Sunday, May 20, 2012

Mbunge Nassari arudi mbele za Mungu kwa ajili ya Shukurani

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida jana Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari aliwakutanisha wapiga kura wake zaidi ya 4000 huku miongoni mwao wakiwa ni makada wa chama cha Mapinduzi pamoja huku Mgombea mwenza wa chama cha Mapinduzi Bw Sioi Sumari akishindwa kufika kwa kuwa amekosa usafiri wa haraka sana.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mbunge huyo kutoa sadaka mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo  ibada ambayo ilifanyika katika kanisa la FPCT Kilinga wilayani Meru Mkoani Arusha

Akiongea na Maelfu ya wananchi wa jimbo hilo katika kanisa hilo Bw Nassari alisema kuwa ameamua kutoa sadaka maalumu ya kushukuru mungu mara baada ya kumaliza vema uchaguzi huku wapiga kura wake wote wakiwa salama tofauti na pale ambapo wengi waliadhimia

Pia alisema kuwa kwa sasa Viongozi wa Vyama vingine ambao nao walishiriki katika uchaguzi hawapswi kukataana na badala yake wantakiwa kuwa wamoja kama walivyoshirriki makada wengine wa chama cha Mapinduzi ndani ya ibada hiyo ya shukurani

“leo nimetoa shukurani yangu ndani ya kanisa hili la Kilinga lakini ninafurai kuwa makada wa CCM tupo nao hapa lakini mbali na hayo mgombea wangu mwenza wakati wa kampeni naye alikuwa anatamani sana kuja ila kwa bahati mbaya alichelewa ndege , ingawaje kwa sasa tuna madiwani wengi sana wa CCM,  Mbunge wa Jimbo la Moibara na wengine wengi nah ii ndio inayotakiwa”alisema Bw Nassari

Awali aliongeza kuwa yeye hana shida yoyote na kiongozi hata kama ni wa chama chake ila ana shida na viongozi ambao wana mikakati na malengo mbalimbali ya kuteketeza  maslahi ya wananchi hasa wa jimbo la Arumeru Mashariki na kamwe kiongozi kama huyo hataweza kumvumilia  kwa kuwa hana msimamo na Taifa

Naye Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye ni Mbunge wa  Mwibara mkoani Mara, bw Kingi Lugora alisema kuwa ili kukabiliana na hali zote ndani ya nchi wapo baadhi ya viongozi ambao wanaharibu mpango wa Mungu hasa kwa nyakati za uchaguzi kwa kuwa wanatumia mabavu ya Rushwa na mara wanapopata uongozi bado wanaendeleza hali ya Rushwa  huku wananchi wa chini nao wakiwa wanazidi kuumia na hali ngumu ya maisha

“wapo wanasiasa ambao wanawapiga wananchi upofu wa Rushwa na ndio maaana uchumi wa leo umeyumba huku waumini wa leo wakiwa wanasuasua na kwa hili naomba makanisa ya sasa yaingie kwenye  maombi dhidi ya hawa watu ambao wanaomba rushwa hasa katika bunge, na pia napenda kuwatia Moyo hata wabunge ambao  wanajidhatiti na kisha kusema hadharani masuala ya Rushwa wasiogope hata kama ni makada kama mimi nilivyo  kwa kuwa wapo baadhi ya viongozi  ambao wanatamani kusema Rushwa lakini wanapata Kigugumizi kwa kuhofia maslahi ya vyama vyao”aliongeza Bw Lugora.

Pia alisema kuwa yeye kama yeye kamwwe hatasita kusema ukweli kwa kada yoyote  wa CCM  ambaye anachangia sana  uchumi wa Nchi kuyumba na badala yake atamuomba Mungu zaidi  ili aweze  kuwasema na kuwaweka hadharani kwa kuwa mpaka sasa Mungu anajibu Maombi juu ya mafisadi  ambao ndio chanzo kikubwa sana  cha umaskini ndani ya Nchi ya Tanzania


Katika hatua nyingine  Askofu Langaeli  Kahaya  naye alisema kuwa wananchi wanapswa kuhakikisha kuwa kamwe hawamchagui kiongozi yoyote kwa ajili ya maslahi ya Rushwa kwa kuwa wote wanaotoa rushwa  ndio wanaosababisha hata umaskini na umwagaji damu ndani ya  nchi

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni mwiko kwa wananchi wma Jimbo la Arumeru  Mashariki kujihusisha na Rushwa kwa vipindi vyote vya uchaguzi kwa kuwa mpaka sasa Rushwa imeshaacha madhara makubwa sana ndani ya jimbo hilo na pia Rushwa ni dhambi kubwa sana.

