Maduka 10 yenye thamani ya zaidi ya million 100 yameteketea
kwa moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni wilayaya Arusha vijijini ambapo chanzo
halisi ni hitilafu ya Umeme
Akiongea na Majira katika eneo la Ngaramtoni mmiliki wa maduka hayo Bw Benjamini Mbayi alisema kuwa moto huo ulianza
majaiara ya saa saba za mchana ambapo ulianza katika duka moja
Alisema kuwa wakati moto huo unaanza alilazimika kuingia
kwenye chumba hicho na kuzima umeme katika kiunganisha cha umeme (SOCKET)
lakini bado haikusaidia kabisa na moto huo uliendelea kutapakaa katikia vyumba
bvingine vya biashara
“baada ya kuona moshi ukiwa unatapakaa kwenye paa
ambapo kwa kweli nilishindwa kuokoa kitu
chochote ila nilifanya jitiada za kuhakikisha kuwa tunaomba msaada hasa kwa
kikosi cha zima moto jambo ambalo lilifanikiwa ndani ya dakika 30”alisema Bw
Mbayi
Pia aliongeza kuwa mara baada ya hapo kikosi hicho
kilifanikiwa kuzima moto lakini vitu venye thamani ya Milioni 100 vilikuwa
vimeshateketea kwa Moto lakini kutokana na zoezi hilo la uokoaji hapakuwa na madhara yoyote yale ya kuunguwa
kwa binadamu
Diwani wa kata ya Olmotony Bw David Kinisi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa kutokea kwa matukio hayo ya mara kwa mara ya moto katika mji mdogo wa Ngaramtoni kunatokana na ubovu wa mundombinu hasa ya maeneo ya biashara hali ambayo kila mara inasababisha matatizo makubwa sana
Bw Kinisi alifafanua kuwa tukio la Moto katika mji huo wa
Ngaramtoni ni la Pili ambapo mwezi uliopita
maduka tisa nayo yaliteketea kwa moto huku maduka hayo yakiwa na gharama
ya milioni 200 huku moja ya maduka yakiwa ni mali yake
”kama mnavyoona hapa ubovu wa miundo mbinu unachangia kwa kiwango kikubwa sana na kama halmashauri haoitaweza kuliangalia suala hili kwa undani zaidi basi itakuwa ni hatari sana kwani kuuungua kwa maduka haya ni dalili kubwa snaa ya umaskini hasa Ngaramtoni”alisema Bw Kinisi
Alifafanua kuwa hali hiyo inatakiwa kuboreshwa sana hasa
katika eneo la Umeme kwa kuwa ndio
chanzo kikubwa Sana cha kutokea kwa majanga ya moto kwa kuwa hata maeneo
yaliongua ndio chanzo kikubwa sana cha
hasara na umaskini katika mji mdogo wa
Ngaramtoni.
Awali aliwataka wananchi hasa wafanyabiashara kuhakikisha kuwa
wanafanya biashara kwa kuzingatia utaalamu wa mafundi wa umeme na wala sio kwa kuwatumia
mafundi wa uchochoroni ambao ndio chanzo kikubwa cha majanga ya Moto
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kujua thamani halisi
ya maduka yaliyoangua katika janga hilo
MWISHO
CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA
0758907891
ARUSHA
No comments:
Post a Comment