Saturday, September 28, 2013

WAFADHILI WATOA MSAADA WA MILIONI 90 KWA AJILI YA MRADI WA WATOTO




Shule ya Ngorika Happy watoto School iliopo katika kitongoji cha Ngorika Tarafa ya Kingori Wilayani Meru mkoani Arusha imefanikiwa kupewa Mradi wa shamba lenye hekari nane huku likiwa na tahamani ya Milioni 90 kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima waliopo katika shule lakini pia kuachana na tabia ya kuwa tegemezi.

Aidha Mradi huo wa shamba upo katika eneo  Lerai Kati ambapo mradi huo umetolewa na wafadhili wa Kitanzania (Friends of Tanzania)hivi karibuni ili ikuwajengea uwezo wa kuwasiaida yatima lakini pia kujiimarisha zaidi

Akiongelea mradi huo katika maafala ya kwanza ya shule hiyo wiki iliyopita mkuu wa shule hiyo Edward Mwololo alisema kuwa wafadhili hao waliamua kukunua mradi huo ili kuweza kusaidia shule hiyo dhidi ya ukosefu wa mahitaji ya chakula

Aidha alidai kuwa mpaka sasaivi mradi huo umeweza kuwasaidia sana wanafunzi ambao wengine ni Yatima wale wanaotokea katika mazingira magumu kwa kuweza kupata vyakula mbalimbali kama vile mboga kwa uraisi sana tofauti na hapo awali ambapo shule hiyo ilikuwa haina mradi huo

Wakati huohuo amedai kuwa ni vema kama baadhi ya shule ambazo zipo chini ya wafadhili mbalimbali lakini pia ambazo zinawahudumia Yatima na wale waliotoka katika mazingira kuhakikisha kuwa wanakuwa wabunifu lakini pia miradi ambayo wamepewa waweze kuitumia vizuri

Alidai kwa kufanya hivyo kutaweza kuruhusu hata watoto yatima wenyewe kuepukana na tabia ya kuwa tegemezi na badala yake watahakikisha kuwa wanaweza kujishugulisha kwa maslahi ya maisha yao ya hapo baadaye lakini pia kwa maslahi ya taifa zima

“tunapswa kujua na kutambua kuwa ipo siku masuala ya ufadhili yatakoma lakini kama yatakoma na miradi ambayo tumepewa tunaiweza kuihudumia vizuri basi tutaweza kupiga hatua ya hali yajuu sana na pia ni muhimu hata kuwajengea hawa yatima pamoja na wale ambao wanatokea katika mazingira magumu kuannza kujitegemea na kuacha kutegemea zaidi misaada’aliongeza hivyo

Awali akielezea changamoto ambazo zinaikabili shule hiyo ambayo asilimia kubwa ya wanafaunzi wake ni Yatima alidai kuwa mpaka sasa wanafunzi katika shule hiyo hawana uhakika wa kupata maji safi na salama kwa kuwa eneo hilo limekosa maji kwa muda mrefu sasa.

“kwa kipindi cha miaka mitatu sasa tumekosa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi hapa shuleni hivyyo basi tunaomba serikali iweze kushirikiana na sisis katika kuhakikisha kuwa tunapata maji kwani maji tunayotumia sasa ndio hayo yanwasababishishia watoto wetu magonjwa kwani floride iliopo katika maji hayop ni kubwa sana”aliongeza mkuu huyo.


No comments:

Post a Comment