Monday, May 6, 2013

ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI ZAIDI ACHANENI NA HABARI ZA SEMINA NA MIKUTANO- MWOLEKA

ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI ZAIDI ACHANENI NA HABARI ZA SEMINA NA
MIKUTANO- MWOLEKA

WAANDISHI wa habari hapa Nchini wameaswa kuhakikisha kuwa wanajiwekea
utatibu wa kuandika zaidi habari za uchunguzi kuliko kurtegemea habari
za semina na mikutano kwani habari za mikutano na semina bado hazitoi
majawabu na changamoto kwa jamii

Endapo kama waandishi wa habari wa Tanzania wataweza kujiwekea utaribu
wa kuandika habari ambazo zina uchunguzi wa kutosha basi watakuwa ni
chanzo kikubwa sana cha maendeleo ya Nchi

Hayo yalielezwa Jana na Anjelo Mwoleka ambaye ni Mkurugenzi wa Jambo
Arusha Publisher wakati  akiongea na wahitimu wa fani ya uandishi wa
habari katika chuo cha uandishi wa habari Arusha (AJTC) katika maafali
ya sita ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.

Aidha Mwoleka alisema kuwa kwa sasa kuna wimbi kubwa la waandishi wa
habari a wanajihusisha zaidi na masuala ya habari za Semina na
kuachana na habari za kiuchunguzi hali ambayo wakati mwingine ina
nyima haki za msingi za jamii kwa kuwa waandishi wa habari wana nafasi
kubwa sana ya kuibua maovu yanaoendelea kwenye Jamii

Alifafanua kuwa habari za uchunguzi ndani ya Nchi ya Tanzania ni
muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hivyo basi wana habari hawapswi
kukimbia na badala yake wanapswa kuzipa kipaumbele kikubwa ili kuweza
kuruhusu changamoto kwenye sekta zote kujilikana

“kuwa mwandishi wa habari sio lazima uwe unajua ratiba za mikutano za
kila siku bali kuna maana kuwa unapaswa kujua na kutambua kuwa
unatakiwa lkuwa mchunguzi na hapo ndio kazi yako itakuwa na manufaa
makubwa sana kwa jamii hivyo basi habari za muhimu zinatakiwa kupewa
kipaumbele tena kikubwa sana ili nchi ya Tanzania iweze kufika mahali
ambapo inatakiwa kufika kama zilivyo nchi nyingine ambazo zimeendelea
duniani”aliongeza Mwoleka

Pia alisema kuwa ili wana habari waweze kufika malengo yao mbalimbali
wanapaswa kujiepusha na rushwa pindi wanapokuwa kazini kwani Rushwa
husababisha sana baadhi ya wananchi kukosa haki ya habari hapa nchini
hivyo kuruhusu wimbi kubwa sana la udanganyifu

Alifafanua kuwa endapo kama watakimbia Rushwa basi watachangia hata
wale watenda maovu kwenye jamii kuweza kuonekana kwa haraka sana hivyo
mlengwa wa haki ataweza kupata tofauti na pale ambapo watajihusisha na
rushwa

Awali wahitimu wa mafunzo hayo ya uandishi wa habari katika ngazi ya
cheti, na shahada walisema kuwa pamoja na kuwa chuo hicho kimewalea
katika maadili mazuri lakini bado wanakabiliwa na uhaba wa vifaa kama
vile Kompyuta, na Kamera kwa ajili ya mazoezi.

No comments:

Post a Comment