardhi katika Halmashauri Mbalimbali.
Madiwani hao waliyasema hayo ijumaa iliyopita katika baraza
la madiwani lililofanyika katika Halmashauri hiyo ambapo agenda ya migogoro ya
ardhi ilifanya baraza hilo
kujikuta likiwa linatoa tamko na vitisho vikubwa kwa watumishi wa Halmashauri
hiyo.
Akiongea kwa niaba ya madiwani wa Halmashauri hiyo bi
Mwanaidi Kimu alisema kuwa wameschoshwa kila siku kujadili agenda za migogoro
ya ardhi lakini hakuna utendaji wowte na badala yake wanabaki wakiwa na
kumbukumbnu ya vikao katika vichwa vyao hali ambayo kwa sasa imefika mwisho
Akitolea mfano moja yashamba lenye migogoro katika
Halmashauri hiyo,shamba la Madira
lililopo katika maeneo ya Seela Singisi ambalo
ni mali
halisi ya Halmasahuri hiyo lakini kwa sasa kuna migogoro ambayo inasababishwa
na baadhi ya viongozi jambo ambalo wamedai kuwa hawataweza kuvumilia bali
wataingia katika vita kwa mara nyingine
“kwa mfano hili shamba la Seela Singisi ni mali ya wananchi
wote wa Meru na hadi Raisi ameshaweka saini yake jamani litumike kwa ajili ya
matumizi ya kata zote za Meru lakini vigogo wanasema ni mali yao alafu bado
tumenyamaza tu haitawezekana tunaachia udiwani alafu htunaingia katika Vita kwa
mara nyingine”aliongeza Kimu
Katika hatua nyingine akiongea kwa niaba ya madiwani wanaume
,Wilson Nyitti alisema kuwa hali hiyo imesababisha kila wanpopita walazimke
kujikuta wakiwa wanazomewa ovyo na wananchi kwa kuwa wananchi wanafikiri kuwa
wao wananufaika na migogoro hiyo ya ardhi
Nyitti alisema wamechoka na hali hiyo ya kudhomewa na
kuabishwa mara kwa mara wakati hawausiki na kutokana na hilo sasa wamejipanga
kushirikiana na wananchi kurudi kwanye vita kwa mara nyingine kwa ajili ya
kuchukua ardhi yao lakini kupigana hata ikiwezekana kabisa.
“hili ni tamko rasmi tunatoa tunataka majibu ya migogoro hii
rasmi kama hatupewi itakuwa ni vita baina ya
Wameru na hawa wanaojichukulia ardhi kinyemelea, pia itakuwa ni huzuni kubwa
kwa CCM manake kwanza sisi wote hapa
tunatokea CCM uzalendo umetushinda kabisa”aliongeza Nyiti
Naye Mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo ya Meru, Goodson Majola
alisema kuwa tamko hilo
la kutaka kujiuzulu kwa madiwani 23 wote wa halmashauri hiyo lipo sawa kabisa
kwa kuwa migogoro yote ya ardhi inasababishwa na Viongozi wasio waadilifu
kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Wizara
Akiongelea suala la shamba hilo la Madira alisema kuwa Raisi Kikwete
tayari ameshatoa ardhi hiyo yenye jumla ya Hekari 360 lakini bado hawajaweza
kulitumia kutokana na vitisho ambavyo walikuwa wanavipata kutoka kwa vigogo
“mimi nasema kuwa tutajiuzulu wiki chache zinazokuja baada
ya kujiridhisha juu ya maangaiko haya ya ardhi ambayo yamedumu toka karne hadi
karne na ninasiistiza kuwa itakuwa ni kilio kwa CCM kwa kuwa wanchama wetu nao
tutaweka chini ya ulinzi hadi tutakapowaambia hawatajishugulisha na shuguli
yoyote ya chama”alisema Majola.
Majola alisema kuwa kujiuzulu kwao lakini pia kuondoka na
wanachama wote wa CCM katika Wilaya hiyo ni uzalendo wao kwa wananchi na hivyo
Hata CCM nao hawapaswi kuumia kwa hilo.
Hataivyo Halmashauri hiyo inaoongozwa na madiwani wote wa CCM
lakini pia kwa upande wa wapinzani inaongozwa na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki
Joshua Nassari.
MWISHO
No comments:
Post a Comment