TANZANIA
INAHITAJI NYUMBA MILIONI TATU –NHC
Na Queen Lema,Arusha
TANZANIA
ina mahitaji ya Nyumba Milioni Tatu ambapo kwa
sasa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeweka mikakati ya kuhakikisha
kila mwaka inajenga nyumba zaidi ya elfu tatu ili kupunguza tatizo hilo hapa Nchini
Hayo yamelezwa na Waziri wa Ardhi,nyumba, na maendeleo ya
makazi,Profesa Anna Tibaijuka leo wakati akizundua mradi wa nyumba za makazi
katika eneo la Levolosi ambazo zimejengwa chini ya Shirika la nyumba
Tibaijuka alisema kuwa mahitaji hayo ya nyumba kila mwaka
yanaongezeka kwa kiasi cha nyumba laki tatu lakini ongezeko hilo
ni lazima liweze kupunguzwa tena kwa haraka sana kwa kubuni aina mbalimbali ya nyumba
ambazo zitarahisisha makazi bora na imara
Aliongeza kuwa Hitaji ni kubwa sana
la nyumba hapa nchini hivyo jitiada za haraka sana zinahitajika katika kuhakikisha kuwa
hata nyumba ambazo zinajengwa ziweze kuwa imara na ziweze kuwasaidia hata zaidi
wananchi wa vijiijini ambao mara nyingine wanaonekana kukosa nyumba bora na
imara
Alisema kuwa kama Shirika hilo amblo kinaendeshwa lenyewe
litaweza kuwa bunifu na kujenga nyumba nyingi zaidi basi litachangia kwa
kiwango kikubwa sana ongezeko hilo la nyumba zaidi ya Laki tatu kwa kila mwaka
kuweza kupungua na hata baadhi ya miji kuweza kupangika kwa uraisi sana
“Tanzania kwa sasa tunakabiliwa na changamoto hii lakini ni
vema sasa Shirika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tukahakikisha kuwa
tunasonga mbele zaidi na hata kuangalia jinsi ya kupunguza tatizo hilo ambalo
kama halitaaweza kutatuliwa kwa uraisi basi litasababisha madhara kwa kuwa wapo
baadhi ya watu ambao watakosa sehemu za kuishi’aliongeza Tibaijuka
Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wanasiasa wana nafasi
kubwa sana ya kushirikiana na Shirika hilo kwa kuwa bado shirika hilo
linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile kushindwa kujenga kutokana na
Ardhi ambayo inauwza kwa bei ya juu sana lakini kama watasaidiana basi wataweza
kutatua changamoto hiyo ambayo nayo inafanya shirika hilo kushindwa kuendelea
kujenga nyumba nyingi zaidi
Awali mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo
Nehemia Mchechu alisema kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo
la ongezeko la mahitaji ya Nyumba hapa
Nchini Shirika hilo
limeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa mpaka 2014 watakuwa tayari
wameshajenga nyumba elfu kumi na tano huku kila mwaka wakijenga nyumba elfu
tatu
Mbali na hayo alisema kuwa kwa Mkoa wa Arusha wanatarajia
kuanza kujenga nyumba za garama nafuu katika wilaya ya Arumeru pamoja na Arusha
huku lengo halisi likiwa ni kuhakikisha kuwa mji wa Arusha unaendelea kuboreka
zaidi kwenye hadhi za kimataifa na kuachana na ujenzi holela ambao mara
nyingine unasababisha ukosefu wa nyumba
MWISHO
No comments:
Post a Comment