TUMIENI KAMUSI HATA MNAPOKUWA MADHABAHUNI-JOKA KUU
Na Bety Alex,Arusha
Mchungaji Herbert Anthony”Joka kuu”amewataka watumishi wa
Mungu kuhakikisha kuwa wanafundisha masomo yao ya kila siku kwa waumini wakiwa
na uhakika wa maneno lakini kama hawana uhakika basi wahakikishe kuwa wanatumia
kamusi ili kujiepusha na tabia ya kupotosha maana ambazo wakati mwingine
zinachangia sana kumtukuza Shetani kwa siri.
Kwa sasa hata unaposema neno unatakiwa kujua maana ya lile
neno ambalo umelisema kwa kuwa maneno ya sasa yanachukuliwa kivingine
kabisa lakini kama
mtumishi wa Mungu unashindwa kujua na
kutambua maana basi tumia hata kamusi
Joka kuu aliyasema hayo jijini hapa wakati akiongea na
waumini wa kanisa hilo
mapema wiki hii katika somo lilolokuwa
lina husuurejesho wa afya ambapo alidai kuwa hata maneno ya sasa yanatakiwa
kuchunguzwa kabla ya kutamkwa
Alidai kuwa kwa kutumia kamusi kutaweza kuwafundisha
wakristo maneno ambayo yana maana lakini
kama watumishi wa mungu watakuwa wanachukua
maneno bila ya kuyachuja kutasababisha mafundisho ambayo wanayatoa kwenye ibada
zao ya bure huku watu wakizidi kuangamia
zaidi katika dhambi
“dunia ya sasa kwa kweli imebadilika sana hivyo basi kuliko uhubiri neno ambalo
hujui maana yake ni bora unyamaze kimya kabisa unakuta mtumishi anasema kuwa
ninyi ni wajanja akijua kuwa mjanja ni mtu mwenye kiwango bora kumbe neno
mjanja linamaanisha mtu tapeli tapeli,sasa hapa unaona kuwa shetani anaweeza
kutawala badala Mungu aweze
kutawala”aliongeza Joka kuu
Awali akiongelea somo
hilo la Urejesho wa afya ndani ya jamii ya sasa
alidai kuwa Tanzania ya leo
imekumbwa na magonjwa mengi sana
kwa kuwa wengi wamesahau kweli ya Mungu tofauti na Miaka iliyiopita ambapo
magonjwa hayo wakati mwingine chanzo chake kikubwa ni Dhambi
Alifafafnua kuwa dhambi zinapozidi maali basi kinachofuata
hapa ni magonjwa na mateso ya kila siku
lakini kwa sasa wakristo pamoja na watanzania kwa ujumla wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanarejea katika torati ya bwana ili bwana mwenyewe aweze kupunguza kasi
ya magonjwa ambayo ndio umaskani wa baadhi ya watu.
“ukiangalia kwenye vyombo vya habari ubakutana na mambo na
unyama wa hali ya juu sana ambao unafanywa na watu ambao mwisho wake huishia
kusababisha kilema cha ugonjwa sasa
inabidi wakristo tuamke na tukatae hali kama hizi na badala yake turudi
katika torati’aliongeza Joka kuu
Alimalizia kwa
kuwataka wakrsito wahakikishe kuwa wanafanya urejesho na kuachana na tabia ya
kuchukulia lugha na mambo mengine
kiraisi bali wahakikishe kuwa wana ishi vema ikiwa ni pamoja na kutojihusishaa
na dhambi ambazo ambazo ndizo zinazozaa maovu katika dunia
MWISHO
No comments:
Post a Comment