“ukiangalia sana mtu anayetoa rushwa ni mtu mwenye elimu yake sasa kwa hili wananchi wanapswa kujua kuwa anayetoa na anayepokea rushwa anafanya dhambi na hiyo dhambi ndiyo inayotapakaa kwa jamii na vizazi vingine ambavyo navyo vinaibuka na  dhambi hiyohiyo”alisema Bw Kaaya

Mbali na hayo alisema kuwa pia taifa la Tanzania linatakiwa kuhakikisha kuwa kila mara linakuwa na maombi makubwa sana hasa ya baadhi ya watu ambao wanatekeleza  ahadi za Rushwa na Ufisadi hali ambayo nayo inachangia ka kiwango kikubwa sana umaskini wa watanzania wa Leo

Mwisho


chanzo cha habari na Queen Lema, arusha

Monday, May 14, 2012

MADUKA 10 YAMEUNGUA KATIKA MJI WA NGARAMTONI



Maduka 10 yenye thamani ya zaidi ya million 100 yameteketea kwa moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni wilayaya Arusha vijijini ambapo chanzo halisi ni hitilafu ya Umeme

Akiongea na Majira katika eneo la Ngaramtoni  mmiliki wa maduka hayo Bw  Benjamini Mbayi alisema kuwa moto huo ulianza majaiara ya saa saba za mchana ambapo ulianza katika duka moja

Alisema kuwa wakati moto huo unaanza alilazimika kuingia kwenye chumba hicho na kuzima umeme katika kiunganisha cha umeme (SOCKET) lakini bado haikusaidia kabisa na moto huo uliendelea kutapakaa katikia vyumba bvingine vya biashara

“baada ya kuona moshi ukiwa unatapakaa kwenye paa ambapo  kwa kweli nilishindwa kuokoa kitu chochote ila nilifanya jitiada za kuhakikisha kuwa tunaomba msaada hasa kwa kikosi cha zima moto jambo ambalo lilifanikiwa ndani ya dakika 30”alisema Bw Mbayi

Pia aliongeza kuwa mara baada ya hapo kikosi hicho kilifanikiwa kuzima moto lakini vitu venye thamani ya Milioni 100 vilikuwa vimeshateketea kwa Moto lakini kutokana na zoezi hilo la uokoaji  hapakuwa na madhara yoyote yale ya kuunguwa kwa binadamu


Diwani wa kata ya Olmotony Bw David Kinisi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa kutokea kwa matukio hayo ya mara kwa mara ya moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni kunatokana na ubovu wa mundombinu hasa ya maeneo ya biashara hali ambayo kila mara inasababisha matatizo makubwa sana

Bw Kinisi alifafanua kuwa tukio la Moto katika mji huo wa Ngaramtoni ni la Pili ambapo mwezi uliopita  maduka tisa nayo yaliteketea kwa moto huku maduka hayo yakiwa na gharama ya milioni 200 huku moja ya maduka yakiwa ni mali yake


”kama mnavyoona hapa ubovu wa miundo mbinu unachangia kwa kiwango kikubwa sana na kama halmashauri haoitaweza kuliangalia suala hili kwa undani zaidi basi itakuwa ni hatari sana kwani kuuungua kwa maduka haya  ni dalili kubwa snaa ya umaskini hasa Ngaramtoni”alisema Bw Kinisi

Alifafanua kuwa hali hiyo inatakiwa kuboreshwa sana hasa katika eneo la Umeme kwa kuwa ndio  chanzo kikubwa Sana cha kutokea kwa majanga ya moto kwa kuwa hata maeneo yaliongua ndio chanzo kikubwa sana  cha hasara  na umaskini katika mji mdogo wa Ngaramtoni.

Awali aliwataka wananchi hasa wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanafanya biashara kwa kuzingatia utaalamu wa mafundi wa umeme na wala sio kwa kuwatumia mafundi wa uchochoroni ambao ndio chanzo kikubwa  cha majanga ya Moto

Naye kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa bado wanaendelea na  uchunguzi wa tukio hilo na kujua thamani halisi ya maduka yaliyoangua katika janga hilo
MWISHO


CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

MNAOTAKA ARDHI HAKIKISHENI KUWA INAKUWA NI KWA AJILI YA WAJANE NA YATIMA MERU

MBUNGE wa jimbo la arumeru mashariki Joshua Nasari amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwa na maono mbali mbali juu ya  matumizi bora  ya ardhi iliyopo wanayoitaka kutoka kwa wawekezaji  kwa kuhakikisha kuwa ardhi hiyo inajengwa vyuo vya ufundi na mambo mengineyo ambayo yatawasaidia wao  na vizazi vyao vijavyo

Nasari aliyasema hayo alipokuwa akiongea na wakazi wa jimbo hilo  katika hafla ya kumuaga muhasisis wa kanisa la African Mission Evangelism Askofu Nickson Issangya iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto yatima cha African Orphanag e kilichopo Sakila wilayani arumeru

Alisema kuwa pamoja na kuwa wana arumeru wanahitaji ardhi yao  kutoka kwa wawekezaji ,lakini  wanapaswa  wawe   na maono juu ya matumizi yake kwa kuwa wako ambao wakipewa ardhi hiyo  wanakimbilia kuuza ili wapate  fedha.

“Arumeru tuna matatizo mengi hatuna vyuo vya ufundi ,mji mdogo  ,wa usa river hauna hata viwanja vya kuzikia ndugu waliofariiki,hakuna hata viwanja vya michezo ila endapo mtakuwa na maono mazuri juu ya ardhi hiyo ni wazi kuwa  mtaifanyia mambo makubwa sana ya maendeleo”alisema Nasari

Aidha akielezea mikakati aliyonayo  alisema kuwa ni pamoja na kuhakikisha anawasaidia watoto yatima na wajane kwa kuwa makundi haya mawili yametekelezwa bila kukumbukwa  hivyo kuwafanya waonekane wametengwa na jamii.

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwasihi vijana kuachana na makundi ya kupotoshana na badala yake  wahakikishe wana kuwa na nidhamu ,maono . na uwajibikaji mzuri wa kazi kwa kuwa endapo watazingatia mambo hayo yatawafanya kufanikiwa katika maisha yao.

Nae mhasisisi huyo Nickson Issanya aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuweka itikadi za kisiasa pembeni na badala yake wawe na umoja kwa kuhakikisha kuwa wanampa mbunge wao ushirikiano ili aweze kutimiza malengo aliyojiwekea.

Issangya alisema kuwa endapo wataendeleza itikadi za kisiasa katika jimbo hilo ni wazi kuwa makundi hayatavunjika jambo ambalo litasababisha kurudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo.
mwisho



CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA


0758907891

Saturday, May 12, 2012

Meru yajipanga kuhakikisha kuwa inafanyamabadiliko ya hali ya juu sana hasa katika kuibua vipaji






mkurugenzi wa Meru Trisias Kagenzi akifanya mahojiano na mwandishi  wa  Upako wa ufalme wa Mungu hayupo pichani kuhusiana na mikakati mbalimbali ya halmashauri hiyo hivi karibuni

WAPO WATU AMBAO HAWATAONA UFALME WA MUNGU KISA SIMU


Wakristo wametakiwa kuwa makini sana na matumizi ya simu za mikononi kwa kuwa asilimia kubwa ya wakristo wanadanganya watu bila kujua na kutambua kuwa wana muasi mungu wao

Asilimia kubwa ya watu wanadanganya na kisha wanakuja makanisani wakijua kuwa wapo sawa lakini hakuna dhambi ndogo hata kidogo

Hayo yameelezwa na mchungaji Joseph moto wa kanisa la antiokia reviaval church liliopo sombetini jijini hapa wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo hivi karibuni

Mchungaji Moto alisema kuwa kila mahala wakristo wanajiwekea utaratibu wa kuongea uongo wakati wa kiwa wanaongea na simu na badala yake wanashindwa kujua kuwa kwa mungu hakuna dhambi ambayo ni ndogo

Alieleza watu hao wanaongea uongo kwa njia ya simu mara nyingi sana huwa wanadhamiria huku wakiwa makanisani mwao wanaonesha kuwa wanapinga dhambi ya uongo

‘napenda kuwasihi wakristo kuhakikisha kuwa duniani hakuna dhambi ndogo na badala yake wajue kuwe mungu hapendi na wakicheza wapo baadhi ambao hawataweza kuona ufalme wa mungu ktokana na simu”alisema mchungaji huyo

Katika hatua nyingine aliwatahadharisha wakristo kuhakikisha kuwa wanajua matumizi ya simu kwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na ukweli hasa kwa wenza wao

Aliongeza kuwa hakuna jambo jema kwenye simu kama kuongea kwa mwenza wako au ndugu yako wa karibu ukweli kwa kuwa hali hiyo itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kujenga jamii

‘leo  unakuta watoto wetu wan waangalia masuala mbalimbali na wananakili sana wazazi wao wanchokifanya sasa kwa hali hii kama wazazi wataangalia zaidi kuongea uongo wanawafundisha nini watoto wao"aliongeza mchungaji huyo
 MWISHO

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

ARUSHA 

0758907891

WENYE HOFU YA MAISHA NA WASIOJIAMINI WATAKIWA KUWA CHINI YA UTAWALA WA MUNGU NA WALA SIO WA SHETANI WAONYWA


,ARUSHA

ASILIMIA kubwa ya watu ambao wanakuwa na hofu ya Maisha na kushindwa kujiamini ni wale watu ambao wapo chini ya utawala wa Shetani huku kwa wale ambao wapo chini ya utawala  wa Mungu wanakuwa majasiri hata wanapopita kwenye mapito ya nguvu za giza.


Hayo yamesemwa Wilayani Meru katika kanisa la E.A.G.T Nkure na Mchungaji Raphael Nanyaro wakati akiongea na Waumini wa kanisa hilo mapema wiki hii

Mchungaji huyo alisema kwa mtu ambaye yupo chni ya utawala wa nguvu za giza mara zote anakuwa na hali ya uoga mkubwa sana wakati kwa ailiye chini ya utawala wa Mungu muda wote anakuwa na imani hata kama anapita katika mapito makubwa sana

Alifafanua kuwa utawala wa nguvu za giza una madhara makubwa sana na kwa mtu yoyote ambaye anaongozwa na utawala huoi anapaswa kujua kuwa mwisho wake uo karibu sana wakati kwa anayekuwa chini ya utawala wa Mungu kila kinachomtokea ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu


Aliongeza kuwa ili utawala huo wa Shetani uweze kukaa vema ni pale unapokuta mkristo anakimbia Neno la Mungu katika Mahubiri yake, Nyimbo za Sifa na hata Nyimbo za Kuabudu kwa kuwa hata naye Shetani analijua vema Neno la Mungu

“ukishakuwa wa kukimbia Neno la mungu basi wewe  ni wa utawala wa shetani na mtu yeyote ambaye  anataka mungu afanye mabadiliko hata ya kiutawala ni lazima matendo na imani na Neno viweze kuambatana kwa pamoja”alisema Mch Raphael


Pia alibainisha kuwa mtu anapokuwa chiuni ya utawala wa milele ambao ni utawala wa mungu basi mtu huyo anaweza kumpinga shetani na kazi zake kwa uraisi sana kwa kuwa silaha zote zimeanishwa vema katika maaandiko matakatifu

Hataivyo alitaja nyenzo mbalimbali za kutumia hasa pale ambapo mtu anapotaka kupigana na utawala wa nguvu za giza ambapo nyenzo hizo ni pamoja na Maombi ya dhamira ya Nafsi, kulijua vema neon la bwana,na pia sifa na kuabudu ambapo ndipo mungu anapotaka

Mchungaji Raphael alisema kuwa hata hizi ni Nyakati za Mwisho kwa hali hiyo ni vema kwa kila mtu kuhakikisha kuwa anatumia vema Nyenzo hizo kila baada ya Dakika ili kuwa na uhakika wa Unyakuo hasa pale ambapo muda utakapofika.


MWISHO


WENYE HOFU YA MAISHA NA WASIOJIAMINI WATAKIWA KUWA CHINI YA UTAWALA WA MUNGU NA WALA SIO WA SHETANI
WAONYWA.

NA BETY ALEX,ARUSHA

ASILIMIA kubwa ya watu ambao wanakuwa na hofu ya Maisha na kushindwa kujiamini ni wale watu ambao wapo chini ya utawala wa Shetani huku kwa wale ambao wapo chini ya utawala  wa Mungu wanakuwa majasiri hata wanapopita kwenye mapito ya nguvu za giza.


Hayo yamesemwa Wilayani Meru katika kanisa la E.A.G.T Nkure na Mchungaji Raphael Nanyaro wakati akiongea na Waumini wa kanisa hilo mapema wiki hii

Mchungaji huyo alisema kwa mtu ambaye yupo chni ya utawala wa nguvu za giza mara zote anakuwa na hali ya uoga mkubwa sana wakati kwa ailiye chini ya utawala wa Mungu muda wote anakuwa na imani hata kama anapita katika mapito makubwa sana

Alifafanua kuwa utawala wa nguvu za giza una madhara makubwa sana na kwa mtu yoyote ambaye anaongozwa na utawala huoi anapaswa kujua kuwa mwisho wake uo karibu sana wakati kwa anayekuwa chini ya utawala wa Mungu kila kinachomtokea ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu


Aliongeza kuwa ili utawala huo wa Shetani uweze kukaa vema ni pale unapokuta mkristo anakimbia Neno la Mungu katika Mahubiri yake, Nyimbo za Sifa na hata Nyimbo za Kuabudu kwa kuwa hata naye Shetani analijua vema Neno la Mungu

“ukishakuwa wa kukimbia Neno la mungu basi wewe  ni wa utawala wa shetani na mtu yeyote ambaye  anataka mungu afanye mabadiliko hata ya kiutawala ni lazima matendo na imani na Neno viweze kuambatana kwa pamoja”alisema Mch Raphael


Pia alibainisha kuwa mtu anapokuwa chiuni ya utawala wa milele ambao ni utawala wa mungu basi mtu huyo anaweza kumpinga shetani na kazi zake kwa uraisi sana kwa kuwa silaha zote zimeanishwa vema katika maaandiko matakatifu

Hataivyo alitaja nyenzo mbalimbali za kutumia hasa pale ambapo mtu anapotaka kupigana na utawala wa nguvu za giza ambapo nyenzo hizo ni pamoja na Maombi ya dhamira ya Nafsi, kulijua vema neon la bwana,na pia sifa na kuabudu ambapo ndipo mungu anapotaka

Mchungaji Raphael alisema kuwa hata hizi ni Nyakati za Mwisho kwa hali hiyo ni vema kwa kila mtu kuhakikisha kuwa anatumia vema Nyenzo hizo kila baada ya Dakika ili kuwa na uhakika wa Unyakuo hasa pale ambapo muda utakapofika.


MWISHO
CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

MAOMBI YASABABISHA KAKA MTU KUVUNJA PAA LA NYUMBA

MAOMBI YASABABISHA KAKA MTU KUVUNJA PAA LA NYUMBA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mke mmoja wa  muinjilisti wa makanisa ya Anglican Bi Elizabeth  Bakari amejikuta katika wakati mgumu sana mara baada ya kufanya maombi ya kuvunja malango ya kuzimu ambapo baada ya muda mfupi  kaka wa dada huyo alipoamua kuvunja  paa la nyumba yake kwa madai kuwa hamtambui

Akiongea na Nyakati mapema  wiki hii Bi Elizabeth alisema kuwa kilichofanya kaka yake ambaye anatambulika kwa majina ya Shabani Bakari ni malango ambayo yeye alikuwa akiyapinga wakati wa kuomba kwake

Alisema kuwa jumamosi iliyopita majira ya usiku alijikuta akiwa anapambana na maroho mbalimbali ambapo hali hiyo ilifanya kaka yake mzazi kutafuta ulimwengu mwingine na kisha kumshambulia ambapo pia hata zoezi hilo la kumnshambulia katika ulimwengu wa roho nao ulikwama

Alifafanua kuwa baada ya mapambano hayo ya muda mrefu sana  hayakuishia hapo na badala yake siku inayofuta ambayo ni jumapili iliyopita majira ya saa nne za asubui kaka huyo alivamia nyumba ya dada yake ambayo wanaishi na kisha kutoa mapaa kwa kisingizo kuwa hamtambui

“mimi nilishangaa sana kwa hali ya juu na kuona kuwa  ni jambo la ajabu sana kwa kuwa kaka yangu tena wa kuzaliwa nae anafanya vitu kama hivi lakini ninachojua ni kuwa  maombi ya vita niliyoyaomba ndio chanzo nah ii ni changamoto hata kwa wengine ambao wanafanya maombi ya kila siku hasa kwa maadui zao”alisema Bi Elizabeth

Alisema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo ambalo liliwavutia watu wengi sana ambapo baada ya muda alilazimika kwenda kwenye ofisi ya kijiji ili kupata haki yake ya msingi kwa kuwa kila mara baada ya maombi kaka huyo anamfanyia vituko vikali sana

Alifafanua kuwa mara baada ya kufika katika ofisi ya kijiji walimtaka afike kwenye kituo cha Polisi Kaloleni ili hatua za juu ziweze kuchukuliwa hali ambayo ilimfanya amtafute kaka yake chini ya uangalizi mkubwa sana wa jeshi la polisi

‘nililazimika kumtafuta chini ya jeshi la polisi kwa RB No KAL/RB/792/2012  ambapo alifanikiwa kukamatwa majira ya Jioni na kisha kuwekwa katika kituo kidogo cha Polisi ambapo  Jumatatu alifikishwa mahakamani na kujibu mashitaka ambayo yalikuwa yanamkabili

Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo kilichomfanya ampeleke katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso ili aweze kujifunza kwa undani wake kwa kuwa Neno msamaha limetakiwa kuwasemehe sasa kwa hali hiyo amemsamehe ili anachokitaka ni aweze kujifunza na anachokitaka ni maombi zaidi kwa kuwa inavyoonekana kaka yake ana matatizo makubwa hasa ya ulimwengu wa  roho

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA 

ARUSHA

0758907891

KANISA LATAKIWA KUWAKUMBATIA ZAIDI VIJANA KATIKA MCHAKATO WA UJASIAMALI

MAKANISA mbalimbali hasa ya kanda ya kaskazini yametakiwa kuhakikisha kuwa yanasoma alama za nyakati kwa kuhakikisha yanasaidia sana vijana hasa katika mchakato wa ajira ambao unaanzia kwenye suala zima la Ujasiamali

Kwa sasa kama makanisa mengi yatahakikisha kuwa yanajiwekeza zaidi hata kwa kuhubiri na kuwapa moyo vijana walio wengi kuhusu umuhimu wa kuwa wajasiamali hata kama wameajiriwa basi watajiokoa kutoka matatizo mbalimbali zikiwemo anasa za dunia

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Mwenyekiti wa kanisa la Morovian jimbo la Kaskazini Tanzania,Mchungaji Peter Malema wakati alipokuwa akizundua kikundi cha wajasimali cha jijini hapa kijulikanacho kama SEMENS GROUP  wiki iliyopita

Mchungaji Malema alisema kuwa endapo  kama kanisa litasoma alama za nyakati na kuweza kujua hilo basi kwa kiwango kikubwa sana litakuwa limeweza kuwaokoa maelfu ya vijana ambao wengine wanateketea kwa kuwa hawana elimu hata ya ujasiamali

Aliongeza kuwa kwa muda huu ni vema kanisa likahakikisha kuwa linawaboreshea vijana bila kujali changamoto yopyote mafundisho hata ya ujasiamali ambayo yatalenga kuwaokoa na hivyo kama wataondokana na umaskini basi jamii nayo itakuwa imetua mzigo mkubwa

“kwa sasa ni vema kwa kila kijana wa kikristo kuhakikisha kuwa anakuwa mjasiamali kwa kuhakikisha kuwa anatafuta sana kwa kuwa hata maaandiko nayo yamewataka watafute na kama watafanya hivyo umaskini ndani ya nchi yetu utapungua kwa kiwango kikubwa sana”alisema mchungaji Malema

Awali mkurugenzi wa kampunin hiyo ya Semens Group  Bw Elias Semens alisema kuwa amejipanga kuhakikisha kuwa anawakomboa wakrisro hasa vijana na wanawake kwa kuwa wao ndio wenye mzigo mkubwa sana katika jamii

Alifafanua kuwa  kwa upande wa wanawake wanapopata elimu ya ujasiamali na kuwezeshwa kufanya kazi mbalimbali faida hiyo huenda kwenye jamii zao hali ambayo ni moja ya malengo ya makanisa mengi hasa kanisa la Morivian hapa nchini

Aliwataka viongozi wa makanisa mbalimbali kuhakikisha kuwa wanatumia kikiundi hicho ambacho kinahusika na usafi wa maofisini,na pia upishi kwenye halaiki kubwa ya watu ambapo hali hiyo nayo itaweza kuongeza hata chachu ya maendeleo ya kanisa na wajasiamali mbalimbali hapa nchini

MWISHO

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA

TANZANITE ONE YAIKUMBUKA WILAYA YA SIMANJIRO


TANZANITE Foundation ambayo ni kampuni tanzu ya TanzaniteOne ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara imechangia maendeleo ya jamii kwenye kijiji cha Naisinyai kwa kujenga shule mbili,zahanati,visima vya maji na kituo cha jamii.
 
Akizungumza wakati akigawa vifaa vya shule na michezo kwa wanafunzi wa shule ya msingi New Vision ya mji mdogo wa Mirerani,Mkurugenzi wa Tanzanite Foundation Hayley Henning alisema lengo lao ni kusaidia jamii na siyo kupata faida.
 
Henning aliongoza na wageni kutoka nchini Marekani wakiwemo waandishi wa habari Robert Weldan Weldo wa Gia na Steve Bennett wa Gems Tv alisema wapo kwa ajili ya kuimarisha na kudumisha imani na uadilifu wa Tanzanite.
 
Alisema walijenga baadhi ya madarasa ya shule ya msingi na sekondari Naisinyai,kliniki na visima vya maji kwa ajili ya kuboresha afya ya watoto wa eneo hilo walioathirika baada ya kutumia maji yenye floride nyingi.
 
“Tuliamua kuchimba visima hivyo baada ya watoto wengi wa Naisinyai meno yao kuwa na rangi ya hudhurungi hivyo hivi sasa maji hayo hayana tatizo hilo na wanatumia jamii pamoja na mifugo yao,” alisema Henning.

Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa American Gem Trade Association (AGTA) Doug Hucker alisema wamefurahia fursa ya kutembelea kampuni ya TanzaniteOne na kufahamu shughuli mbalimbali za madini ya Tanzanite zinazofanyika.
 
“Safari yetu baada ya maonyesho ya Arusha Internation Gem imetusaidia kuona hazina kubwa ya migodi ya Tanzanite na namna mnavyoijali jamii inayowazunguka kwa kuboresha hali ya maisha ya watoto wa Tanzania,” alisema Hucker.
 
Wageni hao walitembelea eneo hilo baada ya kutoka kwenye maonyesho ya kimataifa ya madini ya Arusha International Gem Fair yaliyofanyika wiki iliyopita na kuhusisha wafanyabiashara mbalimbali wa kimataifa.




0758907891

WANAFUNZI watatu walioitimu mafunzo ya kompyuta katika chuocha uhifadhi wa mazingira   cha University Times  training  Insititutekilichoko moivaro mkoani hapa wamepatiwa kompyuta tatu zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili ikiwa    ni njia ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe baada ya kuhitimu mafunzo yao.

Wanafunzi hao wamekabidhiwa kompyuta hizo na  mkurugenzi wa chuo hicho bw Solomon Njiamoja alipokuwa katika hafla  ya mahafali ya kwanza  ya wahitimu  wa  hoteli management na kompyuta   yaliyofanyika chuoni hapo.

Bw Njiamoja alisema kuwa chuo hicho kimeamua  kuwapa wanafunzi hao kompyuta hizo ili ziweze kuwasaidia katika kujiajiri wenyewe ambapo wataweza  kukabiliana na hali ngumu ya kimaisha kwa kuwa vijana wengi wanashindwa kutimiza malengo yao kwa ajli ya kukosa vitendea kazi.

Aidha aliongeza kuwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanahohitimu chuoni hapo wanapata mafanikio mazuri chuo hicho kinatarajia kutoa kompyuta 105 kwa mwaka ambapo kila mwanafunzi anayefanya vizuri katika somo hilo atapata kompyuta yake ya kumuwezesha  kujiajiri.

Mkurugenzi huyo akielezea malengo ya chuo hicho alisema kuwa kinatarajia kuanzisha redio pia kuanzisha mfuko maalum wa kuendeleza waalimu kwa kuwa walioko wana shahada ya kwanza hivyo haiwatoshelezi kutoa elimu .

Awali mgeni rasmi katika mahafali hayo diwani wa kata ya  sokoni one Maiko Kivuyo aliwataka wanafunzi hao kutumia kompyuta hizo vizuri   kwa kuzitunza na badala yake wasiziuze kwani wako baadhi ya vijana  wakipewa zawadi wanakimbilia kuuza ili wapate fedha.

Aliwataka vijana hao kutumia elimu hiyo waliyoipata vizuri kwa kuwa katika dunia ya sasa  hakuna kitu unachoweza kufanya bila kutumia  kompyuta.



0758907891

Thursday, April 26, 2012

WAJASIMALI 70 WA KKKT WAPATIWA MAFUNZO


Wajasiriamali wanawake zaidi ya 70 kutoka kanda ya kaskazini na kati ya dayosisi  za kanisa la kilutheri wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali ya siku nne yaliyolenga kuwajengea uwezo ufahamu, na elimu ya kujikomboa na umaskini.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo mkurugenzi wa mpango  wa kazi za wanawake na watoto kkkt makao makuu arusha Bi Rachel Ramadhani alisema kuwa licha ya changamoto zinazowakabili ikiwemo ya fedha lakini mafunzo hayo yatawatoa katika utegemezi na kuweza kujiendesha na kuandaa semina nyingine kama hizo. kwani wanawake wengi wameathiriwa na mfumo dume.

alisema bi ramadhani kuwa ukosefu wa elimu ya darasani na elimu ya mazingira kutokana na mfumo dume kumewaacha kinamama wakiwa hawana mtegemezi na kuishi kwenye lindi la umaskini na hili kanisa imeliona ndiyo maana likaanza kupigana na umaskini wa kinamama na vijana ilikuondokana na taifa tegemezi.

