ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI ZAIDI ACHANENI NA HABARI ZA
SEMINA NA MIKUTANO- MWOLEKA
Na Gladness Mushi,Arusha
WAANDISHI wa habari hapa Nchini wameaswa kuhakikisha kuwa
wanajiwekea utatibu wa kuandika zaidi habari za uchunguzi kuliko kurtegemea
habari za semina na mikutano kwani habari za mikutano na semina bado hazitoi
majawabu na changamoto kwa jamii
Endapo kama waandishi wa habari wa Tanzania wataweza kujiwekea utaribu wa kuandika
habari ambazo zina uchunguzi wa kutosha basi watakuwa ni chanzo kikubwa sana cha maendeleo ya Nchi
Hayo yalielezwa Jana na Anjelo Mwoleka ambaye ni Mkurugenzi
wa Jambo Arusha Publisher wakati akiongea na wahitimu wa fani ya uandishi wa
habari katika chuo cha uandishi wa habari Arusha (AJTC) katika maafali ya sita
ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.
Aidha Mwoleka alisema kuwa kwa sasa kuna wimbi kubwa la
waandishi wa habari a wanajihusisha zaidi na masuala ya habari za Semina na
kuachana na habari za kiuchunguzi hali ambayo wakati mwingine ina nyima haki za
msingi za jamii kwa kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa sana ya kuibua maovu
yanaoendelea kwenye Jamii
Alifafanua kuwa habari za uchunguzi ndani ya Nchi ya Tanzania ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hivyo basi wana
habari hawapswi kukimbia na badala yake wanapswa kuzipa kipaumbele kikubwa ili
kuweza kuruhusu changamoto kwenye sekta zote kujilikana
“kuwa mwandishi wa habari sio lazima uwe unajua ratiba za
mikutano za kila siku bali kuna maana kuwa unapaswa kujua na kutambua kuwa
unatakiwa lkuwa mchunguzi na hapo ndio kazi yako itakuwa na manufaa makubwa
sana kwa jamii hivyo basi habari za muhimu zinatakiwa kupewa kipaumbele tena
kikubwa sana ili nchi ya Tanzania iweze kufika mahali ambapo inatakiwa kufika
kama zilivyo nchi nyingine ambazo zimeendelea duniani”aliongeza Mwoleka
Awali wahitimu wa mafunzo hayo ya uandishi wa habari katika
ngazi ya cheti, na shahada walisema kuwa pamoja na kuwa chuo hicho kimewalea
katika maadili mazuri lakini bado wanakabiliwa na uhaba wa vifaa kama vile
Kompyuta, na Kamera kwa ajili ya mazoezi.
No comments:
Post a Comment