IMEELEZWA kuwa ongezeko la vijana maeneo ya mijini chanzo
chake kikubwa ni kuwa asilimia kubwa ya vijana hasa wa vijijini bado hawajaweza
kutambua fursa za uchuni walizonazo hali
ambayo nayo inasababisha wimbi kubwa la watu mijini ambao hawana ajira za kutosha
Vijana wanaokimbilia mijini kutoka vijijini ni kutokana na
kuwa kule vijijini hawahapata muongozo wa kutambua na kisha kutumia fursa za mali zilizopo jambo ambalo kwa sasa wadau
ikiwemo serikali inatakiwa kuchukua tahadhari juu ya hilo.
Kauli hiyo imetolewa na askofu Dkt Eliud Isangya wa kanisa
la Intenational evangelism Church wakati akiongea na waandshi wa habari
kuhusiana na fursa za vijana pamoja na changamoto ambazo zinawakabili vijana.
Aidha alidai kuwa inashangaza sana kuona kuwa wimbi kubwa la vijana
wanakimbilia mijini wakati huko vijijini kuna fursa za kutosha na hazitumimiki
wakati mijini fursa za ajira hazipatikani
Kutokana na hilo alisema kuwa
kinachosabbisha waje mijini ni kuwa hawajaweza kutambua fursa zilizopo huku
baadhi ya watumishi wa serikali wenye dhamana na vijana nao wakiwa wamesahu
wajibu wao kwenye jamii wa kusaidia kundi hilo.
“hawa watendaji wa serikali wakati mwingine wanasahu wajibu
wao hata wa kuweza kutangaza fursa za ajira kwa vijana na inasababisha vijana
waweze kuona kuwa wapo pekee yao
na hivyo wanaona bora waje mjini”aliongeza Dkt Isangya.
Hataivyo alidai kuwa kutokana na hilo asilimia kubwa ya
vijana wanaokuja mijini wanasababisha madhara makubwa sana kwani wengi wao
wajikuta wakiwa wanaangukia katika matukio ya kihalifu na matukio mabaya ya
uharibifu wa amani ya nchi kwa hali hiyo ni changamoto kubwa sana kwa serikali,
kwa vijana na hata wadau wa dini’aliongeza Dkt Isangya.
MWISH
No comments:
Post a Comment