UKOSEFU WA UPENDO KWA WALIMU CHANZO CHA UTORO MASHULENI
Arusha
IMEELEZWA
kuwa ili wanafunzi wa shule mbalimbali hapa nchini waweze kupenda shule
na kuthamini masomo walimu wanatakiwa kuwa na lugha pamoja na malezi
yenye upendo wa hali ya juu tofauti na sasa ambapo zipo baadhi ya shule
ambazo zina walimu wasiokuwa na upendo.
Aidha kwa sasa wanafunzi wengi watoro wanakwepa shule kwa kuwa
wamekosa matumaini ya upendo toka kwa walimu wao hivyo basi walimu
wanapaswa kubadilika.
hayo yameelezwa na Kanali Mstaafu
John Mongi wakati akizindua rasmi kamati ya bodi ya shule ya St Benedict
Meliyo Primary iliopo maeneo ya Sekei jijini hapa mapema jana.
kanali Mongi alisema kuwa neno upendo linapaswa kutumika sana
ipasavyo na walimu, wakuu wa bodi pamoja na wazazi na kama litaweza
kutumika ipasavyo basi litachangia sana hamasa ya elimu hapa nchini .
aliendelea
kwa kusema kuwa kwa kukosa upendo kwa baadhi ya walimu kumekuwa chanzo
kikubwa sana cha wanafunzi kuona shule kama ni uwanja wa vita na sababu
hiyo hiyo pia imechangia sana hata utoro.
"tujifunze kwenye hizi shule ambazo zinaongoza kitaifa jinsi
ambavyo walimu, bodi za shule zinavyowapenda wanafunzi,kwa hali hiyo
basi mimi nasisiiza kuwa ili elimu iweze kufika katika kiwango cha juu
lazima kwanza walimu wawe na upendo na wanafunzi ambao
wanawafundisha"aliongeza Kanali Mongi.
hataivyo aliwataka nao walimu mbali na kuhamasiaha upendo kwa
wanafuzni ili kuweza kuepukana na majanga ya utoro shuleni lakini pia
muda ambao wanakuwa na wanafunzi wao wahakikishe kuwa wanawaambia juu ya
madhara yaliopo hapa nchini kama vile mdondoko wa maadili ili kuweza
kuokoa kizazi cha vijana ambacho kwa sasa kinaangamia.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Joseph Laiser alisema
kuwa ili kufanya elimu hapa nchini iweze kufikia katika kiwango ambacho
kinaitajika tayari shule hiyo imeweka mikakati ya kuwapa semina wazazi ,
pamoja na viongozi mbalimbali wa shule hiyo .
Laiser alifafanua kuwa kwa kuwapa semina wazazi, walezi, na
viongozi wa shule kutaweza kusaidia walengwa wa watoto hao kujua
majukumu yao kwani kwa sasa shule nyingi zinashindwa kutekeleza majukumu
yake kwa kuwa wanakwamishwa na vitu mbalimbali likiwemo suala zima la
wazazi pamoja na walezi .
MWISHO
No comments:
Post a Comment