TANZANITE
Foundation ambayo ni kampuni tanzu ya TanzaniteOne ya Wilaya ya Simanjiro
Mkoani Manyara imechangia maendeleo ya jamii kwenye kijiji cha Naisinyai kwa
kujenga shule mbili,zahanati,visima vya maji na kituo cha jamii.
Akizungumza
wakati akigawa vifaa vya shule na michezo kwa wanafunzi wa shule ya msingi New
Vision ya mji mdogo wa Mirerani,Mkurugenzi wa Tanzanite Foundation Hayley
Henning alisema lengo lao ni kusaidia jamii na siyo kupata faida.
Henning
aliongoza na wageni kutoka nchini Marekani wakiwemo waandishi wa habari Robert
Weldan Weldo wa Gia na Steve Bennett wa Gems Tv alisema wapo kwa ajili ya
kuimarisha na kudumisha imani na uadilifu wa Tanzanite.
Alisema
walijenga baadhi ya madarasa ya shule ya msingi na sekondari Naisinyai,kliniki
na visima vya maji kwa ajili ya kuboresha afya ya watoto wa eneo hilo
walioathirika baada ya kutumia maji yenye floride nyingi.
“Tuliamua
kuchimba visima hivyo baada ya watoto wengi wa Naisinyai meno yao kuwa na rangi
ya hudhurungi hivyo hivi sasa maji hayo hayana tatizo hilo na wanatumia jamii
pamoja na mifugo yao,” alisema Henning.
Naye,Mkurugenzi
Mtendaji wa American Gem Trade Association (AGTA) Doug Hucker alisema
wamefurahia fursa ya kutembelea kampuni ya TanzaniteOne na kufahamu shughuli
mbalimbali za madini ya Tanzanite zinazofanyika.
“Safari
yetu baada ya maonyesho ya Arusha Internation Gem imetusaidia kuona hazina
kubwa ya migodi ya Tanzanite na namna mnavyoijali jamii inayowazunguka kwa kuboresha
hali ya maisha ya watoto wa Tanzania,” alisema Hucker.
Wageni
hao walitembelea eneo hilo baada ya kutoka kwenye maonyesho ya kimataifa ya
madini ya Arusha International Gem Fair yaliyofanyika wiki iliyopita na
kuhusisha wafanyabiashara mbalimbali wa kimataifa.
0758907891
No comments:
Post a Comment