NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
SERIKALI imeshauriwa kuhakikisha kuwa inaweka mtaala wa
mabadiliko ya tabia ya nchi kuanzia ngazi ya shule za msingi ili kuweza
kukabiliana na majanga mbalimbali ambayo yanaikumbaa nchi ya Tanzania lakini pia ulimwengu mzima
kwa sasa.
Kauli hiyo imetolewa na Bw Peter Mroso ambaye ni Mwenyekiti
wa Klabu ya Green Social education(GRESOE) kutoka katika chuo kikuu cha Mt Meru
wakati akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa chuo hicho katika mdahalo wa
wanafunzi wa vyuo vikuu Arusha uliofanyika chuoni hapo mapema jana.
Mroso alisema kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya wasomi
wanafanya kujisomea mambo mbalimbali ambayo yanahusu mabadliko tabia nchi
ingawaje kwa sasa nchi inateketea kutokana na majanga hayo hivyo kuna umuhimu
mkubwa sana wa
kuwepo na mitaala ambayo inahusu mabadiliko tabia Nchi
Aliendelea kwa kusema kuwa endapo kama mitaala ya Tanzania ingeweza kuwa na somo la mabadiliko ya
tabia ya nchi basi hata wanafunzi wenyewe wangweza kuwa mabalozi wazuri sana wa masuala hayo ya
mabadiliko tabia ya nchi
Amebainisha kuwa njia hiyo ya kuongeza somo la mabadiliko ya
tabia ya nchi litaweza kuifanya Tanzania
kuepukana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuweza
kurudisha hali kama ilivyokuwa hapo mwanzo
Mbali na hayo alidai kuwa nayo serikali inatakiwa
kuhakikisha kuwa inaweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuwasaidia wananchi wake
kwani tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya wananchi bado
hawajajua vema masuala ya mabadiliko tabia nchi
Alimalizia kwa kuwataka nao wasomi kutoka katika vyuo vikuu
mbalimbali kuweza kujiweka utaratibuw a kufanya midhalo lakini kuelimisha umma
juu ya hatua ambazo zinaweza kutumika ili kupambana na mabadiliko tabia nchi
ambayo wakati mwingine ndiyo chanzo cha umaskini hata kwenye vyuo vikuu
mbalimbali hapa nchini.
Mwisho
No comments:
Post a Comment