MAKANISA mbalimbali hasa ya kanda ya kaskazini yametakiwa
kuhakikisha kuwa yanasoma alama za nyakati kwa kuhakikisha yanasaidia sana vijana hasa katika
mchakato wa ajira ambao unaanzia kwenye suala zima la Ujasiamali
Kwa sasa kama makanisa mengi yatahakikisha kuwa yanajiwekeza
zaidi hata kwa kuhubiri na kuwapa moyo vijana walio wengi kuhusu umuhimu wa
kuwa wajasiamali hata kama wameajiriwa basi
watajiokoa kutoka matatizo mbalimbali zikiwemo anasa za dunia
Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Mwenyekiti wa kanisa la
Morovian jimbo la Kaskazini Tanzania,Mchungaji
Peter Malema wakati alipokuwa akizundua kikundi cha wajasimali cha jijini hapa
kijulikanacho kama SEMENS GROUP wiki iliyopita
Mchungaji Malema alisema kuwa endapo kama kanisa litasoma alama za nyakati na
kuweza kujua hilo basi kwa kiwango kikubwa sana litakuwa limeweza
kuwaokoa maelfu ya vijana ambao wengine wanateketea kwa kuwa hawana elimu hata
ya ujasiamali
Aliongeza kuwa kwa muda huu ni vema kanisa likahakikisha
kuwa linawaboreshea vijana bila kujali changamoto yopyote mafundisho hata ya
ujasiamali ambayo yatalenga kuwaokoa na hivyo kama
wataondokana na umaskini basi jamii nayo itakuwa imetua mzigo mkubwa
“kwa sasa ni vema kwa kila kijana wa kikristo kuhakikisha
kuwa anakuwa mjasiamali kwa kuhakikisha kuwa anatafuta sana kwa kuwa hata
maaandiko nayo yamewataka watafute na kama watafanya hivyo umaskini ndani ya
nchi yetu utapungua kwa kiwango kikubwa sana”alisema mchungaji Malema
Awali mkurugenzi wa kampunin hiyo ya Semens Group Bw Elias Semens alisema kuwa amejipanga
kuhakikisha kuwa anawakomboa wakrisro hasa vijana na wanawake kwa kuwa wao ndio
wenye mzigo mkubwa sana
katika jamii
Alifafanua kuwa kwa
upande wa wanawake wanapopata elimu ya ujasiamali na kuwezeshwa kufanya kazi
mbalimbali faida hiyo huenda kwenye jamii zao hali ambayo ni moja ya malengo ya
makanisa mengi hasa kanisa la Morivian hapa nchini
Aliwataka viongozi wa makanisa mbalimbali kuhakikisha kuwa
wanatumia kikiundi hicho ambacho kinahusika na usafi wa maofisini,na pia upishi
kwenye halaiki kubwa ya watu ambapo hali hiyo nayo itaweza kuongeza hata chachu
ya maendeleo ya kanisa na wajasiamali mbalimbali hapa nchini
MWISHO
CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA
0758907891
ARUSHA
No comments:
Post a Comment