Thursday, January 30, 2014
KATA ZA WILAYA YA KARATU ZATAKIWA KUANZISHA MIRADI ILI KUONGEZA UCHUMI KUANZIA NGAZI YA KAYA
Na Queen Lema, KARATU
CHAMA cha mapinduzi Wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha kimeagiza uongozi
wa kata zote ndani ya Wilaya hiyo kuhakikisha kuwa inabuni miradi ya
maendeleo ambayo itawasaidia wananchi kuweza kujiongezea kipato lakini
pia kuweza kuondokana na umaskini katika kata zao
Hayo yameelezwa na Katibu wa chama hicho kwa wilaya ya Karatu, Bi Elly
Minja wakati akiongea kwenye harambee ya ujenzi wa jengo la Kitega
uchumi ambalo lipo wilayani humo ambapo pia harambee hiyo ilienda
sanjari na mazoezi mengine mengi ya kuazimisha kuzaliwa kwa CCM hapa
nchini
Bi Elly alisema kuwa kuna haja sasa ya kila kata kuhakikisha kuwa
inakuwa na miradi tena endelevu ambayo itaweza kuwasaidia wananchi
kuondokana na dhana ya umaskini ambayo ikwa sasa ni tishio kubwa sana
kwenye baadhi ya familia.
Alifafanua kuwa miradi hiyo ambayo inatakiwa kubuniwa na wananchi kwa
kushirikiana na viongozi wa kata mbali na kuweza kuwaokoa wananchi
kwenye suala zima la umaskini lakini pia itachangia sana kuongezeka
kwa uchumi wa wilaya hiyo ya Karatu.
Mbali na uanzishwaji wa miradi kwenye kata zote za Karatu pia alisema
kuwa kwa upande wa Jengo la Kitega uchumi lililopo Karatu nalo
litaweza kuwasiaida sana wananchi katika kuboresha uchumi wao lakini
pia litakuwa na faida sana
"uwepo wa jengo hilo la kitega uchumi hapa Karatu ni ishara kuwa sasa
uchumi wa mji wa karatu utaongezeka sana na utaweza kuwasaidia sana
wananchi wa eneo hili hivyo basi wananchi wanatakiwa watumie fursa
ambazo zipo zaidi na sisi tutaendelea kuwa wabunifu zaidi kwa ajili ya
kuweza kuwasaidia wananchi wetu hususani kwenye suala zima la Uchumi
wao wa kila siku"aliongeza Bi Elly
Aliwataka wananchi wa Wilaya hiyo ya Karatu kuhakikisha kuwa
wanaendelea kutumia vema fursa za maendeleo ambazo zinatolewa na
chama hicho lakini pia wasikubali kupotoshwa juu ya jitiada ambazo
zinafanywa na baadhi ya watu wasiope4nda maendeleo ya jamii nzima
Hataivyo Harambee hiyo ilienda sanjari na mazoezi mbalimbali kama vile
ya upandaji miti,ufanyaji wa usafi wa mazingira pamoja na matembezi
ikiwa ni maazimisho ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment