WANAWAKE wapatao 33 kutoka tarafa ya
Manyara, wilayani Monduli, mkoa wa Arusha wamenufaika na elimu ya ujasiliamali,
Afya ya uzazi, stadi za maisha na ukimwi iliyotolewa na shirika lisilo la
kiserikali kutoka nchini Ujerumani liitwalo DSW.
Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika kwenye
eneo la Mto-wa-Mbu, na kuwashirikisha wataalam kutoka Mradi wa Kuwawezesha
Wanawake na Wasichana (WOGE)
Akizungumza
juzi, mmoja wa wakufunzi kutoka
mradi wa WOGE, Daudi Tano alisema: “Lengo la mafunzo hayo ni kumjengea
uwezo
mwanamke ili aweze kujitambua yeye kama yeye,mambo muhimu ya kufanya
kwenye jamii,pamoja na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi
Mtaalam huyo alisema mafunzo hayo yalilenga
kumkomboa mwanamke kutokana na changamoto nyingi anazakabiliana nazo katika
maisha yake ya kila siku.
Alifanunua kuwa WOGE ni mradi wa kikanda
ambao unatekelezwa kwenye nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia ukilenga
zaidi kuwakwamua wanawake na wasichana walioko pembezoni hasa wale wa vijijini.
Nchini Tanzania
“Mradi unawalenga zaidi wanawake wa vijijini
walio na umri kati ya miaka 16 na 55, ambao wapo kwenye ajira isiyo rasmi na
ambao hawapo shuleni ama hawana ajira,” alisema,
Pia aliongeza kuwa madhumuni ya
mradi huo ni kutoa mchango katika jitihada za kupambana na umaskini kwa
kuwawezesha wanawake na wasichana ili waweze kusimama wao wenyewe kichumi na
kutokuwa wategemezi.
Naye Afisa ustawi wa jamii Tarafa ya Manyara,
Denis Magiye alilishukuru shirika la DSW kwa elimu hiyo na kuyataka mashirika
mashirika mengine kuiga mfano huo ili kumkomboa mwanamke na msichana wa
Kitanzania.
Alisema elimu ya uzazi inahitajika sana
katika nyakati hizi kwani uzazi wa mpango humpatia mwanamke uhuru wa kufanya
shughuli zake za kuinua kipato cha familia.
“Kuzifahamu njia za uzazi wa mpango
kutawasaidia hata kupunguza idadi idadi ya watoto ambao hawajatarajia kuwapata
na pia kupunguza vifo vinavyotokana na masuala ya uzazi,” alisema.
MWISHO
No comments:
Post a Comment