Na Queen Lema, MERU
UGONJWA WA MAHINDI KUTOKA KENYA WAWAATHIRI WANANCHI KATA YA KIKWE MERU
ZAIDI ya Hekari 300 kutoka katika kata ya Kikwe Wilayani Meru mkoania
Arusha zimeharibiwa vibaya na ugonjwa mahindi kutoka Nchini Kenya
unaojulikana kama ugonjwa wa kusinyaa kwa mahindi hali ambayo itafanya
wakulima washindwe kupata mahindi wakati wa mavuno
Akiongea na “patapata”mapema jana diwani wa kata hiyo bw Emanuel
Silayo alisema kuwa hali hiyo ya ugonjwa ambayo imekumba kata hiyo ya
Kikwe inaashiria njaa kubwa sana kwa kuwa mazao ya mahindi shambani
hakuna huku wakulima wakiwa wameshapanda
Silayo alisema kuwa Miezi michache iliyopita wakulima waliweza kupanda
mazao ya nafaka hasa mahindi lakini baada ya mahindi kuchomoza
yalianza kushambuliwa na ugonjwa hadi kufa
Alisema kuwa pamoja na kuwa mahindi hayo yamekufa wakati wakulimna
wengi wamepanda kwa ajili ya mategemeo ya chakula katika eneo hilo la
Kikwe lakini mahindi machache sana yameweza kusalia hali ambayo bado
ni kiashirio kikubwa sana cha Njaa
Alifafanua kuwa kama tahadhari haitaweza kuchukuliwa kwa haraka sana
basi huenda wakati wa mavuno ndani ya mwaka huu kusiwe na mavuno
kabisa hivyo baa la njaa kuweza kutawala katika Wilaya hiyo ya Meru.
Akiongelea Ugonjwa huo wa mahindi kutoka nchini Kenya Afisa Kilimo
Wilaya ya Meru,Grace Solomoni alisema kuwa ugonjwa huo ni hatari sana
kwa kuwa unashambulia zao la mahindi hadi kufa lakini bado mkulima
anaweza kupata angalau kiasi kidogo
Grace alisema kuwa kwa mujibu wa taararibui za kilimo mara baada ya
shamba kuathiriwa na ugonjwa huo shamba linapswa kupumzishwa kwa
kipindi cha miaka mitatu ili vijidudu vife lakini kama wakulima
wataendelea kulima basi watasababisha vijidudu hivyo kuzaliana kwa
wingi sana
No comments:
Post a Comment