Tuesday, April 29, 2014

DAWA YA NJAA YAINISHWA

IMEELEZWA kuwa ili nchi ya Tanzania iweze kuepukana na majgana hasa ya baa
la njaa Nchi inapaswa kuzalisha kilimo kwa asilimia zaidi ya sita ambapo
chakula kinachozalishwa kitaweza kuwekwa hadi akiba tofauti na sasa ambapo
uzalishaji wa kilimo ni kwa asilimia 4 pekee.

Hataivyo uzalishaji huo wa asilimia sita pia utaweza kuongeza ufanisi wa
kilimo na kitakuwa ni cha kisasa zaidi hivyo majnga hasa ukosefu wa
chakula,umaskini nao utaweza kupungua kwa kiwango kikubwa sana .

Hayo yameelezwa na Bi Nkuvililwa Simkanga ambaye ni mkurugenzi wa sera na
mipango kutoka katika Wizara ya kilimo na ushirikia wakati akiongea kwa
niaba ya wizara hiyo mara baada ya kukabidhiwa kwa Jengo la kuhifadhia
mazao ambalo limejengwa chini ya uzamini wa  TAHA

Mkurugenzi huyo alidai kuwa kwa sasa Tanzania bado inazalisha Kilimo kwa
kiwango cha Asilimia 4 pekee hali ambayo bado inahitajika kuongezewa nguvu
zaidi kwani uwezekano wa kuendelea kuzalisha kwa wingi sana bado upo endapo
kama kutakuwa na umoja baina ya wakulima na wadai wengine wa Kilimo.

"tukizalisha kilimo chenye ubora na kiwango ambacho kinahitajika basi
tutaweza kupunguza tatizo la uhaba wa chakula na hata umaskini nao
utapungua kwani uwezo wa kufanya hivyo tunao kabisa ila changamoto bado
zinashindwa kutufikisha"aliongeza Bi Simkanga.

Mbali na hayo alisema kuwa Kilimo kinachangia uti wa mgongo wa taifa kwa
asilimia 24.7 huku wananchi nao wakiwa wanategemea kama ajira kwa asilimia
75 ambapo pia asilimia 95 ya chakula kinachotumika hapa nchini kinatokana
na kilimo

"Takwimu zinaonesha kuwa hali si mbaya sana na kilimo kinaendelea vizuri
sana ingawaje pia wakulima wana uwezo mkubwa sana wa kuzalisha chakula
kingi na hata kikaweza kupelekwa nje ya nchi hivyo jitiada za makusudi
zinahitajika kwa haraka sana"aliongeza

Wakati huo huo Mwenyekiti wa TAHA Erick Ngmario    erick alisema kuwa ili
wakulima waweze kufikia malengo yao ya kila siku wanatakiwa kuachana na
mila ambazo zimepitwa na wakati kwani wakati mwingine zinasababisha waweze
kulima kilimo cha umaskini

Erick alidai kuwa moja ya mila hizo amnazo zimepitwa na wakati ni pamoja na
mila za kulima kwa mazoea bila kulima kilimo cha kisasa hali ambayo wakati
mwingine husababisha umaskini ingawaje wanatumikia Kilimo kila mara

"kwa sasa wakulima wanatakiwa kujifunza kulima kilimo ambacho kinatija na
kamwe wasikubali kulima ili waweze kuonekana kama wamelima bali sheria,
taratibu na mbinu za kilimo zinaitajika kufuatwa"aliongeza Erick

Alimalizia pia kwa kuwataka wakulima hasa wa Eneo hilo la Midawi
wahakikishe kuwa wanatumia vyema jengo hilo kwa ajili ya kuhifadhi mazao na
kisha kuondokana na changamoto ya kuharibika kwa mazao.

MWISHO

No comments:

Post a Comment