alisema bi Rachel kuwa dayosisi zaidi ya 7 zinashiriki  zikwemo dayosisi ya kaskazini,dayosisi ya Pare,dayosisi ya kaskazini kati,dayosisi za Mbulu,Meru,kaskazini mashariki,na kati na kuwataka wakinamama kufahamu kuwa kitu ulichonacho kiwe halali kitawafanya kuondokana na umaskini wa kujitakia hata mchicha ni biashara halali isiyohitaji fedha za kukopa kwenye asasi za kifedha unapatikana kwa njia ya kujituma na kujiamini aliongeza bi ramadhani

Kuwa wanachangamoto nyingi kubwa ni fedha lakini elimu hii itasaidia kuondokana na kuomba omba au kutafuta wafadhili wa kusaidia semina kama hizo na kuwataka angependa kuwaambia biashara si lelemama biashara ni nia na wazo lakujenga na ni kitu chochote halalikinachoweza kuuzika tufanye sasakwani tunamazingira yetu yanakila kitu cha kuweza kutusaidia.

Nae mjasiriamali aliyepata mafunzo hayo bi Elizabeth Ngoi alisema kuwa anamshukuru mama ramadhani kwani hapo mwanzo hakuwa anajua kuwa kunapato la kwanza na patozalishi linaloweza kumuendeleza mtu na kuondokana na lindi la umaskini na kuwa akifika nyumbani atakuwa balozi mzuri wa kuwafundisha wengine na kuwa atakuwa na uwezo wa kubuni biashara nyingi zaidi kutakana na mafunzo aliyopata.
MWISHO.

chanzo cha habari na Queen Lema,

0758907891

Arusha

CHONDE CHONDE ONGEZEKO LA VIJANA MANISPAA YA ARUSHA

MANISPAA YAKABILIWA NA ONGEZEKO LA VIJANA

Na queen lema, arusha

Manispaa ya mkoa wa arusha kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya
ongezeko kubwa la vijana ambapo ongezeko hilo linasababishwa na baadhi
ya vijana wa vijijini kukimbilia mijini kwa ajili ya kutafuta ajira.

Hayo yamebainishwa jana na mkurugenzi wa taasisi ya maendeleo ya
vijana (YDN) Bw Elipokea Urio wakati alipokuwa akiongea na Majira
kuhusu mabadiliko ya maitaji ya vijana kwa mkoa wa arusha hususani
ndani ya halmashauri ya manispaa ya arusha

Bw Elipokea alibainisha kuwa ongezeko hilo ambalo limeongezeka kwa
kipindi cha miaka mitano sasa linasababishwa na matatizo mbalimbali
likiwemo tatizo la hali ngumu ya maisha hasa ya vijijini


Alisema kuwa mwaka 2002 vijana katika manispaa ya arusha kulikuwa na
vijana chini ya laki moja wakati kwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la
vijana laki moja sabini elfu mia tano na hamsini na saba ambapo napo
nusu yao hawana ajira.

“tukijaribu kuangalia sana tunaweza kuona kuwa nusu ya hawa vijana
hawana ajira kutokana na matatizo na changamoto mbalimbali
ukilinganisha manispaa na jiji la arusha ni mji wa kitalii hivyo kuna
umuimu mkubwa wa serikali kuliangalia suala hili kwa undani”aliongeza
Bw Elipokea.

Katika hatua nyingine bw Elipokea alisema kuwa nusu ya vijana hao
ambao hawana ajira kwa sasa wamekosa  ajira kutokana na changamoto
mbalimbali  ambapo changamoto kubwa ni pamoja na vijana kushindwa
kutumia na kutambua fursa mbalimbali zilizomo kwenye ngazi ya
vijiji,kata,na halmashauri

Alisema kuwa kama vijana wa leo wataweza kutambua fursa mbalimbali
ambazo zimo kwenye ngazi hizo basi wataweza kunufaika hata kwa njia ya
mikopo  hali ambayo itaweza kuinua hata kiwango cha maisha.

“katika ngazi ya halmashauri unakuta kwa mfano fedha zimetengwa kwa
ajili ya vijana lakini fedha hizo vijana hawazitumii wala
hawazifuatlii kwa visingizio kuwa sio mali yao basi fedha hizo
zinaenda kwenye matumizi mengine sasa  kwa hali hiyo tatizo la uhaba wa ajira linazidi kuku asana katika jamii”aliongeza bw Elipokea.

Aliwataka vijana wa hususani katika manispaa ya arusha kuhakikisha
kuwa wanajijengea tabia ya kufuatilia fursa mbalimbali ambazo zimo
kwenye ngazi za serikali ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu ya
kujiajiri wao wenyewe ili kuepukana na tatizo la uhaba wa ajira.

MWISHO

chanzo cha habari na Queen Lema,Arusha

0758907891

Arusha

WATU MILION 45 HATARINI KUPATA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

JUMLA ya watu milioni 45 duniani hasa waishio katika jamii za kifugaji
wako katika hatari ya kupata magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutokana
na kukithiri kwa changamoto mbalimbali ikiwemo uchafu wa mazingira, na
uhaba wa maji

 Juhudi za kuahakikisha kuwa magonjwa  hayo yanathibitiwa wilaya 75
kati ya wilaya zote nchini  tayari zimeshafikiwa na utekelezaji wa
ugawaji wa madawa  kwa mwaka 2011.

