Na Queen Lema, Arusha
Waziri wa nchi,ofisi ya rais na utumishi George Mkuchika
ameishauri wizara ya elimu kutoa elimu dhidi ya mapambano ya rushwa kwa
wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu ili kuwawezesha
kutambua madhara yanayotokana na rushwa.
Mkuchika aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika
ufunguzi wa mkutano wa nchi za umoja wa Afrika zinazopambana na rushwa unaoendelea jijini hapa
Alisema kuwa endapo kama elimu ya rushwa itaweza kutolewa
mashuleni kuanzia ngazi za awali itawezesha kupunguza kasi ya rushwa kwa
nchi husika na hivyo taifa husika kupata haki zake za msingi
Aliongeza kuwa watu wengi wanatoa rushwa kwa kushindwa
kufahamu haki zao za msingi hivyo elimu hiyo ikitolewa kuqnzia ngazi za
chini itapunguza vitendo vya rushwa ambavyo vimekithiri kwa baadhi ya
nchi.
Alitolea mfano nchi za Norway na Sweden ambazo zimekuwa
zikitoa elimu ya rushwa kuanzia ngazi za chini mpaka vyuo vikuu ambapo
imesaidia kila mtu katika nchi hizo rushwa kuwa adui wao.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Takukuru hapa nchini
Valentine Mlowola alisema kuwa kutokana na rushwa kukithiri hapa
tanzania wamefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 14 kwa kipindi
cha mwaka huu ambazo zilikuwa zikitumika kwenye rushwa.
Alidai kuwa kwa sasa rushwa imekuwa tatizo la kimataifa
hivyo kupitia mkutano huo wa umoja wa nchi za afrika wataweza kupanga
mikakati ya kupunguza tatizo la rushwa katika nchi hizo.