Sunday, September 22, 2013

MAASKOFU NCHINI WASHAURIWA KUSEMA UKWELI JUU YA MADAWA YA KULEVYA

MAASKOFU NCHINI WASHAURIWA KUSEMA UKWELI JUU YA MADAWA YA KULEVYA



Na Bety Alex, Arusha



Viongozi wa dini hasa maaskofu wameshauriwa kuhakikisha kuwa kamwe
hawaogopi kusema ukweli juu ya biashara ya madawa ya kulevya ambayo
inaendelea hapa nchini na kama hawatasema ukweli na kisha kuelezea
umma juu ya madhara ya kujihusisha na biashara hiyo basi Tanzania
itaweza kuyumba sana



Kwa sasa wapo baadhi ya watanzania ambao wanasingizia umaskini na
kisha kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya bila kujua
na kutambua kuwa wanaweka nchi kwenye sifa mbaya



Hayo yameelezwa na Askofu Mstaafu wa kanisa la Angikan Jijini
Arusha,Simon Makundi wakati wa kuwaingiza rasmi Viongozi wa dayosisi
ya Arusha katika Kanisa la Tanzania Methodist Church lilopo njiro
jijini Arusha mapema jana.



Askofu Makundi alisema kuwa inasahangza sana kuona kuwa wimbi kubwa la
watanzzania bado wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya biashara
haramu ya madawa ya kulevya ingawaje viongozi wa dini wapo hapa nchini



Alisema, viongozi wa dini wana nafasi kubwa sana ya kuhakikisha kuwa
wanakemea masuala hayo kwani wao wana nafasi nzuri sana ya kukuytana
na wananchi kila siku na kila juma tofauti na viongozi wa serikali
ambao ni mara chache sana.



“kwa sasa hii biashara inaonekana kufanywa na watu wengi sana na kama
viongozi wa dini hasa ninyi mnaoitwa maaskofu mtaendelea kukaa kimya
mtakuwa hamtendi haki kabisa kwenye jamii na badala yake hii biashara
itazidi kushamiri hapa nchini’alisema Askofu Makundi



Wakati huohuo Askofu Mteule wa kanisa hilo la Tanzania Methodist
Church jimbo la Arusha Dkt Izack Sarakikya alisema kuwa uwepo wa
kanisa hilo kwa mkoa wa Arusha utaweza kuraisisha shuguli mbalimbali
za kidini lakini pia za kijamii kwani bado jamii inakabiliwa na
changamoto nyingi sana



Alifafanua kuwa Kanisa hilo lina huduma maalumu ya kungalia majanga
ndani ya Nchi ya Tanzania hasa yale ambayo yanawakumba viongozi wa
dini mbalimbali lakini pia hata yatima na wajane



Alimalizia kwa kusema kuwa huduma ya kanisa hilo ambayo itawafikia
watu wenye mahitaji mbalimbali pia itaweza kuwakumbuka hata viongozi
mbalimbali wa dini ambao wakati mwingine wanasahulika kwa kuwa tayari
ni wastaafu au ni wazee jambo ambalo sio hazina ya taifa la Tanzania


No comments:

Post a Comment