WAZIRI KABAKA AZINDUA RASMI MCHAKATO WA MAANDALIZI YA USHIRIKI WA WAJHASIRIA MALI .......
Waziri wa Kazi na
Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka
leo tarehe 19/09/2013, amezindua rasmi mchakato
wa maandalizi ya ushiriki wa Wajasiria
mali wa Tanzania katika Maonesho ya 14 ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo
kama Nguvu kazi/Jua kali.
Maonesho hayo
yaliyoanza kufanyika mwaka 1999 jijini Arusha Tanzania wakati wa kusainiwa mkataba wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki yameendelea kufanyika kila mwaka kwa mzunguko
katika nchi ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dhumuni kuu la
maonesho haya ni kuwezesha sekta isiyo
rasmi kukua na kurasimisha shughuli zao katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa
kuwapatia fursa Wajasiriamali wa sekta hii kuonesha bidhaa zao, kukutana na
wenzao, kubadilishana taarifa, ujuzi, kukuza masoko ya bidhaa na huduma pamoja
na kuwezesha kupanuka kibiashara.
Jumla ya
Wajasiriamali 1,070 kutoka nchi tano za
Jumuiya ya Afrika Mashariki wanategemewa kushiriki na Tanzania
inatarajiwa kupeleka washiriki 250.
Mhe. Waziri
Kabaka amesema,ili kurahisisha na kuharakisha ushiriki wa Wajasiriamali wa
Tanzania katika maonesho hayo, kuna swala la usajili, na fomu za usajili pamoja
na vigezo vya kuangalia kabla ya kujaza fomu ambavyo vinapatikana kwenye Tovuti ya Wizara ambayo ni www.kazi.go.tz
IMETOLEWA
Ridhiwan.M.Wema
Msemaji
No comments:
Post a Comment