VIONGOZI WA DINI WAKUTANA ARUSHA KWA AJILI YA KUOMBA
AMANI KWA NCHI ZA EAC
Na Queen Lema,Arusha
Viongozi wa dini wakiwemo wachungaji zaidi ya 400 kutoka
katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wamekutana Jijini Arusha katika
Kongamano kwa ajili ya kujadili mambo
mbalimbali ya uongozi wao pamoja na kuombea nchi hizo amani hasa ya Nchi ya Kenya na Tanzania.
Akiongea na “Majira”jana mratibu wa kongamano hilo ambalo
limeandaliwa na mtandao wa wachungaji mkoa wa Arusha,Bw Geofrey Ayo alisema
kuwa kongamano hilo lina manufaa makubwa sana kwa Nchi hizo
Ayo alisema kuwa amani ya nchi inatakiwa ipite hata kwa
viongozi wa dini kwa kuwa wao wana nafasin kubwa sana ya kuweza kuhubiri amani tofauti na
viongozi wengine wowote hivyo basi mtandao huo umechukua nafasi hiyo kwa ajili
ya kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na amani
Alisema kuwa wachungaji hao zaidi ya 400 ambao wamekutana
Jijini Arusha wameweza kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na hata jinsi
ya kulinda amani ambayo baadhi ya Nchi imepotea kwa sababu mbalimbali hivyo
kupitia kwa waumini wao wataweza kuwafanya wananchi walinde amani
“tumekutana hapa kuhakikisha kuwa tunajadili mambo
mbalimbali ya msingi lakini pia kuhakikisha kuwa kila Kiongozi anakuwa balozi
wa kulinda amani na wala sio kwenye serikali kwani sisi Viongozi wa dini tuna
nafasi kubwa sana ya kutekeleza suala hilo ambalo wakati
mwingine tunaachia Serikali pekee’aliongeza Ayo
Mbali na hayo aliwataka Viongozi wa dini kuhakikisha kuwa
wanajiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa mbali na kuomba amani kwa nchi husika
lakini watumie nafasi mbalimbali ambazo wanazo kwa kuwataka waumini wao waweze
kufanya kazi kwa bidii na kisha kupambana na Umaskini
Alifafanua kuwa kama Viongozi wa dini wataweza kufanya hivyo
basi wataweza kuondoa Mataifa ya jumuiya ya Afrika ya Mashariki hususan Tanzania kutoka katika hali ya umaskini ambayo ipo na kufika katika
viwango vya hali ya juu ambapo hata hali ya ugumu wa maisha wakati mwingine
inachangia sana
uharibifu wa amani, pamoja na umaskini.
“kwa sasa kuna changamoto kubwa sana za masuala ya kimaisha lakini viongozi
wa dini wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kusisisitiza watu
wahakikishe kuwa wanafanya kazi na waache kukaa kaaa ovyo mitaani na pindi
wanapokaa mitaani ndipo wanapofanya na kuwaza hata mbinu za kuharibu
amani’aliongeza Ayo
MWISHO.
No comments:
Post a Comment