NA BETY ALEX, ARUSHA
HUDUMA ya Maisha ya Yesu iliopo maeneo ya Kisongo jijini
Arusha imesema kuwa kwa kutambua mchango wa wahudumu lakini pia wazee wa kanisa
hilo wanatarajia kuwagawia mashamba ya kulima
ili waweze kujiendeleza kwenye maisha yao
ya kila siku na kuachana na tabia ya kuwa tegemezi
Aidha mpango huo unakuja mara baada ya kanisa hilo kuanza kutoa na
kusisitiza masomo ya upendo ambayo yanalenga kumuinua zaidi Mungu kuliko
mwanadamu
Akitangaza msimamo huo wa kuwasaidia wahudumu hao mchungaji
kiongozi wa huduma hiyo Eliakimu molel”Channel”alisema kuwa mpango huo
utasaidia sana kuongeza ufanisi wa kazi za kila siku lakini hata za kanisa
Alisema kuwa kwa kufanya hivyo wahudumu hao hasa wale ambao
hawana kazi wataweza kuepukana na dhambi mbalimbali ambazo zinasababishwa na
ukosefu wa kazi za kufanya
“ukiwa kama muhudumu hapa
kanisani kwangu nilazima nihakikishe kuwa mnatoka siwezi kutoboa mimi mwenyewe
halafu ninyi mkabaki mkiwa hamna lolote nasema nitagawa mashamba ya kulima na
kila atakayweze akulima katika mashamba hayo ni lazima atoke”aliongeza Channel
Pia alisema kwa kanisa lolote lile ili liweze kusimama vema
wahudumu lakini pia hatawazee wa kanisa wanapaswa kuwa makini kuanzia kiroho
hadi kimwili hivyo ni wajibu wa viongozi wa makanisa kuhakikisha kuwa
wanawaangalia makundi hayo
Alidai kuwa kama wakiwa
dhaifu kwenye nyanja yoyote ile ni lazima kuwepo na kasoro kwenye huduma hiyo
na badala yake badala ya kusonga mbele kwenye wokovu basi hata waumini watakuwa
wanarudi nyuma kwenye wokovu
“wahudmu, wazee wa kansiani watu muhimu sana kwenye
maendeleo ya kanisa la leo tusiwaache wakawa legelege bali tuwainue juu hata
hali zao za maisha ziweze kubadilika ni faraja sana kama mhudumu wa kanisa
akapanda daraja kwenye kiwango cha juu alafu pia akawa na imani basi hata mimi
mchungaji nitafanya kazi yangu bila shaka ila kama akiwa legelege pepo likija
linaanza nay eye kwanza”aliongeza Channel
Wakati huo huo alisema kuwa pia kanisa hilo limejiwekea hata
utaratibu wa kuweza kuwasaidia wale wasiojweza kwa kuwa msaada wa vyakula ili
wasiwe wakrisro wenye imani lakini pia wawe na uwezo kuamini kuwa hata kama
hawana kitu bado mchungaji wao anawapenda na anaweza kufunga na kuomba juu yao
ili hali za maisha ziweze kubadilika.
MWISHO
No comments:
Post a Comment