Wakristo
wametakiwa kuwa makini sana na matumizi ya simu za mikononi kwa kuwa asilimia
kubwa ya wakristo wanadanganya watu bila kujua na kutambua kuwa wana muasi
mungu wao
Asilimia
kubwa ya watu wanadanganya na kisha wanakuja makanisani wakijua kuwa wapo sawa
lakini hakuna dhambi ndogo hata kidogo
Hayo
yameelezwa na mchungaji Joseph moto wa kanisa la antiokia reviaval church
liliopo sombetini jijini hapa wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo hivi
karibuni
Mchungaji Moto
alisema kuwa kila mahala wakristo wanajiwekea utaratibu wa kuongea uongo wakati
wa kiwa wanaongea na simu na badala yake wanashindwa kujua kuwa kwa mungu
hakuna dhambi ambayo ni ndogo
Alieleza
watu hao wanaongea uongo kwa njia ya simu mara nyingi sana huwa wanadhamiria
huku wakiwa makanisani mwao wanaonesha kuwa wanapinga dhambi ya uongo
‘napenda
kuwasihi wakristo kuhakikisha kuwa duniani hakuna dhambi ndogo na badala yake
wajue kuwe mungu hapendi na wakicheza wapo baadhi ambao hawataweza kuona ufalme
wa mungu ktokana na simu”alisema mchungaji huyo
Katika hatua
nyingine aliwatahadharisha wakristo kuhakikisha kuwa wanajua matumizi ya simu
kwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na ukweli hasa kwa wenza wao
Aliongeza
kuwa hakuna jambo jema kwenye simu kama kuongea kwa mwenza wako au ndugu yako
wa karibu ukweli kwa kuwa hali hiyo itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata
kujenga jamii
‘leo unakuta watoto wetu wan waangalia masuala
mbalimbali na wananakili sana wazazi wao wanchokifanya sasa kwa hali hii kama
wazazi wataangalia zaidi kuongea uongo wanawafundisha nini watoto wao"aliongeza mchungaji huyo
MWISHO
CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA
ARUSHA
0758907891
No comments:
Post a Comment