Hayo yalisemwa na mkurugenzi katika huduma za kinga kitengo cha
kutibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele  Dr Peter Mbuji wakati
akifungua  mkutano wa wizara ya afya na ustawi wa jamii uliofanyika
mjini hapa.

Alisema kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele  ni pamoja na
matende,kichocho,usubi trakoma na minyoo ya tumbo ambapo haya  ni
magonjwa ambayo yalikuwepo toka awali na yako nchi nzima  lakini
tayari wizara inatoa dawa na mikakati imetumika ili kuhakikisha kuwa
yanatibiwa.

Alieleza kuwa mkakati na sera za wizara zipo za kuhakikisha kuwa
magonjwa hayo yanathibitiwa na moja ya  mikakati hiyo ni kuhakikisha
kuwa kila kijiji kinakuwa na huduma ya kutoa kinga dhidi ya kuthibiti
magonjwa  hayo.

Kwa upande wake mratibu wa kitaifa wa kuthibiti magonjwa yasiyopewa
kipaumbele kutoka wizara ya afya  Dkt. Upendo Mwingira alisema kuwa
ili  magonjwa hayo yaweze kuteketezwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa
maeneo yote ambayo yana magonjwa hayo yanafanyiwa usafi     kwa kuwa
ndio njia pekee ya kuthibiti.
Aidha alisema kuwa ni vema watu wa mazingira wakahakikisha kuwa elimu
ya usafi wa mazingira inawafikia wananchi ili kuweza kuthibiti
magonjwa hayo.

Pia amefafanua kuwa katika magonjwa hayo matano kila wilaya ina
maambukizi ya magonjwa mawili ambapo wilaya 75 zimeshapatiwa dawa
ambapo hadi ifikapo mwaka 2014 nchi nzima itanufaika na utekelezaji
huo.

Naye mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu( NIMR)dr
Mwele Malechela almesema kuwa taasisi hiyo ina mchango mkubwa kutokana
na juhudi zilizotokana nautafiti ili kutafuta majibu ya kuendesha
mipango kwa ufanisi zaidi.
Alisema kuwa mkutano huo utaangalia jinsi ya kuboresha sera na njia
mbali mbali za kutoa huduma kwa watu wenye ugonjwa wa matende .
mwisho


chanzo cha habari na Queen Lema

0758907891

Arusha
SAKATA la wachungaji wa kanisa la sabato na uongozi wa kanisa hilo umechukua sura mpya mara baada ya wachungaji watatu ambao walikuwa wanashitakiwa kwa makosa ya kudaiwa kurudufu vitabu,kusema kuwa wanatoa muda kwa kanisa hilo kuomba radhi hata kwenye vyomboi vya habari na endapo kama watashindwa kufanya hivyo basi watawapeleka mahakamani.

Akiongea na mjini upako wa habari za ufalme wa mungu  kwa niaba ya wachungaji wengine wawili Dkt Tulla Paul alisema kuwa wameamua kufikia uamuzi huo kwa kuwa Kanisa hilo limepotosha umma na pia wameshindwa kufika hata kituo cha polisi ambapo ndipo waliposhitaki

Dkt Tulla alisema kuwa kwa mara ya tatu tena mfululizo Walalkamikaji ambao ni kanisa hilo wameshindwa kufika katika kituo cha kati cha polisi mjini hapa hali ambayo inafanya hata kesi hiyo ishindwe kupelekwa mahakamani

Alifafanua kuwa kanisa hilo la Sabato ambalo lilisema kuwa lina ushahidi dhidi ya wachungaji hao kurudufu vitabu vya nabii Hellen .G. White ni uongo kwa kuwa kanisa ndilo lilorudufu vitabu

“kanisa la Sabato ndilo lilorudufu vitabu na ushaidi upo kwa maana hiyo basi ni vyema tukaenda mahakamani tukapambane huko huko ila kama hawataki waombe radhi hadharani kwa kuwa wametuweka katika wakati mgumu sana na ni sawa na kifungo cha Nje kwa kuwa mara nyingi sana tunahudhuria kituoni ili kesi iende mahakamani lakini wao hawaji “aliongeza Dkt Tulla

Katika hatua nyingine alisema kuwa tukio hilo ni sawa na uonevu mkubwa sana na hata taasisi nyingine za dini nazo zinatakiwa kujifunza kitu kwa kuwa wamepoteza muda na rasilimali fedha kwa ajili ya madai ambayo si ya msingi

Walifafanua kuwa kwa muda wa zaidi ya Miezi mitatu sasa wamefuatilia kesi hiyo ambayo ni AR/IR/1130/2012 huku shuguli zao za kueneza injili nayo ikikwama hali ambayo ni kichocheo kikubwa sana cha kukata tama

“sasa kama sisi wengine tunatoka Mwanza tunakuja kwa ajili ya kesi ambayo tulifunguliwa sisi kwa kisa kuwa tumerudufu vitabu wakati ni uongo na walalamikaji hawaji ili kesi iende mahakamani basi huu si ni uongo wa ajabu sana jamani nini nafasi ya kanisa hapa na je mtu ambaye haamini anajifunza nini kutoka kwa hawa viongozi wa kanisa ‘alisema Dkt Tulla

 

chanzo cha habari na queen Lema

0758907891

 Arusha