WATENDAJI 17 KUTOKA KATIKA KATA 17 MERU HAWANA SIFA ZA KUWA NA CHEO HICHO
IMEELEZWA kuwa watendaji wa kata 17 kutoka katika Wilaya ya Meru mkoa
wa Arusha hawana sifa za kuwa watendaji kutokana na kuwa na elimu
chini ya kiwango hivyo wanatakiwa kuacha kukaidi amri ya Serikali
iliyowataka waende shule kwa ajili ya kujiendeleza
Aidha Serikali ilishatoa waraka toka July mosi mwaka 2003 kuwa
watendaji wanatakiwa kwenda shule lakini mpaka sasa watendaji hao
hawajaweza kwenda shule kutokana na sababu mbalimbali
Hayo yameelezwa na Afisa utumishi wa Wilaya hiyo Anord bureta wakati
akielezea kazi mbalimbali za watendaji hao kwenye baraza la madiwani
wa Halmashauri hiyo kwa malengo ya kuelezea changamoto mbalimbali
ambazo zinawakabili watendaji hao mapema jana
Bureta alisema kuwa July Mosi 2013 Serikali iilitoa tamko ambalo
liliwataka watumishi hao kuweza kwenda mashuleni lakini mpaka sasa
tunaweza kusema kuwa agizo hilo halijaweza kutimizwa jambo ambalo ni
madhara makubwa kwa ajili ya utendaji kazi lakini pia hata kwa ajili
ya maslahi ya umma
Pia alisema kuwa ili kuweza kukabiliana na hali hiyo kwa sasa wameweka
utaratibu wa watendaji hao kuweza kwenda kusoma ili kuweza kukidhi
matakwa ya sheria hiyo ambayo inawataka kuwa na elimu lakini kuweza
kwenda sanjari na mpango wa serikali wa sasa yaani Big Result
Akiongelea suala hilo kwa niaba ya madiwani wa halmashauri hiyo Makamu
Mwenyekiti Frida Kaaya alisema kuwa ni lazima watendaji hao waweze
kwenda shule lakini pia hata Halmashauri ihakikishe kuwa inasimamia na
kutatua changamoto zao ambazo zinajali maslahi
‘hapa ni lazima tujiulize kuwa hawa watendaji walikosa fedha au fursa
za kwenda kusoma au walikaidi agizo hilo lakini pia kuanzia sasa
maslahi ya watendaji yawekwe hadharani na pia waweze kupewa kwa
wakati ili nao pia waweze kupata moyo wa kufanya kazi”aliongeza Frida
Pia Bi Frida alidai kuwa kama Halmashauri lakini pia Serikali
itashindwa kuwajali watendaji ni wazi kuwa lawama zitakuwa nyingi sana
kwani wao ndio wapo na wananchi kila siku ingawaje kwa sasa zipo
changamoto lukuki ambazo zinasababishwa na watendaji hao.
MWISHO
No comments:
Post a Comment