Tuesday, May 22, 2012

ADUMU NA UJAUZITO KWA MIAKA MINNE, AZAA MARA KUMI NA SABA



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Bi Chausiku Sulemani mkazi wa Maji ya chai wilayani Meru mkoani hapa amewaomba wataalamu mbalimbali wa afya pamoja na wachungji mbalimbali  kuweza kumsaidia kuchunguza kizazi chake kwa kuwa mpaka sasa ana uzao wa 17 huku mimba ya 17 ikiwa imedumu tumboni kwa miaka minne

Akiongea na UPAKO WA HABARI YA UFALME WA MUNGU wiki hii  bi Chausiku alieleza kuwa amekaa na Mimba hiyo kwa kipindi cha miaka minne sasa bila kujifungua huku kiumbe kikiwa kinaendelea kukua ndani ya Tumbo lake hali ambayo inamuweka katika njia panda na kusababisha kuomba msaada wa wachungaji  na watumishi wa Mungu kwa kuwa hali hiyo inamtesa  sana

Alifafanua kuwa hali hiyo ya kuwa na uzao wa 17 imewafanya watoto ambao wapo hai 13 kukosa maitaji yao ya Muhimu kama watoto hali ambayo wasamaria wema wanatakiwa kuiangalia kwa undani sana

Alieleza kuwa pamoja na kuweza kwenda kwa watalaamu mbalimbali wa afya katika hospitali za Arusha na Kilimanjaro lakini bado hali yake inaendeleea kuwa hiyohiyo ya kupata ujauzito wakati ni mzazi

Aliongeza kuwa kwa sasa kinachoitajika ili aweze kuoko maisha ya kiumbe ambacho kimo ndani ya Tumbo lake ni kupatiwa fedha za upasuaji (Oparesheni) hasa pale wakati utakapofika sanjari na kuweza kuwasaidia watoto wake katika mchakato wa Elimu

“Wakristo wenzangu naombeni mnisaidie jamani nina uzao wa kumi na saba sasa huku nikiwa bado nina mimba kubwa hivi sasa naishije watumishi wa Mungu kwa lolote lile nipo tayari kwa kuwa watoto nao wanaishi maisha ya shida sana baba yao hawezi kuwalea kwa kuwa ni wengi na watoto hawa pia wanalazimika hata kulala chini kwa ajili ya ukosefu wa vitanda”aliongeza Bi Chausiku

Naye diwani wa kata hiyo ya Maji ya Chai,bw Lotti Nnko alisema kuwa mama huyo ambaye kila mwaka anahistoria ya kuzaa bila kukutana na Mwanaume anaitaji msaaada wa hali ya juu kwa kuwa familia ambayo anailea nayo inamlemea kutokana na uhaba wa Kipato.

Bw Nnko alifafanua kuwa hali hiyo inachangia kwa kiwango cha hali ya juu sana watoto wake kukosa maitaji kama lishe hali ambayo nayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana kushindwa kuendelea mbele na maisha ya kila siku hasa katika mchakato wa Elimu

Aliwataka Wasamaria wema kuhakikisha kuwa hawaachi watoto wa mama huyo kuendelea kupata shida ya uhaba wa lishe, maitaji muhimu ya shule, pamoja na sehemu ya kulala kwa kuwa hata nyumba wanayolala haina Milango wala Madirisha.


Diwani huyo aliwataka wakristo na watumishi wa Mungu kutumia Vipaumbele mbalimbali ambavyo vimo hata kwenye biblia kwa kuweza kumsaidia mama huyo hata kwa njia ya mambi pamoja na kuweza kupata kiasi cha Laki Tano ili aweze kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine tena 

KWA YEYOTE ATAKAYEGUSWA NA MAMA HUYO ASIISITE KUMSAIDIA KUPITIA NAMBA 0764650288
MWISHO

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA,ARUSHA

0758907891

No comments:

Post a Comment