NYUMBA ZAIDI YA 300 ZILIZOBOLEWA ARUSHA ZALETA DALILI YA
WAWEKEZAJI WA KIMATAIFA
Arusha
JIJI la Arusha limefanikiwa kuvunja nyumba zaidi ya 300
katika oparesheni maalumu ya kusafisha jiji huku pia likiweza kuweka
mikakati mbalimbali ya kuendelea kuboresha sehemu ambazo zimebomolewa nyumba
hizo huku pia Viongozi nao wakidai kuwa
kuanzia kubomolewa kwa nyumba hizo kumeanza kuongeza idadi ya wawekezaji wenye
nia ya kuwekza katika maeneo hayo.
Aidha nyumba hizo zilibomolewa siku chache zilizopita ambapo
pia zoezi hilo
liliweza kwenda sanjarai na ukamataji wa bidhaa ambazo zilikuwa zinauzwa nje
bila mipangilio.
Hayo yamelelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela
wakati akiongea na viongozi wa Majiji mbalimbali hapa nchini wakati akielezea
mpango wa kuboresha jiji la Arusha
Mongelea alisema kuwa hapoa wali nyumba zilizobomelewa
zilikuwa katikati ya Jiji na zilikuwa
zinalipa kodi ndogo sana
ukilinganisha na hadhi yenyewe ya Jiji la Arusha hali ambayo ilisababisha
waweze kuchukua hatua hiyo.
Hatiavyo Monngela alisema kuwa kabla ya hapo walilazimika
kuburutwa mahakani ambapo wenye nyumba hzio walidia kuwa Jiji limewaonea na
hivyo hawapaswi kuondolewa katika nyumba hizo.
“hawa walituburuza mahakamani na kudai kuwa tunawaonea sasa
sisi tulishinda katika kesi hiyo na tuliweza kubomoa nyumba hizo ambazo
walikuwa wanalipa kiasi cha kati ya elfu sita mpaka kumi kama
kodi wakati kwenye majumba mengine watu wanalipa mpaka kiasi cha Mamilioni kwa
ajili ya nyumba za biashara na nyumba za kuishi”aliongeza Mongela
Hataivyo Mkurugenzi mtendaji wa Jiji Juma Iddi alisema kuwa
kwa sasa kuna mpango wa kuweza kuendeleza maeneo hayia mbayo yalikuwa kwanza na
ujenzo holela lakini pia yalikuwa hayaingizi faida kubwa kwa Jiji
Iddi alisema kuwa toka nyumbha hizo kubomolewa Jiji la
Arusha limekuwa katika taswira tofauti sana
kwani kwa sasa hata wawezekaji nao wameanza kujitokeza tofauti na hapo awali
ambapo kulikuwa na nyumba hizo
“hapo awali tulikuwa hatufanikiwi kwa lolote hata kodi yao
kwetu ilikuwa ni ndogo sana lakini kwa sasa tumeweza kubomoa na sisi tutawekeza
kwenye majengo makubwa yenye hadhi zake na wala sio yale”aliongeza Iddi.
Pia alisema kuwa mbali na kuwekeza majengo yenye hadhi ya
Jiji na kimataifa kwenye maeneo ambayo nyumba hizo zimebomolewa lakini pia
wanampango endelevu wa kuhakikisha kuwa nyumba za Jiji la Arusha zinajengwa
kwenye hadhi ambayo inakubalika na wala sio ujenzi holela.
MWISHO
No comments:
Post a Comment