FANYENI KAZI KWA BIDII ILI
MUONGEZE UFANISI WA BENKI YETU-MKURUGENZI ACB
Na MWANDISHI WETU,ARUSHA
IMEELEZWA kuwa endapo
kama watendaji wa Benki ya Akiba watafanya
kazi kwa bidii basi wataweza kuruhusu ushindani wa kibenki hivyo kuweza kutoa
ruhusa hasa kwa wateja wake kunufaika na huduma mbalimbali zikwemo huduma za
Mikopo
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba
hapa nchini John Lwande,wakati akiongea na wafanyakazi wa benki hiyo kutoka
katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro mapema wiki hii
Aidha Lwande alisema kuwa
ipo haja ya wafanyakazi wa Benki kuhakikisha kuwa kamwe hawasababishi
dosari zozote za kibenki kwa kuwa kwa sasa kuna wimbi kubwa sana la huduma hizo na badala yake wanatakiwa
kuwafanya wateja waridhike na huduma za kibenki hasa kwenye Mikopo
Alifafanua kuwa endapo kama watafanya hivyo basi watakuwa ni
miongoni mwa chanzo kikubwa sana cha kufanya
mabadiliko ndani ya Nchi ya Tanzania
kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania wataendelea kutumia huduma hizo za
Kibenki kwa ajili ya maslahi ya Jamii zao
Akiongelea Suala la Mikopo kwa watanzania alisema kuwa kwa sasa wanajiopanga kuhakikisha kuwa
wanaongeza kiasi cha Mikopo ili kuweza kuwafikia watanzania walio wengi zaidi
tena hasa wa Mikoa ya Dodoma na Mwanza ambapo wanatarajia kufungua matawi mengi zaidi kwa maslahi ya shuguli za kibenki
kwa wananchi wa mikoa hiyo.
Alimalizia kwa kusema kuwa pamoja na kuweka mikakati ya
kufungua matawi ambayo yataweza kuwasaidia wananchi kwenye masuala ya Kifedha
lakini pia Benki hiyo kwa Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro kwa kipindi cha mwaka 2012 waliweza kuvuka
malengo hali ambayo imeweza kuinua mapato ya Benki hiyo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment