SAKATA la wachungaji wa kanisa la sabato na uongozi wa
kanisa hilo umechukua sura mpya mara baada ya wachungaji watatu ambao walikuwa
wanashitakiwa kwa makosa ya kudaiwa kurudufu vitabu,kusema kuwa wanatoa muda
kwa kanisa hilo kuomba radhi hata kwenye vyomboi
vya habari na endapo kama watashindwa kufanya
hivyo basi watawapeleka mahakamani.
Akiongea na mjini upako wa habari za ufalme wa mungu kwa niaba ya
wachungaji wengine wawili Dkt Tulla Paul alisema kuwa wameamua kufikia uamuzi
huo kwa kuwa Kanisa hilo
limepotosha umma na pia wameshindwa kufika hata kituo cha polisi ambapo ndipo
waliposhitaki
Dkt Tulla alisema kuwa kwa mara ya tatu tena mfululizo
Walalkamikaji ambao ni kanisa hilo
wameshindwa kufika katika kituo cha kati cha polisi mjini hapa hali ambayo
inafanya hata kesi hiyo ishindwe kupelekwa mahakamani
Alifafanua kuwa kanisa hilo la Sabato ambalo lilisema kuwa lina
ushahidi dhidi ya wachungaji hao kurudufu vitabu vya nabii Hellen .G. White ni
uongo kwa kuwa kanisa ndilo lilorudufu vitabu
“kanisa la Sabato ndilo lilorudufu vitabu na ushaidi
upo kwa maana hiyo basi ni vyema tukaenda mahakamani tukapambane huko huko ila
kama hawataki waombe radhi hadharani kwa kuwa wametuweka katika wakati mgumu
sana na ni sawa na kifungo cha Nje kwa kuwa mara nyingi sana tunahudhuria kituoni
ili kesi iende mahakamani lakini wao hawaji “aliongeza Dkt Tulla
Katika hatua nyingine alisema kuwa tukio hilo ni sawa na uonevu mkubwa sana na hata taasisi nyingine za dini nazo
zinatakiwa kujifunza kitu kwa kuwa wamepoteza muda na rasilimali fedha kwa
ajili ya madai ambayo si ya msingi
Walifafanua kuwa kwa muda wa zaidi ya Miezi mitatu
sasa wamefuatilia kesi hiyo ambayo ni AR/IR/1130/2012 huku shuguli zao za
kueneza injili nayo ikikwama hali ambayo ni kichocheo kikubwa sana cha kukata tama
No comments:
Post a Comment