Asasi ya Informal Sector team(INSERT)imefanikiwa kutoa
msaada wa Mablanketi yenye thamani ya zaidi ya milioni moja na nusu kwa Jukwaa
la wazee wa mkoa wa Arusha (JUWA)huku lengo halisi likiwa ni kuhakikisha kuwa
wazee wote wanaendelea kusihi maisha ya upendo na amani
Akiongea na wazee hao mara baada ya kuwapa msaada mratibu wa
asasi hiyo ya INSERT,Japhet Saruni alisema kuwa msaada huo unalenga kuhakikisha
kuwa afya za wazee zinaendelea kuboreka zaidi
Aidha Saruni alisema kuwa kwa sasa wazee wengi sana wamekuwa wakisahulika kwenye maslahi yao
hali ambayo inachangia sana
kuzorotesha hata afya zao ingawaje sera za wazee bado zipo
Alifafanua kwa kusema kuwa hali hiyo imechangia kwa kiwango
kikubwa sana
wazee wengi kupoteza maisha kabla ya siku zao hivyo basi ndio maana Asasi hiyo
ya INSERT ikaweza kuona kuwa kuna umuhimu wa kuwasaidia wazee
Pia alisema kuwa kuna umuhimu wa jamii kuhakikisha kuwa
wanatatua kero za jamii kila mara kwani kwa sasa jamii imeacha kabisa
kuwasaidia wazee huku wazee nao wakikabiliwa na changamoto kubwa sana
Hataivyo alifafanua kuwa kama
jamii itaweza kuwakumbuka wazee kila mara basi kasi ya ongezeko la vifo visivyo
vya lazima hasa vya wazee vitaweza kupungua kwa kiwango kwani takwimu
zinaonesha kuwa wazee wengi wanakufa kutokana na kuwa hawana msaada wa
kuwasaidia.
Awali wazee waliopewa msaada walisema kuwa pamoja na kuwa
wamepewa msaada huo bado kuna umuhimu wa sera za wazee kuweza kutekelezwa hasa
kwenye sekta muhimu kwani sera hizo zipo lakini hazitekelezwi na baadhi ya
watendaji tena wwa Serikali.
MWISHO
No comments:
Post a Comment