KESI YA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ALIYEUWAWA
BURKINAFASO KUANZA KUSIKILIZWA KATIKA MAHAKAMA YA AFRIKA
Na Queen Lema,Arusha.
Mahakama ya juu ya
haki za binadamu inatarajia kuanza kusikiliza rasmi kesi iyaokabili Serikali ya
bukinafaso juu ya mauaji ya Mwandishi wa habari za Uchunguzi Nobert Zongo pamoja
na wenzake watatu wakati wakiwa kazini December
13 mwaka 1998
Akiongea na Vyombo
vya habari mapema jana jijini hapa Afisa habari wa mahakama hiyo Bw jean
Pierre alisema
kuwa Kesi hiyo itaanza kusikilizwa kuanzia March saba na nane mwaka huu
Jean alisema kuwa kesi hiyo ambayo inaikabili Serikali ya
burkinafaso itaweza kusikilizwa na Majaji 11 wa mahakama hiyo huku upande kwa Upande wa wanasheria wakitoka katika Nchi za Nigeria na Burkifaso ambao wanasimama kama wanasheria wa walalamikaji
“kesi hii itaendeshwa kisasa zaidi ambapo jopo la majaji
wetu watasikiliza na kisha kuharisha kwa mujibu wa sheria za mahakama yetu hivyo mara baada ya kuhairisha kesi hiyo basi
watataja siku nyingine ya kusikilizwa tena’aliongeza Jean
Katika hatua nyingine alisema kuwa pia mahakama hiyo kupitia
kwa Raisi wake Sophia Akufye inatarajia kumuapisha jaji Aba Kimelabaou kutoka
Burkinafaso kama Jaji wa mahakama hiyo mara baada ya jaji Nyamihala Mulenga wa
nchini Uganda
kufariki dunia
Alisema kuwa Raisi wa Mahakama hiyo atapisha jaji huyo March
4 katika mahakama hiyo na kisha kuhudhuriwa na majaji 10 kutoka nchi mbalimbali
duniani huku lengo likiwa ni kuongezea nguvu mahakama hiyo.
“March 4 mwaka huu tutamuapisha jaji huyu rasmi kama jaji halali kwa ajili ya shuguli mbalimbali za
mahakama yetu hivyo pia wadau mbalimbali wa mahakama hii nao watakuwepo pamoja
na viongozi wengine ili kuweza kushuhudia kitu ambacho kinaendelea siku
hiyo”aliongeza Jean
MWISHO
No comments:
Post a Comment