MBUNGE wa jimbo la arumeru
mashariki Joshua Nasari amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwa na maono mbali
mbali juu ya matumizi bora ya ardhi iliyopo wanayoitaka kutoka kwa
wawekezaji kwa kuhakikisha kuwa ardhi
hiyo inajengwa vyuo vya ufundi na mambo mengineyo ambayo yatawasaidia wao na vizazi vyao vijavyo
Nasari aliyasema hayo alipokuwa
akiongea na wakazi wa jimbo hilo katika
hafla ya kumuaga muhasisis wa kanisa la African Mission Evangelism Askofu
Nickson Issangya iliyofanyika katika kituo cha kulea watoto yatima cha African
Orphanag e kilichopo Sakila wilayani arumeru
Alisema kuwa pamoja na kuwa wana
arumeru wanahitaji ardhi yao kutoka kwa
wawekezaji ,lakini wanapaswa wawe
na maono juu ya matumizi yake kwa kuwa wako ambao wakipewa ardhi
hiyo wanakimbilia kuuza ili wapate fedha.
“Arumeru tuna matatizo mengi hatuna
vyuo vya ufundi ,mji mdogo ,wa usa river hauna hata viwanja vya kuzikia ndugu
waliofariiki,hakuna hata viwanja vya michezo ila endapo mtakuwa na maono mazuri juu ya ardhi hiyo ni wazi
kuwa mtaifanyia mambo makubwa sana ya
maendeleo”alisema Nasari
Aidha akielezea mikakati aliyonayo alisema kuwa ni pamoja na kuhakikisha
anawasaidia watoto yatima na wajane kwa kuwa makundi haya mawili yametekelezwa
bila kukumbukwa hivyo kuwafanya
waonekane wametengwa na jamii.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo
kuwasihi vijana kuachana na makundi ya kupotoshana na badala yake wahakikishe wana kuwa na nidhamu ,maono . na
uwajibikaji mzuri wa kazi kwa kuwa endapo watazingatia mambo hayo yatawafanya
kufanikiwa katika maisha yao.
Nae mhasisisi huyo Nickson Issanya
aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuweka itikadi za kisiasa pembeni na badala
yake wawe na umoja kwa kuhakikisha kuwa wanampa mbunge wao ushirikiano ili
aweze kutimiza malengo aliyojiwekea.
Issangya alisema kuwa endapo
wataendeleza itikadi za kisiasa katika jimbo hilo ni wazi kuwa makundi
hayatavunjika jambo ambalo litasababisha kurudisha nyuma maendeleo ya jimbo
hilo.
mwisho
CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA
0758907891
No comments:
Post a Comment