Na Queen Lema, Arusha
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watu wasiofahamika
jana(leo)wamevamia ofisi ya Chadema Kanda ya kaskazini iliopo Jijini Arusha na kisha
kuanza kuwasha moto ambao ulisababisha hasara kubwa sana.
Akizungumza na “Majira”katibu wa kanda ambaye pia ni katibu
wa mkoa wa Arusha Chadema, Amani golugwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea
majira ya asubuhi katika ofisi za kanda zilizopo eneo la Ngarenaro mjini Arusha.
Golugwa alisema kuwa watu hao waliingia mara baada ya mlinzi
kutoka zamu ya kulinda usiku ambapo walilazimika kuvunja kioo kikubwa na kisha
kuingia ndani ili kufanya lile walilolikusudia.
Aliendelea kwa kusema kuwa baada ya kuingia ndani walipanda
kwenye dari la nyumba hiyo ambapo walianza kutafuta uwiano wa chumba ambacho
kinahifadhi nyaraka mbalimbali za Chama na kisha kuwasha moto
Alidai kuwa wakati wanawasha moto huo ghafla uliweza
kulipuka hivyo lengo halisi halikuweza kutimia kwa haraka na badala yake walishuka
na kuanza kukimbia wakati jingo letu likiwa linateketea kwa moto
Pia alisema baada ya watu hao kuona kuwa hawawezi kuchoma
chumba hicho walitengeza shoti kubwa ya umeme ambayo iliweza kusababisha vyumba
vya choo na bafu kuunguwa na hatimaye walishuka wakiwa wanakimbia huku moto
ukiendelea kutapakaa kwenye jingo la ofisi hiyo.
“kilichofanya tuweza kusema kuwa walikuwa na lengo la
kuchoma chumba hiki ambacho kinahifadhi nyaraka muhimu za chama ni baada ya
kuona kuwa wameacha maeneo yote na kisha kuingia hapa na inavyoonekana lengo
lao ni kupoteza ushahidi wa vitu mbalimbali ambavyo tunapambana navyo”aliongeza
Golugwa
Katika hatua nyingine Golugwa alisema kuwa tukio hilo la
kuchoma ofisi linaonesha kuwa wapo baadhi ya watu ambao wanatumia muda na fikra
zao nyingi kuwawinda viongozi wa Chadema na kuingilia hata kwenye maisha yao ya
kila siku
Aidha aliwataja watu ambao wanawindwa sana kwa ajili ya
kujeruliwa ni pamoja nay eye ,mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema,
pamoja na mwenyekiti wa wilaya ambaye ni Ephata Nanyaro
‘mpaka sasa tunawahisi watu watatu katika sakata hili na kwa
maana hiyo tumesharipoti polisi ili waanze mara moja upelelezi wao lakini jingo
letu tumeliwekea ulinzi mkubwa sana na kumbukumbu zote zipo ingawaje mpaka sasa
bado hatujaweza kujua kwanza ni hasara ya shilingi ngapi tumeipata’aliongeza
Golugwa
No comments:
Post a Comment