VIJANA WA MERU WATAKAOKIUKA MAADILI NA KUIGA TAMADUNI ZA NJE
YA NCHI KUCHAPWA VIBOKO 60 HADHARANI
Na Queen Lema, Meru
UONGOZI wa Kimila ujulikanao kama
Rika la Kilovio kutoka katika kabila la Kimeru
umepitisha sheria
kali ya kudhibiti maadili kwa vijana wa kike na wa kiume hasa wale ambao
wanaiga tamaduni za mataifa ya nje ya
nchi ambapo kwa kijana atakayebainika kuiga au kukiuka maadili ya Kitanzania
basi atalazimika kuchapwa viboko 60 hadharani
Hatua hiyo inakuja mara baada ya baadhi ya vijana katika
eneo hilo la
Meru kuanza tabia ya kuiga tamaduni lakini hata madili ya mataifa ya nje hali
ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa maadili kuendelea kuporomoka.
Hayo yameelezwa na Bw Akundaely Mbisse ambaye ni kiongozi wa
marika ya vijana katika kabila hilo wajulikao kama “Kilovio”wakati wakimsimika
na kumuingiza rasmi kiongozi wa vijana katika eneo hilo la Mareu Bw Herieli
Mafie mapema jana.
Mbisse alisema kuwa utaratibu huo wa kuwapa vijana adhabu ya
viboko 60 utaweza kurudisha maana halisi ya kijana wa kabila hilo ambapo kwa
sasa jamii ya Mkoa wa Arusha bado inaonekana kuendelea kulelemewa na tatizo la
vijana wengi kuiga tamaduni za nje ya nchi huku hali hiyo nayo ikichangia sana
hata ubaribifu wa amani ya Kaya,hadi mkoa.
Alifafanua kuwa adhabu hiyo ya viboko 60 hadharani itaenda
sanjari na vijana wote wenye tabia mbalimbali ambazo hazina tija kwenye jamii
hiyo ya Meru kama vile Uzinzi, ulevi wa
kupindukia saa za kazi, wizi, Mavazi yanaonesha maumbile,ukosefu wa adabu
pamoja na makosa mengine ambayo chanzo chake ni kuiga maadili yasiyokuwa na
tija kwennye jamii.
“tumejipanga kuhakikisha kuwa wilaya hii ya Meru inakuwa na
utofauti wa hali ya juu sana kwani tunao uwezo wa kuwaweka vijana wetu wawe
katika maadili mazuri, na masuala kama vile uvaaji wa nguo za ajabu utaisha na
kwa hali hiyo jamii itaweza kupungza hata ujinga unaofanywa na baadhi ya vijana
wachache huku wakisingizia umaskini’aliongeza Mbisse.
Hataivyo Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye ni Mjumbe wa
kamati ya siasa ya mkoa wa Arusha John Palangyo alisema kuwa kuna umuhimu
mkubwa sana wa maadili ya kila kabila kurudiwa
ili kuweza kuwajengea vijana uwezo wa kufanikiwa zaidi kwenye maisha yao ya kila siku.
Palangyo alisema kuwa suala hilo
la ulindaji wa maadili lina manufaa sana
sio kwa vijana kwani hata kwa taifa kwani kwa sasa wapo baadhi ya vijana ambao
wanaharib na kuvunja amani ya Nchi kwa kuwa hawana maadili ambayo yanaanzia
ngazi za marika hadi taifa.
‘hili jambo la kuweza kuwaweka vijana katika mazingira
mazuri ya kimaadili linawezekana kabisa na sisi watanzania tunatakiwa
kuondokana na dhana potofu kuwa eti vijana wa sasa hawana maadili wa
kuwafundisha maadili ni sisi wazee wa ukoo,rika, na hata wana siasa hivyo basi
kila mtu anatakiwa kuzingatia hili lakini pia kuona kuwa kijana wa mwenzake ni
wa kwake na hata kama ataharibikiwa basi atachangia uharibifu bila kujali
anaharibu kwa nani”aliongeza Palangyo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment