KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida jana Mbunge wa jimbo la
Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari aliwakutanisha wapiga kura wake zaidi ya
4000 huku miongoni mwao wakiwa ni makada wa chama cha Mapinduzi pamoja huku
Mgombea mwenza wa chama cha Mapinduzi Bw Sioi Sumari akishindwa kufika kwa kuwa
amekosa usafiri wa haraka sana.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya mbunge huyo kutoa sadaka
mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo
ibada ambayo ilifanyika katika kanisa la FPCT Kilinga wilayani Meru
Mkoani Arusha
Akiongea na Maelfu ya wananchi wa jimbo hilo
katika kanisa hilo
Bw Nassari alisema kuwa ameamua kutoa sadaka maalumu ya kushukuru mungu mara
baada ya kumaliza vema uchaguzi huku wapiga kura wake wote wakiwa salama
tofauti na pale ambapo wengi waliadhimia
Pia alisema kuwa kwa sasa Viongozi wa Vyama vingine ambao
nao walishiriki katika uchaguzi hawapswi kukataana na badala yake wantakiwa
kuwa wamoja kama walivyoshirriki makada
wengine wa chama cha Mapinduzi ndani ya ibada hiyo ya shukurani
“leo nimetoa shukurani yangu ndani ya kanisa hili la Kilinga
lakini ninafurai kuwa makada wa CCM tupo nao hapa lakini mbali na hayo mgombea
wangu mwenza wakati wa kampeni naye alikuwa anatamani sana kuja ila kwa bahati
mbaya alichelewa ndege , ingawaje kwa sasa tuna madiwani wengi sana wa
CCM, Mbunge wa Jimbo la Moibara na
wengine wengi nah ii ndio inayotakiwa”alisema Bw Nassari
Awali aliongeza kuwa yeye hana shida yoyote na kiongozi hata
kama ni wa chama chake ila ana shida na viongozi ambao wana mikakati na malengo
mbalimbali ya kuteketeza maslahi ya
wananchi hasa wa jimbo la Arumeru Mashariki na kamwe kiongozi kama huyo
hataweza kumvumilia kwa kuwa hana
msimamo na Taifa
Naye Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye ni Mbunge
wa Mwibara mkoani Mara, bw Kingi Lugora
alisema kuwa ili kukabiliana na hali zote ndani ya nchi wapo baadhi ya viongozi
ambao wanaharibu mpango wa Mungu hasa kwa nyakati za uchaguzi kwa kuwa
wanatumia mabavu ya Rushwa na mara wanapopata uongozi bado wanaendeleza hali ya
Rushwa huku wananchi wa chini nao wakiwa
wanazidi kuumia na hali ngumu ya maisha
“wapo wanasiasa ambao wanawapiga wananchi upofu wa Rushwa na
ndio maaana uchumi wa leo umeyumba huku waumini wa leo wakiwa wanasuasua na kwa
hili naomba makanisa ya sasa yaingie kwenye
maombi dhidi ya hawa watu ambao wanaomba rushwa hasa katika bunge, na
pia napenda kuwatia Moyo hata wabunge ambao
wanajidhatiti na kisha kusema hadharani masuala ya Rushwa wasiogope hata
kama ni makada kama mimi nilivyo kwa
kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao
wanatamani kusema Rushwa lakini wanapata Kigugumizi kwa kuhofia maslahi ya
vyama vyao”aliongeza Bw Lugora.
Pia alisema kuwa yeye kama yeye kamwwe hatasita kusema
ukweli kwa kada yoyote wa CCM ambaye anachangia sana uchumi wa Nchi kuyumba na badala yake
atamuomba Mungu zaidi ili aweze kuwasema na kuwaweka hadharani kwa kuwa mpaka
sasa Mungu anajibu Maombi juu ya mafisadi
ambao ndio chanzo kikubwa sana
cha umaskini ndani ya Nchi ya Tanzania
Katika hatua nyingine Askofu Langaeli Kahaya
naye alisema kuwa wananchi wanapswa kuhakikisha kuwa kamwe hawamchagui
kiongozi yoyote kwa ajili ya maslahi ya Rushwa kwa kuwa wote wanaotoa
rushwa ndio wanaosababisha hata umaskini
na umwagaji damu ndani ya nchi
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni mwiko kwa wananchi wma
Jimbo la Arumeru Mashariki kujihusisha
na Rushwa kwa vipindi vyote vya uchaguzi kwa kuwa mpaka sasa Rushwa imeshaacha
madhara makubwa sana ndani ya jimbo hilo na pia Rushwa ni dhambi kubwa sana.
“ukiangalia sana
mtu anayetoa rushwa ni mtu mwenye elimu yake sasa kwa hili wananchi wanapswa
kujua kuwa anayetoa na anayepokea rushwa anafanya dhambi na hiyo dhambi ndiyo
inayotapakaa kwa jamii na vizazi vingine ambavyo navyo vinaibuka na dhambi hiyohiyo”alisema Bw Kaaya
Mbali na hayo alisema kuwa pia taifa la Tanzania linatakiwa kuhakikisha kuwa kila mara
linakuwa na maombi makubwa sana hasa ya baadhi
ya watu ambao wanatekeleza ahadi za
Rushwa na Ufisadi hali ambayo nayo inachangia ka kiwango kikubwa sana umaskini wa watanzania
wa Leo
Mwisho
chanzo cha habari na Queen Lema, arusha
No comments:
Post a Comment