INSERT KWA KUSHIRIKIANA NA JUKWAA LA WAZEE LATARAJIA KUJENGA
KITUO CHA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA
Asasi ya Informal Sector team(INSERT)Kikiana na jukwaa
la wazee wa mkoa wa Arusha wanatarajia
kujenga kituo kwa ajili ya makazi ya wazee ambapo kituo hicho kitagarimu kiasi
cha zaidi ya Milioni 150 huku lengo likiwa ni kusaidia wazee ambao hawana uwezo
ndani ya mkoa wa Arusha
Akizungumza katika jukwaa la wazee wa mji wa Arusha (JUWA)
mratibu wa jukwaa hilo bw Javes Sauni alisema kuwa mpaka sasa kuna
mikakati mbalimbali ya kuanza marra moja ujenzi wa kituo hicho cha wazee kwa
mkoa wa Arusha
Alitaja kuwa mikakayi hiyo inasema kuwa kituo hicho cha
wazee kitajengwa katika eneo la Kisongo ambapo kituo hicho kwa mara ya kwanza
kitaweza kuhudumia wazee zaidi ya 60
hasa wale ambao wanatoka katika mazingira magumu
Aliongeza kuwa endapo kama mpango huo wa hivi karibuni
utaweza kufikiwa tena kwa haraka basi utaweza kuwa na faida kubwa sana kwa wazee wa mkoa wa
Arusha kwa kuwa baadhi yao wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku
wengine nao wakiwa wanakabiliwa na
ukosefu wa mahala pa kuishi
“hili jukwaa la wazee limeona kuwa upo umuhimu tena mkubwa
sana wa kuhakikisha kuwa tunaangalia zaidi maslahi ya wazee hasa wale ambao
wanatokea katika mazingira magumu lakini njia mojawapo ya kuweza kuwasaidia
wazee hawa ni kuhakikisha kuwa kwa kiasi Fulani wanakuwa na kituo ambacho kama
sio kukutanika pale na kuongea masuala yao ya wazee lakini pia kitasadiia sana
kuokoa maisha ya wengi”aliongeza Sauni
Wakati huo huo alisema kuwa kwa sasa bado asilimia kubwa sana ya wazee hasa wa mji wa Arusha wanakabiliwa na
changamoto kubwa sana
ya matibabu hali ambayo wakati mwingine husababisha vilema vya kudumu au vifo
hasa kwa wazee ambao wanatoka katika familia ambazo hazina uwezo
Pia alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo watatumia
jukwaaa la wazee kwa kuhakikisha kuwa wanatafuta mbinu mbadala ambazo zitaweza
kuwaokoa wazee hasa wale ambao hawana uwezo wa kujitibu ikiwa ni pamoja na
kukosa hata fedha kwa ajili ya manunuzi ya dawa
“hii ni changamoto kubwa sana ambayo inawakabili wazee wa
mkoa wa Arusha lakini tutatafuta mbinu mbadala na kuhakikisha kuwa wazee
wanapata matibabu kwa kuwa tayari Serikali ilishatoa Agizo lakini vituo vya
afya vya Mjini hapa bado havitekelezi
sera hiyo pamoja na Tamko hilo”alifafanua
Bw Sauni
No comments:
Post a Comment